sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Ni moja ya kanisa linaloendelea kufuata sheria za agano la kale ikiwemo kuheshimu sheria zilizowekwa na Mungu kuhusu uchambuzi wake wanyama wa kula pamoja na kuendelea kuamini Pombe ni chukizo kwa Mungu, Siku yao ya kuabudu huanza ijumaa jioni hadi jumamosi kama ilivyo kwa wayahudi wanaoabudu siku hio kwa kuiita shabat (Sijajua uhalali wa wao kuona ndio siku ya sabato)
Ila sasa kuna baadhi ya sheria wameanza kupwaya.
Miaka ya 90s na 2000s mwanzoni nilishuhudia wasabato wengi wakienda kunyoa walikuwa wanakataa kuchongwa mpaka wakajipatia umaarufu wa mtindo wao kuitwa "kunyoa kisabato", Lakini leo hii hali ni tofauti, ukienda makanisa ya wasabato utaona mpaka wachungaji wamepiga panki na kuzichonga nywele, ndevu wamechonga kwa mtindo wa O.
Huyu ni mojawapo wa kundi la wachungaji wengi wa kisabato wanaochonga nywele na ndevu.
Pia mabinti wengi sana walikuwa hawasuki wala kuvaa hereni waliamini kwa
mujibu wa Nyaraka za Mitume- Paulo na Petro, KUSUKA kumetizamwa kama MAPAMBO, Kwa mujibu wa Biblia, MAPAMBO MAZURI ni Tabia Njema, utu wa Moyoni, kuvaa kwa kujisitiri, kujikubali uumbaji wako bila kujitoboa (hereni), kuchora tattoo, ama kubadili mtindo wa nywele ulizoumbiwa mfano kuzirefusha nywele fupi kwa kuzisuka rasta.
, lakini leo hii imeshakuwa kawaida kuwakuta hereni zinaninginia masikioni na kila wiki/mwezi msuko mpya.