Hii inaonyesha jinsi AI inavyoweza kurahisisha utengenezaji wa software na uwezo mkubwa wa kujenga software ambazo hapo awali zingehitaji timu kubwa.
Brandon Thomas ametumia AI kutengeneza mbadala wa software 7 za Adobe akitumia Ai kupitia mradi unaoitwa ArtCraft.
Mradi huo una apps zinazolenga kuchukua nafasi ya Photoshop, Illustrator, Premiere Pro, Lightroom, After Effects, InDesign na Acrobat Pro.
Kilichovutia zaidi ni kwamba apps hizi ni bure, zipo wazi, zinapatikana bure, na zimekusudiwa kufanya kazi kwenye Windows, macOS na Linux.
Hata hivyo, bado ziko kwenye hatua za mwanzo za maendeleo, hivyo kuna changamoto za bugs, utendaji na baadhi ya features ambazo hazijakamilika.