Aibu kubwa! Msomi unakosaje kazi ya kufanya nchi hii yenye kila aina ya rasilimali?

Waje Mang'ura hapa Tuwafundishe kazi.... Vijana tunalima mpunga kama hatuna akili nzuri.
Tatizo hao waliomaliza digiriii wako sharo sana dah.. Acha waishi kwa mashemeji tu
 
Kuhusu masoko huo nao ni uvivu kwa sababu kuna zaidi ya Watanzania million 23 kwenye mtandao wa intaneti

Je mnatumia mtandao kutafutia wanawake na kuchat tu?
 
Anabwabwaja anafikiri Kilimo ni KAZI rahisi.Kilimo cha kisasa kinahitaji mtaji,ujuzi na maarifa, Elimu ya ugani nk.Anasema wazee wetu walitusomesha kwa Kilimo chenye tija ipo,unalima heka moja unapata junia kumi za mahindi badala ya junia zaidi ya hamsini.
 
Umuhimu wa kusoma ni kuongeza maarifa ili utatue changamoto za maisha.
kama umesoma ili upate kazi na bado una changamoto ya uchumi basi jua hauna akili na kweli hakuna umuhimu wa kusoma.
Baeleze mazee, maana kuna watu wanatoa maoni kana kwamba kusoma =kazi.
 
Upuuzi mtupu huu yani inakatisha tamaa
 
Wasomi hamtaki kilimo. Kuweni wakweli msijifiche kwenye changamoto. Kuthihitisha hilo ndiyo maana hata wahitimu wa SUA hatuwaoni mashambani wako kwa masheji zao wanafua boksa wakisubiria kazi.

Kusema kwamba hukufundishwa kilimo ndiyo maana hulimi ni uwongo wa shetani kabisa. Kuna wahitimu wanafanya umachinga, bodaboda, na udalali. Nani aliwafundisha?
 
Wewe jamaa nilifikiria una akili kumbe choko tu! Hivi nani ambaye ana hela za kukupa ukajaribu kilimo? Huyo mwenyewe aliekusomesha ameunga unga mpaka ukamaliza chuo nae amepata ahueni apumue sasa!

We unafikiri ukiuza smartphone kwa laki 2 tu hio laki 2 utakodi eneo na kununua dawa na petrol ya kumwagilia kwa kipindi chote hicho? Maana mazao ya muda mfupi ni miezi 3-5! Shamba heka nzima utasafishia bila vibarua!

Unaropoka kama vile hujawahi kulima kabisa mwehu wewe! Kilimo ni pesa! Kulima maharage tu acre 2 i wasted almost 2.5M na hio ni kwa uangalizi wa karibu na still nilipigwa usinga nikatoa gunia 8 instead ya 15 ambazo nili expect! Uzito nilipata kama 1.1 tonnes

Bei ya soko niliisubiria ikafika pazuri nikauza harage nikapiga 3.3M faida kama 800K ila haikuwa rahisi! By the time nilikua na kipato cha uhakika yani ila kwa hali ya sasa siwezi thubutu maana shamba litanishinda kuhudumia.
 
Mwanzo mgumu mkuu mkuu. Unapoanza tumia nguvu zako zaidi kama mtaji namba moja, lima, palilia na kuvuna mwenyewe. Wewe ulitumia hela nyingi kwasabb ulilima kwa remote (maagizo).

Pambana mwenyewe kwa miaka miwili upate mtaji wako halafu kidogo kidogo anza kujiondoa kwenye ushiriki wako wa moja kwa moja
 
Nilienda mwenyewe daily, Kama ushapasikia mahali panaitwa Kahe!

Kilimo cha kimaskini huwezi pata mavuno ya maana nakwambia! Utalima heka nzima upate gunia 4! Mbaya zaidi uwe umelima mahindi yani 😂 gunia elfu 20 times 4 ni 80K huku gharama umetumia laki 4!
 
Kwani we mwenzetu umesoma mpaka wapi? Maana hapa sioni kitu chochote cha msaada kwa hao vijana.Vipi huu ni mchambo ama ni kitu gani? Kingine hiyo ardhi unayosema ni kuwa inatolewa bure au vipi? Kama inatolewa bure unaweza wasaidia wapi inapatikana wakalime au kwa sababu we umezaliwa ukakuta mababu zako wana mashamba ukahisi kila mtu anayo hiyo fursa.

Kingine kuna tatizo gani mtu kuishi mjini? kama ndio kwao unataka aende wapi sasa.Mwisho kabisa achana na maneno ya kisiasa hayana msaada kwa vijana hao unaowasimanga.Unasema sijui asilimia kadhaa inafanya kilimo,Je hicho kilimo chenu kimekufikisheni wapi kama taifa?Kwahiyo unataka mtu apate mafunzo ya minimun 14 years then awe exposed kwenye hicho kilimo cha jembe na nyundo?Yes,they need to engage in production but not these stupid things done in your country.
 
Acre kukodi ni 150K mpaka 200K kulingana na location yake na umbali toka mtoni.

Kilimo cha sasa hulimi na mkono! Trekta kukusafishia ni 50K-80K per acre!

Madawa nayo yanaweza kutafuna almost 150K kwa wastani pamoja na vifaa vya kukodi vile kwa msimu mzima!

Petrol pump na mpira lazma ukodishe.

Kupanda lazma ulipe watu.

Kipindi cha palizi lazma ulipe watu.

Kuvuna lazma ulipe watu.

Hizo zote ni gharama hamna power ilanda au hawafu mwenye nguvu wa kulima heka 1 au 2 peke yako! Hela lazma itumike ili ulime kwa ufasaha!

Hapo sijagusa gharama za usafiri kufata madawa, wewe kusavaivu shamba lazma ule na unywe maji ikibidi uende hospitalini.

Nani wakukupa hizo hela atleast 3M unaweza lima kitu cha maana kidogo!
 
Zama zimebadilika. Nao wabadilike,vinginevyo wataishia kudeki na kufua nguo za mashemeji zao huku wakiwa na miaka 30
Dah mrembo hapa umenogeshaa...!!

Maana ninae Shemeji angu anapiga deki na kufua nguo zangu mpaka rahaa now ana 1st Degree ya Biashara.



Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Everybody needs a little somethn for them to be independent! Nobody just grew up and became independent! ~ Tafakari za Genius Tupac Shakur atleast uta gain kitu mzee! Amna mtu alianza akatoboa tu bila support hakunaaa!!!


Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…