Aibu ya Tanzania. Mkuu wa nchi anazindua minara ya bil 270+ huku wananchi vijijini hawana maji wala huduma za afya za uhakika

Aibu ya Tanzania. Mkuu wa nchi anazindua minara ya bil 270+ huku wananchi vijijini hawana maji wala huduma za afya za uhakika

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Watu wa vijinini hawana uhakika wa huduma za afya na maji ya uhakika.

Kati ya watu kumi ni mmoja tu anaweza kuwa na smart phone huko vijjini. Hizi pesa kwa nini zisitumike kwa mambo ya muhimu
Screenshot_20230514-120425.jpg
 
  • Minara ni muhimu ili kufungua vijijini.
  • Ungelia yale magari ya kifahari yanayoagizwa na kuhudumiwa na billions ningekusikia
 
  • Minara ni muhimu ili kufungua vijijini.
  • Ungelia yale magari ya kifahari yanayoagizwa na kuhudumiwa na billions ningekusikia
vijiji hufunguka kwa huduma safi ya barabara, maji, afya na elimu. Hizo minara should be the last. Ni sawa na kumkokea moto mwenye njaa aote moto badala ya kumpa chakula
 
Sijajua unafananisha na nini lakini kwa tulipofikia ni aibu pia kusikia Kuna wanakijiji hawana huduma ya Mawasiliano. Fikiria tu hapo ulipo, huwezi kupiga simu, huwezi kuperuzi mtandaoni kama hapa unavyopost, huwezi hata kujua kinachoendelea nje ya kijiji chako.

Kuna huduma muhimu zinashindikana kwa sababu tu watu hawana Mawasiliano.

Tumechelewa kwa mengi, lakini hili la minara ya simu naunga mkono serikali 100 %.
 
Watu wa vijinini hawana uhakika wa huduma za afya na maji ya uhakika.

Kati ya watu kumi ni mmoja tu anaweza kuwa na smart phone huko vijjini. Hizi pesa kwa nini zisitumike kwa mambo ya muhimu
View attachment 2621259
Mkuu hata mawasiliano ni muhimu sana.
Unaweza kupata mgonjwa bila mawasiliano unaweza kumpoteza.
 
vijiji hufunguka kwa huduma safi ya barabara, maji, afya na elimu. Hizo minara should be the last. Ni sawa na kumkokea moto mwenye njaa aote moto badala ya kumpa chakula
Hivi haya mawasiliano si ndo yanafanya mpaka tunapata pesa kwa vijana wetu waliopo mijini?
 
Watu wa vijinini hawana uhakika wa huduma za afya na maji ya uhakika.

Kati ya watu kumi ni mmoja tu anaweza kuwa na smart phone huko vijjini. Hizi pesa kwa nini zisitumike kwa mambo ya muhimu
View attachment 2621259
Mkuu hii nchi ukiifuatilia ni pasua kichwa kila mtu na style yake katika kujinufausha kodi zetu,yaani minara inapata priority badala ya maji
 
Wananchi wa wapi hawana maji Sasa wanaishije? Umekuja kjjn ukakuta hatuna maji? Kwasasa kila kata ina kituo Cha afya...kilichobaki Sasa ni network tu tumechoka kutafuta network maporini usku
 
Kuna mjinga mmoja kule Afrika Magharibi aliwahi kutumia matrilion kujenga kijijini kwao huku akishindwa kusaidia wananchi wake wa sehemu nyingine ya nchi waliokumbwa na tsunami na kuwapora pesa zao walizochangiwa na wasamaria wema, Nasikia ameshafariki dunia.
 
Minara ya mawasiliano ni muhimu zaidi kuliko yale madege ya awamu ya tano.
 
Watu wa vijinini hawana uhakika wa huduma za afya na maji ya uhakika.

Kati ya watu kumi ni mmoja tu anaweza kuwa na smart phone huko vijjini. Hizi pesa kwa nini zisitumike kwa mambo ya muhimu
View attachment 2621259
Du, mawasiliano si mambo ya muhimu. Sikujua kuwa mawasiliano ni anasa!
Kwangu mawasiliano ni moja ya chachu za maendeleo ya wananchi.
Nchi yeyote iliyoendelea utakuta hata njia za mawasiliano hususan simu takwimu zao ziko juu.

Tusipo pajua tuulize.
 
Mimi sijajua, ni minara ya TTCL?, Vodacom or CCM? , Au universal fund ya kuwezesha mawasiliano ambapo hakuna mawasiliano?
 
Watu wa vijinini hawana uhakika wa huduma za afya na maji ya uhakika.

Kati ya watu kumi ni mmoja tu anaweza kuwa na smart phone huko vijjini. Hizi pesa kwa nini zisitumike kwa mambo ya muhimu
View attachment 2621259
Nadhani kangara uliyotengeneza leo umekunywa mwenyewe pipa zote badala ya kuuza

Umeanzisha uzi wa kiboya Sana

Nadhani miradi mingi Sana ya maji iko kwenye pipe lines sasa hivi. Sema binadamu mmeumbwa kuona kila kitu kibaya tu. Wewe ingekuwa kijijini kwenu hakuna mawasiliano ungelalamika na usingewaza mautopolo haya umeandika hapa. Ukiamka asubuhi na kangala zako kichwani una beep tu kwa shemeji aliyeko wilayani anakutumia vocha huoni umuhimu wa wale wasio na mawasiliano
 
Back
Top Bottom