Aaaah huyo ni katili sana..Kuna siku atamcharanga vipande....Huko njombe wanakunywa Nini mbona wendawazimu sana?
Dah, acha niwape story moja alafu utaona jinsi watu wanavyopelekewa kua na roho za kikatili..,
Kisa kama hiki kimewahi kumtokea swahiba wangu, mke wake alikua pasua kichwa, kuna siku nimeenda nae kwake, kufika tunakuta watoto wao wawili wako nje, mama kaondoka na kafunga nyumba, mtoto mmoja anatambaa mwingine anamiaka minne (4). Nyumba ilikua mpya, maeneo yale hakuna majirani karibu, japo kuna fence fupi ya maua.
Nilikaa pale mpaka saa1, kiza kinaingia, niliondoka mke wake hajarudi, kikawaida tulikua tunatoka nae kazin mida ya saa3 kwaiyo kumbe ndo hua kawaida ya uyo mwanamke kutupa watoto hapo anaondoka. (Zingatia ni watoto wake kabisa)
Huyo mwanamke akili zake ni kama unavyomuona gigy, ni kama copy yake.
Kuna kipindi alindoka na watoto akapotea, kumbe kaenda kupanga na kibwana chake huko (kisiri), maisha yavowashinda, akampeleka jamaa yangu ustawi, ili wale pesa za matunzo, swahiba wangu alikubali ila akasema ataoa mke mwingine, yule mama kusikia ivo akafunga safari akarudi akasema ye ndo mke na ndo mama mwenye nyumba, kama vipi apewe taraka ila yeye abaki na nyumba kwajili ya watoto au nyumba ipigwe bei kilamtu apite njia yake, jamangu akaghailisha kuoa, akamwacha ili watoto wakue kwanza.
Sasa nasikia siku moja wamegombana, jamaa akapiga yule mwanamke haswa, sasa mwanamke kumkomoa jamaa kumbe alienda kwa bwana yake, “ alipokua anakaa kipindi kaondoka na watoto “. Yan kaenda akamwambia amfi*re then usiku huo huo akaenda hospital kuchukua vyelelezo kua kafanyiwa ukatiri, kapigwa na mme wake then kaingiliwa kinyume na maumbile.
Hasubui tupo kazini na jamaa, wakaja wazee wakazi na defender lao, wakamuulizia, boss akamwita, sijui waliongea nini, nikaona jamaa anapigwa pingu anaingizwa kwenye defender yao, na huo ndo ulikua mwisho wa kunwona swahiba wangu.
Nilivokuja kusikia kesi yenyewe ndo ile aah nikajua kabisa jamaa katengenezewa sababu alishanambia hua halali chumba kimoja na yule mwanamke, na pia kwa mwili wa yule mwanamke na ubabe wake hawezi kufanyiwa kitendo na uyo jamangu.
Nilikuja kupata habari jamaa kapigwa nyundo sijui miaka mingapi jela na sijui kama alishatoka au lah.
Kwaiyo, sio wote unaosikia wamehukumiwa ni kweli wamefanya hayo makosa, na sio wote unaosikia wamefanya ukatili ukawaona hawana akili, kuna mda maisha na wanadamu wanakutia wendawazimu akili zinazima, unafanya mambo usitotegemea kufanya.