100 others
JF-Expert Member
- Aug 5, 2017
- 10,825
- 38,702
Nchini Marekani mwigizaji maarufu wa filamu ya Ant Man and the Wasp, Evangeline Lilly(pichani), amefunguka kuhusu hali ya sintofahamu inayoendelea studios kubwa za filamu kupunguza wafanya kazi na nafasi zao kuchukuliwa na AI.
Inadaiwa kuwa Disney sasa imeanza kutumia teknolojia ya AI kuchukua nafasi za wasanii na wabunifu, Disney wanatumia mifumo ya AI kufanya kazi hizo kwa gharama nafuu na haraka zaidi. Wamepunguza watu takribani watu 1000.
Evangeline Lilly amethibitisha kuwa mbunifu maarufu, Andy Park aliyehusika kubuni suti ya Wasp(kama uliona filamu ya Ant Man and The Wasp, yale mavazi huyu Andy Park ndiye mbunifu) na wahusika wengine wengi wa Marvel, naye ameachishwa kazi.
Hali hii inakuja wakati kukiwa na hofu kubwa Hollywood kuhusu AI.
Kiukweli ukitizama movie ambazo AI inatengeneza kwa sasa, hali inatisha sana, AI sio poa wazee.
Hollywood nao wamefikiwa.
SAG-AFTRA, ambao ni umoja wa waigizaji na wasanii wa redio wenye wanachama zaidi ya laki moja na nusu. wamekuwa wakipambana kishujaa kuhakikisha kuwa haki za waigizaji hazipotei, hasa baada ya mgomo wao wa kihistoria wa mwaka 2023 uliotingisha studio kubwa kama Disney na Netflix. Sababu kubwa ya mapambano haya imekuwa ni kulinda maslahi ya binadamu dhidi ya kasi ya kukua kwa Akili Bandia (AI).