Ahukumiwa kwenda jela miaka 4 kwa kumuua mkewe baada ya kumfumania na jirani yake

Ahukumiwa kwenda jela miaka 4 kwa kumuua mkewe baada ya kumfumania na jirani yake

mwanamkee analetaa mwanaumee ajee amgongeee kitandani kwa mume wake??? aisee ilibdi hata huyo jamaa aliefumaniwaa awee kuzimuu muda huuu..
 
1686571280643.png

Mahakama ya Mkoa wa Tabora, imemuhukumu Kwenda jela miaka minne Juma Edward (30), Mkazi wa kijiji cha Shitage wilayani Uyui mkoani humo kwa kumuuwa mkewe Kulwa Vincent (29) kwa kumshambulia hadi kufa baada ya kumfumania akifanya ngono na mwanaume mwingine ambae ni jirani yao nyumbani kwake.

Akitoa adhabu hiyo leo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Tabora Jovith Kato, amesema kwamba katika shitaka hilo mwanamke alijitakia mwenyewe kwa kukutwa akiwa na mwanaume mwingine ambaye sio mume wake ni jirani yao, na wamekuwa wakifanya hivyo zaidi ya mara mbili.

Hakimu huyo amesema kwamba Mahakama hiyo imeona impunguzie adhabu hiyo kuto kifungo cha maisha hadi miaka minne kwa sababu aliweza kukubali shitaka lake na hakuisumbua mahakama kwamba alikiri kufanya mauaji hayo.

Kato katika hukumu hiyo alisema kwamba mshitakiwa alikuwa gerezaji kwa muda wa miaka7, hivyo Mahakama inajicho la huruma kutokana na kukaa kwake na kukiri shitaka lake lililokuwa likimkabiri la mauaji ya bila kukusudia kupitia kifungu cha sheria cha 195 na cha 198 ambacho ndio kilitumika dhidi yake.

Hapo awali mshitakiwa katika Mahakama hiyo aliweza kukiri kufanya mauaji na hakuweza kuisumbua Mahakama hiyo ndio maana imemuonea huruma kutokana na kuwa na uchungu baada ya kumfumania mke wake akiwa na mwanaume mwingine ambae ni jirani yao katika kitanda chake.

Mshitakiwa Juma Edward alikiri kufanya mauaji ya mke wake kutokana alikuwa na hasira lakini hakujua kama kitatokea kifo alijua anamuonya tu na sio kumuuwa.
 
KATAA NDOA
NDOA ITAKUPELEKA JELA
NDOA INAFILISI
NDOA NI ADUI WA MAENDELEO

KATAA NDOA KWA MAENDELEO YAKO.
MKuu ndugu zangu wengi baada ya kuoa na kufunga ndoa walifilisika.... Wengine wanadai walitumia gharama kubwa kwenye maandalizi ya ndoa,wengine wanadai baada ya ndoa walibebeshwa majukumu makubwa kwenye familia ya mkewe n.k ,..Sasa najiuliza ivi ni hayo au kuna mengine yaliyo wafilisi baada tu ya kufunga ndoa?
 
miaka 7 maana yake alifanya hilo tukio hilo 2016 akiwa na miaka 23 au naona kama umechanganya mambo
 
Hata hiyo miaka minne ni mingi pia!Angeachwa huru tu.

Lulu alimuua hawara yake kanumba bila kukusudia hukumu yake alipewa miaka miwili tu. Na jela akakaa mwaka mmoja tu kisha akatolewa kwa msamaha wa Rais kabla hata hajaingia mwaka wa pili jela.

Huyu jamaa kamuua mke wake kwenye fumanizi.. hukumu yake jela miaka minne na hapo hapo ameshakaa mahabusu miaka 7. Jumla miaka 11 gerezani
 
Dah! Hakuna mtihani mgumu kwa mwanaume katika ndoa kama huu wa kumfumania mke wako akichepuka. Tena na jirani yako!! 🙁
 
Lulu alimuua hawara yake kanumba bila kukusudia hukumu yake alipewa miaka miwili tu. Na jela akakaa mwaka mmoja tu kisha akatolewa kwa msamaha wa Rais kabla hata hajaingia mwaka wa pili jela.

Huyu jamaa kamuua mke wake kwenye fumanizi.. hukumu yake jela miaka minne na hapo hapo ameshakaa mahabusu miaka 7. Jumla miaka 11 gerezani
Inahuzunisha sana.
 
Back
Top Bottom