Aibu: Air Tanzania yalalamikiwa kuchelewesha abiria na kisha kuwakodia hoteli ya hadhi ya chini

Huku vivuko havifanyi kazi huku nauli za ndege ni ghali kwenda mpanda nauli yake ni sawa na kwenda dubai🤣🤣🤣mara abiria wawacheleweshe na kuwapeleke hotel za efu tatu tatu.Mara waziri kawaba kibali wahuni wenye mtaji wa milion 50 waaginze sukari ya billion 6.Hebu nile mm viazi na maziwa hapa nikiwaza sana ntakufa bure.
 
Mtanzania wee mwambie kukata
Mauno,udaku,uchawa
Huoni sahv kila kijana mtoto wao ni kukata unoooo na mamizikimiziki tu

Ova
 
Mwendokasi imekufa kwa sababu ya wingi wa abiria tumerudi kwenye Daladala, Kivuko cha Kigamboni kimekufa kwa sababu ya wingi wa abiria tumerudi kwenye Mitumbwi na ATCL itakufa kwa sababu ya wingi wa abiria tutarudi kwenye mabasi. Treni ya mwendokasi nayo itakufa ni jambo la muda tu.

Ni Tanzania pekee ambapo biashara hufa kwa sababu ya wingi wa wateja. Yaani biashara za Tanzania zinaelemewa na wateja hadi zinakufa.

Chini ya utawala wa CCM tusitegemee chochote cha maana watafanya. Miaka 60+ ya ufukara, rushwa, ufisadi chini ya CCM.
Angalia hoteli ATCL waliyopeleka watu Vingunguti.

View: https://x.com/cleosexxy/status/1803374356669640755?s=19
 
Air Tanzania was3ng3 sana, kuna siku nilipaswa niingie Mwanza saa 6 usiku kutokea Dar, matokeo yake nilifika saa 11 alfajiri, mwaka huu huu, hapo nauli nimetoa 700K. Nimekaa kwenye ndege nikachoka ikabidi nitoke nje, nilikuwa natoka narudi nakuta bado nawauliza jamani hatuondoki? narudi tena nje naendelea kupiga mitungi narudi tena ndani... wanasema wanapaka rangi ndege... Jamaa wapuuzi sana..
 
Wanapaka rangi Ndege ndio nini?
 
Eti bwana kama imechelewa kwa bahati Mbaya kuna ulazima wa kulipia Vyumba watu? Mbona tunalala airport hata nchi zingine?
Kuna muda fulani ukifika ni lazima uwapatie abiria chakula na malazi hio ni sheria za IATA, ila kwenye process hii ni wajanja wanapiga. Kwahio kucheleweshwa abiria wa ATCL ni mrAdi wa wapigaji.
 

Haina mantiki wala haichekeshi stori yako
 

Bado tuna viongozi ambao wanadhani Internet ni anasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…