Mwaka ajana naenda Uwanja wa andege moja wapo wa Kimataifa hapa Tanzania, naondoka na Halotel yangu.
Nafika Uwanjani no Cellphone internet lakini pia Wife ya uwanjani ni mbovu kupita maelezo.
Hata kupost ujumbe whatsapp haiwezi.
Tunaelekea Dubai-hapo Airpot internet yake ni ya maajabu, speed ambayo sijawahi kushuhudia.
Nikajiuliza hivi sisi wafrika kwanini tuko nyuma kila kitu. Wale Mainjinia wa Viwanja vya ndege, wafanyakazi, mafundi wa ICT n.k hakuna anayeona hili au hawatembei kujifunza kwa wengine?
Nakaa Dubai siku Tatu baadae naelekea Uturki Instabul very wonderful services.
Nikarudi Tena Nyumbani nikadhani labda siku ile mtandao ulikuwa mbovu......nakutana wasafiri wanalalamikia Internet mbovu mtu hata ndugu yake anashindwa kuwasiliana.
Viwanja vyetu vinapokea maelfu ya wageni kutoka duniani kote. Kukosa internet ya uhakika kwa watu kuwasiliana ni aibu kubwa sana.