Aibu: Watuhumiwa watatu kesi ya Mbowe wadai kuteswa na Polisi ili wakubali kuandika maelezo ya uongo

Aibu: Watuhumiwa watatu kesi ya Mbowe wadai kuteswa na Polisi ili wakubali kuandika maelezo ya uongo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,138
Reaction score
288,731
Watuhumiwa hao watatu walioshitakiwa pamoja na Mbowe Wameiomba Mahakama kutoyatambua maelezo waliyoyaandika Polisi kwa vile waliyaandika kwa shinikizo la vipigo na mateso, hayakuwa maelezo ya kweli , bali waliyaandika ili wasiuawe kwa mateso .

Ombi hilo limetolewa Mahakamani na washitakiwa hao watatu , waliodai kwamba walilazimishwa kuandika maelezo ya uongo kibabe na kwa mateso makubwa mno , Polisi walitesa watuhumiwa hao kinyama ili kulazimisha kwamba walitumwa na Mbowe kufanya ugaidi kwa lengo la kuhalalisha Tuhuma dhidi ya Freeman Mbowe zilizopangwa kishamba ili kuwafurahisha watawala

Washitakiwa hao wamedai kwamba ili kujinusuru na mateso makubwa ya kinyama na ya kudhalilisha walipokuwa mikononi mwa Polisi , walilazimika kuandika MAELEZO YA UONGO WALIYOYATAKA POLISI ili kuokoa uhai wao
 
Hii serikali imeshapoteza maono,sasa hivi inafanya tu kazi ya kuvizia wananchi,Believe me-Hawa wanatutega wananchi waanze kutukata tozo ya vocha na line za simu kwanzia mwezi wa saba mwisho wa mwezi huu.Inasikitisha sana
 
Mama nakuomba vaa ujasiri na uingilie kati. Najua unawaogopa waliokuzunguka. Katiba, vifungu vya Kurani na Sheria vinakulinda. Chochote utamkacho ni sheria. Muachie Freeman Mbowe sasa hivi.
Mahakama ni muhimiri huru.
 
1629721317172.png


2878995_images_9.jpeg
 
Tayari maji yashamwagika kwani maelezo yao yamefanikisha vyombo vya usalama kufahamu mengi.

Sasa tuiachie mahakama ndo chombo cha mwisho.
 
Maelezo ya Watuhumiwa waliyotoa Polisi ni moja ya vielelezo vinavyowasilishwa kati ya vielelezo 19 vilivyoahidiwa na Polisi. Hivyo hata wakikataa maelezo yao ya polisi haimaanishi ndio mwisho wa kesi. Kuna kazi ya kuonyesha vielelezo 18 vilivyobaki navyo ni invalid. TUSISHANGILIE
 
Hii imekaaje kisheria?
Kisheria ili tukubaliane na maelezo yao inatakiwa usikilizwe na upande wa pili ili kujiridhisha na walichoongea. Hauwezi kukata kesi kwa kusikiliza upande mmoja tu maana kauli au tukio linaweza kuwa limetengenezwa na walalamikaji ili kujinasua na mkono wa sheria.
 
Hamna kesi hapo.

MUNGU kashaingilia kati baada ya maombi, watuhumiwa wameanza kusema ukweli.
 
Back
Top Bottom