Uchaguzi 2020 Aida Khenani (CHADEMA): Siwezi kuwasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini, mimi ni mbunge halali, ninasubiri kuapishwa tu

Safi saana
Aende bungeni na madiwani wafanye kazi..
Atakua chachu ya mijadala yenye tija
 
Kilichomtokea Kessy ndio kilichomtokea Juma Nkamia...
 

..hiyo 18% imepatikana kwa nguvu na jasho la wagombea wote.

..kwa hiyo waliopata nafasi wanatakiwa kushirikiana na wenzao ambao hawajapata nafasi au wamedhulumiwa.
 
Haya matatizo yote yameletwa na viherehere wa chama akina Malisa ambao ndio kwanza kuanza kukimbilia kumshauri aukatae ubunge

2015 tulipigwa bao na akina mbowe wakapita ila hawakuuacha ubunge kuwaunga mkono wenzao walodhulumiwa
Ila Aida imekua shida
 
..hiyo 18% imepatikana kwa nguvu na jasho la wagombea wote.

..kwa hiyo waliopata nafasi wanatakiwa kushirikiana na wenzao ambao hawajapata nafasi au wamedhulumiwa.
18% inatokana na kura za urais katika majimbo. Mgawavyo wake ni wenyewe cdm watumie busara tu lkn sio kulazimisha wabunge waliopita kwa kuchaguliwa kususia.
 
Wamfutie uanachama fasta asituletee ngonjera wakati huu wa maombolezo
Soma attachment ambayo ameongea mwenyewe ,acha maneno ya kuongeza ya mtoa post.
Huyo mbunge amesema yupo tayari kuungana na wenzake, anasubiria maamuzi.
 
18% inatokana na kura za urais katika majimbo. Mgawavyo wake ni wenyewe cdm watumie busara tu lkn sio kulazimisha wabunge waliopita kwa kuchaguliwa kususia.
Waache watu wakavute mkwanja, wasiwazuie.
Watanzania bado ni waoga sana mbele ya vyombo vya dora, hayo wanayotaka akina mbowe hawawezi kuyapata sasa.
 
Kale hela mama. Nchi hii imejaa mazwazwa hayahitaji kutetewa. Ukipata nafasi piga hela.
 
Aende bungeni kwa heshima na kuenzi damu ya mawakala iliyomwagika kwa ajali huko sumbawanga
 
Inawezekana huyo mbunge alipambana vya kutosha mpaka akawashinda wapinzani wake, pengine nae angefyagiliwa mbali kimkakati ila misheni za wapinzani wake zilifeli hazikulenga shabaha, yule mpinzani wake hakuwa mwepesi kuanguka kutokana hoja zake bungeni. Kiroho safi CHADEMA waridhje tu aingie bungeni, ushupavu wake utajulikana huko. Huenda kuna makosa ya kiufundi yalitendeka huko akabahatika kushinda, vinginevyo naye angegaragazwa vibaya kama wenzake
 
Hii kauli ameitoa kwenye platform gani?

Weka source
 
Hata mimi ningefanya kama yeye, maana hata na hivo ni nafasi moja, kuigomea kabisa haina tija yoyote kwa Chadema na Kwake binafsi
 
Kama uchaguzi hautarudiwa sioni mantiki ya yeye kukubali wazo la kukataa ubunge, kawakilishe wananchi wako...huku tukiipambania demokrasia...ana familia na maisha ya kuishi licha ya gharama alizotumia
Mimi ningemshauri aachie ngazi akaunge mkono juhudi kisha agombee akiwa huko ili aweze kwenda kugonga meza vizuri.
 
Hapo Bwn. Mwenyekiti anabadili kila channel hakuna inayokaa,

Akishika hiki anakiweka chini,

Kupoteza ruzuku ambazo ulikuwa unafix mahesabu ili ziwe mapato yako, lazima presha ikupande.
 

Lijualikali, Komu etc. Hujajifunza tu??? Ccm wamekutumia na ukakubali kutumika. Utakipata ulichokitaka.
 
Viziri sana DEMOKRASIA ya kweli ni kuheshimu mawazo ya wengi. Asante kwa kuheshimu kura za wana Nkasi. Kawawakilishe mama.
Kafanye yale wamekutuma.
 
Halafu mimi nilivoanza kusoma kichwa cha habari nikajua ameukataa ubunge kama viongozi wake walivosema uchaguzi haukua halali 🀣🀣🀣

kumbe pesa tamu aise ... duh !
 
..it is a very tricky situation.

..Chadema wakianza kugombana naye, Ccm hawatapoteza muda kumchukua na kumtumia dhidi ya Chadema.

..Ndio maana napendekeza Chadema waende naye taratibu na waepushe migogoro naye.
mbowe alika kumzibia ridhiki dada wawatu sasa naye kachaluka sijui itakuwaje,maana kina mbowe hawatambui matokeo yoyote!! Labda wamfute uanachama!! Cdm buanaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…