Aibu: Anayetafsiri Uwanja wa Jamhuri kamati hakujiandaa

Aibu: Anayetafsiri Uwanja wa Jamhuri kamati hakujiandaa

Mtaalamu ni wewe...sawa?
Ukalimani ni profession. Kwa nini hawatumiki watu waliyosomea hiyo kazi badala ya kumpa mtu yeyote tu anayeonekana anaweza. Naamini kuna watu waliyosomea hiyo kazi na wapo Tanzania.... Kama hao wa leo wamesoma hiyo kazi, basi siju walifaulu vipi.
 
Hii si ni zao ya English course ya pale Royal Goldland college au brothers academy ukonga au Rasi simba. Unafundishwa kingereza cha kuongea miezi mitatu.
Haya ni mazao ya vyuo vinavyopatikana ghorofa ya kwanza.

Juu kuna chuo, chini gereji.
 
Usijifanye kuwa mjuaji...ni Nani alikuambia kuwa hiyo kazi ya leo alipewa mtu yeyote na siyo professional interpreter?
 
Ni kweli lakini si lazima tukizungumzia sana suala hilo kuliko hotuba ya rais Samia
Ile ilisimama aisee
 
Tumjue jina jamani [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tumsamehe kwakuwa si lugha yake mama hiyo ipo tu saaana tu hasa kwa beberu na wala hajali akikosea
Kwa tunaofuatilia matangazo ya mazishi ya kitaifa ya Hayati JPM kutoka uwanja wa Jamhuri dodoma, watakubaliana namimi kuwa aliyeandaliwa kutoa tafsiri hana huo uwezo.
  • Anaachwa mara kadhaa nyuma,
  • Anatoa tafuasiri zisizo sahihi.
  • Anaongea uelewa wake badala ya kutafuasiri.
Kamati isijirudie tena kwenye matukio ya kitaifa kama hilo.
Hayati alisisitiza tutumie kiswahili ili kikuwe kiwekinatumika kimataifa,
 
Hatakiwi mtu wa majribio kwenye kazi kama hiyo, ni aibu sana.
Yeye ni nafuu mara 100 zaidi yako! Tafuasiri ni neno la kiswahili? Mwenzio walau anajaribu Kiingereza, wewe hata Kiswahili ni tabu. 'Anayetafuasiri'.
 
Kwa tunaofuatilia matangazo ya mazishi ya kitaifa ya Hayati JPM kutoka uwanja wa Jamhuri dodoma, watakubaliana namimi kuwa aliyeandaliwa kutoa tafsiri hana huo uwezo.
  • Anaachwa mara kadhaa nyuma,
  • Anatoa tafuasiri zisizo sahihi.
  • Anaongea uelewa wake badala ya kutafuasiri.
Kamati isijirudie tena kwenye matukio ya kitaifa kama hilo.
Ni kweli! Japo English yangu ni ya kawaida sana,Ila huyo mtafsiri siyo. Na hapo ndipo sasa tuone kama kweli elimu yetu inahitaji kuwa kwa Kiswahili au tunatakiwa kuboresha English Ili Kila mtu amalize elimu akiwa na ujuzi nayo
 
Yani huyo jamaa ameendeleza uongo tena ilhali waliyekua wanamuogopa hayupo tena!
 
Sure mkuu. Yani mtu afanye blunder peke yake then tubebeshwe Taifa zima?
Itabidi hizi lawama na aibu ziende kwa mataga na Lumumba
FB_IMG_16164424763302199.jpg
 
Kikubwa sisi tunaelewana maana aliyekufa ni Rais wetu sisi wa Tz.... Kwaiyo tunaelewa nini kinaendelea!!!!

Wewe unafikiri hizo lugha ni mchezo! kumbuka hapo mtu ana majonzi ya msiba sisi tumuelewe uyo Rais wa south ili kiwe nini?

Tumpuzishe mpedwa wetu tuache na kejeli wakuu, we unaejua icho kingereza hata hapo Uingereza ukute hujaenda

Acha utani bwana wewe, wakati anapewa kazi hii bila shaka walizingatia uwezo wake na huenda hii ndio kazi yake katika kitengo cha mawasiliano. Sasa je huyo ndio muwakilishi wetu?? Lugha ya kiingereza bado ni muhimu, labda kama tunataka kujitenga ni sawa! Ndio lugha namba moja inayozungumzwa duniani!!

Umeleta mada mfu hapa. Kwanini tukio zima limekuwepo tunajua, hakuna haja ya kulitaja mara 100. Hapa hoja ni mkalimani na kutuabisha kwa kutuambia mawazo yake na sio alichotakiwa kufanya - kutafsiri!!!
 
Kwenye mazishi ya Mandela, alikuwapo huyu jamaa aliyezingua kinoma kutafsiri lugha ya viziwi. Baadaye alipohojiwa alijitetea kuwa katikati ya event alipatwa na ugonjwa wa schizophrenia, ambapo alikuwa anaona malaika wanakuja kutoka angani

View attachment 1731678
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Karma
 
Back
Top Bottom