Brainwashed
New Member
- Sep 3, 2022
- 1
- 0
Uongozi ndiyo kiini cha mafanikio au anguko la jamii yeyote ile. Hakuna jamii, tasisi, kampuni hata taifa ambalo mafanikio yake au anguko lake halihusishwi na uongozi wake uliyopita au uliyopo sasa.
Wengi wetu tunakubalina na dhana hii, na ndiyo sababu tunakuwa wepesi kuwaanyooshea vidole vya lawama viongozi wetu pale mambo yanapokwenda kombo na kuwapigia makofi pale unapofanya vizuri. Kwakuwa tuna amini wanajibu juu ya usalama, amani, mafanikio na usawa katika jamii zetu.
Siku zote wanapofanya vizuri ni mara chache sana huwa tuna hoji, ubora wa sheria zetu, sera zetu na ubora, uimara, ufanisi na uhuru wa nifumo yetu ya kiutawala. Ila pale wanaposhindwa, ndipo tunaponza kuhoji, sheria zetu, sera zetu na mifumo yetu kama ni bora au la. Na hatuiishi hapo tu, uhawa tunahoji hata mambo binafsi ya viongozi hao.
Kama vile kiwango chao cha elimu, ufaulu wao, kozi waliyosoma, shule walizosoma, tuna hoji familia zao, marafiki zao n.k. ili mradi tupate kuhalalisha kushindwa kwake na msingi wa lawama zetu.
Lakini tukumbuke kuwa viongozi wazuri au wabaya duniani kote, katika siku zilizopita au za sasa hawakuwa wabaya kwasababu ya sheria dhaifu, sera mbaya au mifumo mibovu. Sijui kama hili umewahi kulifikiri, lakini na kushawishi kuwa huu ndiyo ukweli. Sheria nzuri haitengezi kiongozi nzuri, zina leta usawa tu kati ya kiongozi na watu, na kati ya mtu na mtu.
Sera nzuri hazimfanyi kiongozi kuwa mzuri, ila zinatengeneza msingi mzuri wa shunghili za kimaendeleo na za kimaisha za watu. Kadhalika na mifumo mizuri, rahisisha utendaji au kuleta ufanisi wa kuitendaji kati ya serikali na watu.
Vitu hivi vitatu (sheria, sera na mifumo bora) ni vya muhimu sana, wala hakuna mjadala katika hilo, ila huwa vinaathiriwa mara nyingi na aina ya kiongozi anaye vitumia kuliko vyenyewe kuadhiri uongozi wake.
Kwa mfano, kulikuwa na tafauti gani katika sheria, sera na mifumo ya kiutawala, kati ya marais hawa watatu wote wanatoka chama kimoja. Kikwete, Magufuli na Samia. Naomba utazame kwa uangalifu zaidi kati ya Magufuli na Samia, zile Sheria zilizotungwa na bunge ilikukidhi mahitaji yake( Magufuli) ambazo wengi hawakukbaliana nazo, hazijabadilishwa, lakini kwa nini watu wanahisi haueni kubwa sasa wakati wa mama Samia ukilinganisha wakati wa Dk Magufuli.
Sijaribu kusema huu ni uongozi bora kuliko ule mwingine na jaribu kuangazia kile nincho kiona katika jamii juu ya viongozi hawa wawili, ili kukuonyesha kile ambacho mara nyingi huwa tunakisahau.
Mfano mwingine, ni kwa raisi wa sasa wazambia, anawezaje kufanya anayo yafanya kwa tofauti kubwa na watangulizi wake, ikiwa sheria za nchi ni zile zile na mifumo ya kiutawala ni ile ile?
WATOTO TU NDIYO UZALIWA
Nilisoma habari moja mahali Fulani, kuhusiana na matalii moja. Katika kusafiri kwake alifika katika kijiji kimoja porini sana. Akiwa katika kijiji aliweza kukutana na mmoja kati ya wazee waliyo heshimika kwa busara zao katika kijiji hicho.
Mtalii alimuuliza maswali kadhaa mzee huyo ilipata taswira ya kijiji hicho, moja ya maswali aliyo uliza ni hili “ Je kuna mtu yeyote hodari au maarufu amewahi kuzaliwa katika kijiji hichi?”
“Hapana, katika jijichi huzaliwa watoto tu”, alijibu mzee.
Maana yake ni hii, uhodari au umaarufu mtu azaliwi nao, unatengenezwa.
Viongozi wazuri hawazaliwi, hawapatikani kama ajali viongozi wazuri wanatengenezwa, wanajengwa, wanaandaliwa, wanalelewa. Tusipofanya juhudi za makusudi kuwaandaa iongozi wazuri itakuwa shida kuondoa tatizo la uongozi.
Ilikuvunja mnyororo wa uongozi mbaya ni lazima kuanza kuwandaa viongozi mapema.
Napenda kupongeza jitihada za kupaza sauti zinazofanywa na asasi mbali mbali zisizo za kiserikali na vyama mbadala, juu ya utawala unao zingatia sheria, sera na mifumo bora. Uelimishaji, uwezeshwaji watu juu ya ushiriki katika shughuli mbalimbali za kisiasa, na uhamasishaji vyote hivi ni muhimu kuendelezwa, lakini mabadiliko ya kudumu au endelevu yatatokana na uwekezaji kwa njia ya malezi na mafunzo mbali mbali ya uongozi, uadilifu na uzalendo kwa watoto na vijana.
Kama tunaamini juu ya kuwandaa watoto wakiwa wadogo ili ili wawe na maisha bora kuliko sisi wazazi, kama tunawanda watoto wajekuwa wanasayansi bora, wanamichezo bora, kwa nini tusiwandae kujakuwa viongozi bora, siyo wanasiasa bora, viongozi bora.
ili taifa ilipige hatua kubwa kimaendeleo ya watu na vitu, tuna hitaji viongozi wazuri, wenye maono, maadili, uzalendo na wachapaji kazi. Vitu ambavyo hujengwa tangu utoto, kwa njia ya malezi na mafundisho.
Kumbuka hili; viongozi wetu wanatoka kwenye jamii, na kwenye familia zetu
Nina amini haiba, tabia na maono ya viongozi yana nguvu kubwa katika kuathiri aina ya uongozi wao na hatma ya nchi kuliko hata sera na sheria za nchi. Na hili ndilo jambo ambalo huwa mara nyingi tuna lisahau, kuwa malezi ya watoto na vijana ni moja ya mfumo bora ya kuandaa viongozi bora.
Hoja hii halisi sana hapa kwetu ukizingatia sensa ya 2012 inayosema 77% ya watanzania ni watoto na vijana(www.nbs.go.tz).
Ni kweli kuwa hili ni gumu lakini linawezakana, ni kweli litachukuwa muda lakini wakati si ukuta. Tuanze sasa pasina kuacha harakati nyingine zinazoendelea za kuimarisha utawala bora.
Nigharama kulifanya jambo hili, lakini pia itatugharimu zaidi tusipo fanya hivyo

Upvote
0