Aibu kubwa! Msomi unakosaje kazi ya kufanya nchi hii yenye kila aina ya rasilimali?

Hizo gharama zimeangazia maeneo ya mijini zaidi. Na hata mtindo wa kilimo ni ule wa kidotCom zaidi. Huku kwetu vijijini tunajieleza tu kwa wazee wenye mashamba yao wanaturuhusu tulime bure. Na hatutumii pump kumwagilia. Tunabeba vidoo mwanzo mwisho. Na mwisho wa siku tunavuna.

Tena huwa tunaingia mkataba na vijana wa kitaa wa kumwagilia mpk mavuno halafu malipo wakati wa mavuno. Kijijini raha sana
 
Hujui hata unachoongea mleta mada.

Maisha yangekuwa rahisi hivyo watanzania wote wangekuwa mamilionea.
 
Everybody needs a little somethn for them to be independent! Nobody just grew up and became independent! ~ Tafakari za Genius Tupac Shakur atleast uta gain kitu mzee! Amna mtu alianza akatoboa tu bila support hakunaaa!!!


View attachment 1975343
You don't need any support

Huhitaji msaada wa mtu yoyote kwa sasa ili KUANZA maisha yako.

Support itakuja automatically utakapokuwa umeanza maisha yako
 
Ni nani hasiye hitaji msaada wa mtu yoyote dunia hii?

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Sina uhakika kama ulisoma comment yangu yote mpaka mwisho

Sijasema huhitaji msaada, nimesema ili KUANZA maisha yako huhitaji msaada wowote na nimemaliza kwa kusema msaada utakuja wenyewe automatically utakapokuwa umeanza maisha yako

Kama hujuwi kwa kawaida unapoanza jambo huwa hakuna mtu wa kukusupport lakini unapojitoa mhanga na kulianza na ukaonyesha juhudi watu kutoka kila kona hujitokeza kukusaidia

You must first take the first step
 
Unahisi support ni pesa tu eeh
Hata haya mawazo ni support

Kumbuka tunapoteza muda kukushauri na hujalipa hata sh 100

Ushauri huu unapata bure hapa jf mahali pengine ungelazimika kutoa pesa ndiyo ushauriwe

Unapoanza jambo kwa kawaida hutaona mtu akija kukusaidia mpaka umelianza na kuonyesha juhudi katika hilo
 
Hujui hata unachoongea mleta mada.

Maisha yangekuwa rahisi hivyo watanzania wote wangekuwa mamilionea.
Tatizo wasomi wengi mnatafuta umilionea. Mm natoa ushauri wa ninyi wasomi kuyaendesha maisha yenu kupitia kilimo badala ya kudhalilika kwa kukaa kwa ndugu miaka minne unasubiria ajira.

Tafuta hela kupitia kilimo itakayokupa heshima ktk jamii kupitia kilimo hata kama fedha hiyo haikupi umilionea.
 
Hii comment imejaa madini sijui kwann sikuiona mapema!!?
 
Unaona mbali Sana we jamaa
 
Mleta uzi ntakuunga mkono kama wewe umejiajiri, ila kama unaleta hizi dhihaka kwa vijana wetu wakati na ww ni muajiriwa tu utakua na matatizo sio bure.!
Ukute jamaa nae ni mwajiriwa,tena ameajiri na taasisi ya mtu binafsi .
 
Shida ipo kwenye mfumo wa elimu haumuandai kijana ili ajiajiri. Pia umeongelea kilimo, je unafaham ng'arama ya kilimo cha kisasa?
Elimu kazi yake ni kumpa mtu maarifa. Anapaswa kuyatumia maarifa hayo kupambana na changamoto za mazingira yanayomzunguka. Nadhani elimu isitupiwe lawama Sana. Lawama ziende kwa wasomi na jamii kwa ujumla, wamejenga mtazamo kwamba msomi lazima aajiriwe.

Kuhusu gharama za kilimo nalo pia sikubaliani. Hzi gharama zipo kwa wasomi tu? Mbona watu wengi kule kijijini wanaendesha maisha yao kwa kilimo ktk hali duni hiyo hiyo? Sasa huyu msomi anashindwa vipi kuanzia hapo Kisha akaboresha???
 
Umeshinda.
 
Nani alikwambia maisha ni kilimo pekee? Punguza ushamba kijana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…