Aibu: Polisi yatuhumiwa kudukua simu ya Wakili Mwabukusi na kumuwekea maudhui Instagram ili impe kesi

Aibu: Polisi yatuhumiwa kudukua simu ya Wakili Mwabukusi na kumuwekea maudhui Instagram ili impe kesi

Polisi wajiweke mbali na haya mambo madogomadogo,hatakama wanapewa oda,wawe wanahoji.Hii inawachafua sana,halafu mwisho wa siku,viongozi haohao wanaotoa oda,wanakuja wanaanza kuwafokea mbele ya kadamnasi.Wajirekebishe, ikiwezekana hata kuijuzulu,ukiona unachoamriwa ni cha kijinga.
Mshahara inasemekana ni mdogo,kikokotoo kinawaimiza,halafu na watu wengine wawatumie kwa maslahi yao kweli?
PT,amkeni.
Noma sana !
 
View attachment 2718990

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Mbeya , Wakili wa Mwabukusi , Mwakilima , amesema kwamba Maudhui yanayosambaa mtandaoni na kudaiwa kwamba ni ya Boniface Mwabukusi yamewekwa na Polisi wenyewe baada ya kudukua akaunti yake ya Instargram baada ya kumnyang'anya simu yake ya mkononi .

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba , ndio maana hakukuwa na taarifa hizo awali, zimeletwa ghafla baada ya udukuzi huo kufanikiwa .

Lengo la jambo hili ni kuudanganya umma ili ijulikane kweli kwamba Mwabukusi na wenzake ni Wahaini .

Ni aibu sana kwa Jeshi letu la Polisi , kugundulika kufanya njama hii ya kijinga , na ni kuidhalilisha nchi nzima kwa manufaa ya DP WORLD na wapambe wake
Yaani hatuna polisi. Na ikichukuliwa maanani, Kingai ndie DCI mtaalam wa kesi za kubumba.
 
Ni kweli naamini hayo, nia ya polisi ni ovu.

Haiwezekani huu ushahidi wao unatokea wakati huu wakiwa wamewakamata watuhumiwa, wanafanya hivyo kwa lengo la kuudanganya umma kwamba watuhumiwa walikuwa na hiyo mipango, na wale wahuni wanachukua huo uongo wa polisi na kuusambaza.

Utasema vipi simu yangu ilikuwa na mipango ovu dhidi ya serikali ikiwa wewe ndie uliyekuwa ukiishikilia kwa siku zaidi ya tatu? Ni mjinga pekee atakayeamini madai hayo ya polisi.
 
Back
Top Bottom