AI yaanza kuchukua nafasi za watu Marvel na Disney; wasanii wakubwa wapigwa chini

Mkuu kuna projects zinakuja kwa wafanya kazi kwenye makampuni ya ujenzi na migodi kuanza kutumia AI robots, yale madude hayana bima ya afya, haki za mfanya kazi , hata launch beak hakuna , hata likizo hakuna , hayaumwi na yanafanya kazi masaa 24 siku 7 za wiki bila kupumzika, hii itapunguza gharama ya uendeshaji wa kampuni kwa kiwango kikubwa sana na kufanya kazi ziende kwa haraka kitu ambacho kampuni nyingi zitafanya hivyo kwa sababau mwisho wa siku wanachoangalia ni faida.

Binadamu anaanza kunekana liability/mzigo..

Tujiulize, nani atabaki salama?
 
Kama itafikia hiyo hatua, basi ajira kwenye sekta ya ujenzi itakuwa changamoto

Bora tumezeeka, hadi hizo robots zimefike Tanzania, basi tutakuwa tumeshakufa na kufa
 
Muvi gan hiyo?
 
Usanii tu....
 
Kuna AI robot zina jenga nyumba
Kuna hizo robot za zinaitwa Optimus.. wanaotengeneaz ni kampuni ya Elon Musk na gharama yake ni milioni 80 hivi, Tshs(30,000 USD) zinfanya mambo ya ajabu. Elon anasema ataanza kuziuza 2027 mwishoni hivi sasa zinafanya kazi kwenye viwanda vya Elon Musk, spaceX, Tesla. AIse niliangalia hadi nikaogopa.

View: https://www.youtube.com/watch?v=Sdz21k-X7gc
 
Mkuu sijui tunapoelekea..
Unaona kazi inayofanywa na Midjourney ilivyo ya hatari. Alafu AI inafundishika kwa kasi sana.

Claude imetumika na US kuandaa mashambulizi ya Venezuela na Iran. Kwahiyo hata kwenye majeshi nako pataguswa. Ukizingatia suicide drones zimepunguza uhitaji wa artillery crew, drone operator mmoja anafanya kazi ya reconnaissance unit nzima tena kwa gharama nafuu na kuondoa hatari.

Jet drones zitaendeshwa kwa AI na kuweza kufanya dogfights na hivyo marubani hawatotumika sana. 6th generation fighter itakuwa na uwezo wa kuendeshwa na rubani au AI, au rubani anaendesha fighter moja ila inaongoza drones kadhaa (loyal wingmen) kwenye manned-unmanned teaming.

Kila mtu atafikiwa.
 
Mliingizwa kwenye mfumo mkajaa , sasa ni maumivu . wenyewe waafrika wanaandaa makongamano a AI , vitu vya kuletewa vinaenda kuwageuza . Wanasiasa watabaki juu b
 
Kama Sisi watunzi wa riwaya ndio kabisa. AI katunyuka fimbo. Mpaka unasikia uvivu kuandika stori.

Maana AI ukimwambia akuandikie stori anakupa chuma kilichonyooka.
Kazi yako ni kumpa Idea, kufanya story twist, lakini kwenye kusuka mpangilio wa visa na sentensi AI NI habari nyingine

Haya kwenye Proposal na Design sidhani Siku hizi kama kuna mtu anaajiri watu wa design na graphics. Sijui Proposal


Kwenye Nyimbo, sijui Muvi ndio kabisa.

Ndio maana wenye akili wote sasa hivi akili zao wamehamishia kwenye Ardhi, mashamba makubwa wakijiandaa na miaka 20 ijayo
 
Hatutaki AI
 
Lakini mwisho wa siku nani atakuwa mlaji wa kazi/huduma ya AI bila ya uwepo wa binadamu? Manna kwa namna inavyoongelewa kwenye huu uzi ni kama vile existence ya mwandamu itakuwa limited sana. Nadhani sayansi imegeuka kuwa hatari kuliko hatari yenyewe ya njaa na kutoelimika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…