Ai IMEDONDOSHA BOMU LA NUCLEAR! 💣🔥 Mtu mmoja atumia Ai kutengeneza mbadala wa software za Adobe bure - Photoshop, Premiere Pro, Illustrator, n.k.

Ai IMEDONDOSHA BOMU LA NUCLEAR! 💣🔥 Mtu mmoja atumia Ai kutengeneza mbadala wa software za Adobe bure - Photoshop, Premiere Pro, Illustrator, n.k.

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Adobe imekuwa ikilalamikiwa na baadhi ya watumiaji wake kutokana na gharama za usajili na ada za kughairi huduma.

Brandon Thomas ametumia uwezo wa AI kutengeneza programu zinazolenga kuchukua nafasi ya bidhaa mbalimbali za Adobe zitazokuwa bure na wazi, bila kuhitaji kulipia usajili. Watumiaji wanaweza kupakua code, kuibadilisha na kuchangia maboresho.

Thomas amesema alitumia AI ya Claude Opus 5.5 kutoka Anthropic kusaidia kujenga programu hizo.

Kupitia mradi unaoitwa ArtCraft, Brandon Thomas ametumia AI kufanya reverse engineering na kujenga programu saba ambazo zinafanana na programu maarufu za Adobe.

Programu hizo ni pamoja na:

  • Photocraft — mbadala wa Photoshop.
  • Vectorcraft — mbadala wa Illustrator.
  • Filmcraft — mbadala wa Premiere Pro.
  • Lightcraft — mbadala wa Lightroom.
  • Effectcraft — mbadala wa After Effects.
  • Designcraft — mbadala wa InDesign.
  • Printcraft — mbadala wa Acrobat Pro.

Pia, anaamini kuwa mradi huo unaweza kufikia kiwango cha kufanana kwa uwezo na programu za Adobe kwa asilimia 100 ndani ya mwezi mmoja lengo kubwa ambalo bado linahitaji kuthibitishwa.

Hii inaonyesha jinsi AI inavyorahisisha utengenezaji wa software na kuwezesha developer kujenga programu ambazo hapo awali zingehitaji timu kubwa na muda mwingi.


View: https://www.reddit.com/r/SaaS/comments/1wwnhbt/ive_created_open_source_100_rust_cleanroom/

 
Hii inaonyesha jinsi AI inavyoweza kurahisisha utengenezaji wa software na uwezo mkubwa wa kujenga software ambazo hapo awali zingehitaji timu kubwa.

Brandon Thomas ametumia AI kutengeneza mbadala wa software 7 za Adobe akitumia Ai kupitia mradi unaoitwa ArtCraft.

Mradi huo una apps zinazolenga kuchukua nafasi ya Photoshop, Illustrator, Premiere Pro, Lightroom, After Effects, InDesign na Acrobat Pro.

Kilichovutia zaidi ni kwamba apps hizi ni bure, zipo wazi, zinapatikana bure, na zimekusudiwa kufanya kazi kwenye Windows, macOS na Linux.

Hata hivyo, bado ziko kwenye hatua za mwanzo za maendeleo, hivyo kuna changamoto za bugs, utendaji na baadhi ya features ambazo hazijakamilika.
PUMBA TUPU UNAONGEA HAPA HATA LINK HUNA
 
Back
Top Bottom