Uchaguzi 2020 Aida Khenani (CHADEMA): Siwezi kuwasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini, mimi ni mbunge halali, ninasubiri kuapishwa tu

Uchaguzi 2020 Aida Khenani (CHADEMA): Siwezi kuwasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini, mimi ni mbunge halali, ninasubiri kuapishwa tu

Safi saana
Aende bungeni na madiwani wafanye kazi..
Atakua chachu ya mijadala yenye tija
Huu ndo ukweli, namjua AIDA na nimekuwepo Namanyere tangu siku ya upigaji kura hadi kutangazwa matokeo, ilikuwa mbinde kweli kweli. Dada kapambana na majizi kwa nguvu hadi kunyang'anyana fomu za matokeo na Msimamizi wa kata ambazo baadaye zilijulikana ni feki. Mabomu ya mshindo zaidi ya 30 yamepigwa eneo la Halmashauri ya Nkasi kufukuza Wafuasi wake lakini walinawa maji na kujifunika vitambaa puani mapambano yakaendelea.

Mkuu wa Wilaya Said Mtanda na Mgombea wa chama chake walipita alfajiri tarehe 29/10 wakitangaza ushindi feki wa Ally Keissy, hali iliyowaamsha wananchi waliokuwa wanajua mshindi ni nani kuingia barabarani hadi Halmashauri kudai Mshindi halali atangazwe. Viongozi wa CHADEMA wanatakiwa kitumia busara kwa wale walioshinda, siyo kwamba wamepewa bure, wamepambana. Mbali ya kuwepo wizi lakini CHADEMA wamepata Madiwani 4 kati ya kata 17 baada ya mapambano makali.
 
Kilichomtokea Kessy ndio kilichomtokea Juma Nkamia...
 
Hivi mnashindwa hata kuuliza muelimishwe. Nani amekwambia cdm wana mbunge mmoja?
Ipo hivi, hata cdm wasingeshinda jimbo lolote, kwa kufikisha 18% ni zaidi ya 5% ya kula zote, tayari wana wabunge wa kuteuliwa. Kwa haraka haraka, cdm watakuwa na wabunge zaidi ya 10 wa kuteuliwa + na huyo mmoja.
Act wana wabunge kama wanne tu wa kuchaguliwa na cuf wana wabunge 3. So hizo akili zenu kuwa hakutakuwa na wabunge wa upinzani ni utopolo mtupu. Kinacho piganiwa kwa sasa ni maslahi ya kina mbowe tu.

..hiyo 18% imepatikana kwa nguvu na jasho la wagombea wote.

..kwa hiyo waliopata nafasi wanatakiwa kushirikiana na wenzao ambao hawajapata nafasi au wamedhulumiwa.
 
Haya matatizo yote yameletwa na viherehere wa chama akina Malisa ambao ndio kwanza kuanza kukimbilia kumshauri aukatae ubunge

2015 tulipigwa bao na akina mbowe wakapita ila hawakuuacha ubunge kuwaunga mkono wenzao walodhulumiwa
Ila Aida imekua shida
 
..hiyo 18% imepatikana kwa nguvu na jasho la wagombea wote.

..kwa hiyo waliopata nafasi wanatakiwa kushirikiana na wenzao ambao hawajapata nafasi au wamedhulumiwa.
18% inatokana na kura za urais katika majimbo. Mgawavyo wake ni wenyewe cdm watumie busara tu lkn sio kulazimisha wabunge waliopita kwa kuchaguliwa kususia.
 
Wamfutie uanachama fasta asituletee ngonjera wakati huu wa maombolezo
Soma attachment ambayo ameongea mwenyewe ,acha maneno ya kuongeza ya mtoa post.
Huyo mbunge amesema yupo tayari kuungana na wenzake, anasubiria maamuzi.
 
18% inatokana na kura za urais katika majimbo. Mgawavyo wake ni wenyewe cdm watumie busara tu lkn sio kulazimisha wabunge waliopita kwa kuchaguliwa kususia.
Waache watu wakavute mkwanja, wasiwazuie.
Watanzania bado ni waoga sana mbele ya vyombo vya dora, hayo wanayotaka akina mbowe hawawezi kuyapata sasa.
 
Kale hela mama. Nchi hii imejaa mazwazwa hayahitaji kutetewa. Ukipata nafasi piga hela.
 
Aende bungeni kwa heshima na kuenzi damu ya mawakala iliyomwagika kwa ajali huko sumbawanga
 
Inawezekana huyo mbunge alipambana vya kutosha mpaka akawashinda wapinzani wake, pengine nae angefyagiliwa mbali kimkakati ila misheni za wapinzani wake zilifeli hazikulenga shabaha, yule mpinzani wake hakuwa mwepesi kuanguka kutokana hoja zake bungeni. Kiroho safi CHADEMA waridhje tu aingie bungeni, ushupavu wake utajulikana huko. Huenda kuna makosa ya kiufundi yalitendeka huko akabahatika kushinda, vinginevyo naye angegaragazwa vibaya kama wenzake
 
Chama kiliniamini kikarudisha mamlaka kwa wananchi na wananchi wamenipa mamlaka. Kama niliapa Chadema siwezi isaliti hali kadhalika siwezi wasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini.

Naomba nitoe msimamo wangu, mimi Aida nimechaguliwa kwa mujibu wa sheria na ni mbunge halali wa Nkasi Kaskazini, ninasubiri kuapishwa na hakuna jambo jingine, sina mabadiliko mengine.

Pia soma> Aida Khenan: Demokrasia ni muhimu kuliko ushindi wangu. Nipo tayari kuungana na wenzangu kwa maamuzi yoyote

Hii kauli ameitoa kwenye platform gani?

Weka source
 
Hata mimi ningefanya kama yeye, maana hata na hivo ni nafasi moja, kuigomea kabisa haina tija yoyote kwa Chadema na Kwake binafsi
 
Kama uchaguzi hautarudiwa sioni mantiki ya yeye kukubali wazo la kukataa ubunge, kawakilishe wananchi wako...huku tukiipambania demokrasia...ana familia na maisha ya kuishi licha ya gharama alizotumia
Mimi ningemshauri aachie ngazi akaunge mkono juhudi kisha agombee akiwa huko ili aweze kwenda kugonga meza vizuri.
 
Hapo Bwn. Mwenyekiti anabadili kila channel hakuna inayokaa,

Akishika hiki anakiweka chini,

Kupoteza ruzuku ambazo ulikuwa unafix mahesabu ili ziwe mapato yako, lazima presha ikupande.
 
Chama kiliniamini kikarudisha mamlaka kwa wananchi na wananchi wamenipa mamlaka. Kama niliapa Chadema siwezi isaliti hali kadhalika siwezi wasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini.

Naomba nitoe msimamo wangu, mimi Aida nimechaguliwa kwa mujibu wa sheria na ni mbunge halali wa Nkasi Kaskazini, ninasubiri kuapishwa na hakuna jambo jingine, sina mabadiliko mengine.

Pia soma> Aida Khenan: Demokrasia ni muhimu kuliko ushindi wangu. Nipo tayari kuungana na wenzangu kwa maamuzi yoyote

Lijualikali, Komu etc. Hujajifunza tu??? Ccm wamekutumia na ukakubali kutumika. Utakipata ulichokitaka.
 
Chama kiliniamini kikarudisha mamlaka kwa wananchi na wananchi wamenipa mamlaka. Kama niliapa Chadema siwezi isaliti hali kadhalika siwezi wasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini.

Naomba nitoe msimamo wangu, mimi Aida nimechaguliwa kwa mujibu wa sheria na ni mbunge halali wa Nkasi Kaskazini, ninasubiri kuapishwa na hakuna jambo jingine, sina mabadiliko mengine.

Pia soma> Aida Khenan: Demokrasia ni muhimu kuliko ushindi wangu. Nipo tayari kuungana na wenzangu kwa maamuzi yoyote

Viziri sana DEMOKRASIA ya kweli ni kuheshimu mawazo ya wengi. Asante kwa kuheshimu kura za wana Nkasi. Kawawakilishe mama.
Kafanye yale wamekutuma.
 
Halafu mimi nilivoanza kusoma kichwa cha habari nikajua ameukataa ubunge kama viongozi wake walivosema uchaguzi haukua halali 🤣🤣🤣

kumbe pesa tamu aise ... duh !
 
..it is a very tricky situation.

..Chadema wakianza kugombana naye, Ccm hawatapoteza muda kumchukua na kumtumia dhidi ya Chadema.

..Ndio maana napendekeza Chadema waende naye taratibu na waepushe migogoro naye.
mbowe alika kumzibia ridhiki dada wawatu sasa naye kachaluka sijui itakuwaje,maana kina mbowe hawatambui matokeo yoyote!! Labda wamfute uanachama!! Cdm buana😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom