Uchaguzi 2020 Aida Khenani (CHADEMA): Siwezi kuwasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini, mimi ni mbunge halali, ninasubiri kuapishwa tu

Uchaguzi 2020 Aida Khenani (CHADEMA): Siwezi kuwasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini, mimi ni mbunge halali, ninasubiri kuapishwa tu

Hiyo ndio haki na demokrasia mnazozihubiri kila siku ila sasa mnataka kumnyima Aidah
Chadema hawajawahi kuwa serious na chochote wanachoongea na wala wanachokifanya
Kwa akili yako ile tunayoifaham, unadhani hakukuwa na mbunge kwenye jimbo lingine aliyeshinda na kumpa ushindi ila huyu dadako ndiye alionekana kushinda bila hila?.
 
Kwa akili yako ile tunayoifaham, unadhani hakukuwa na mbunge kwenye jimbo lingine aliyeshinda na kumpa ushindi ila huyu dadako ndiye alionekana kushinda bila hila?.
Ushindi usiothibitika hatuwezi kuungelea. Wewe unaona kumshinikiza Aidah ajiuzulu ni haki?
 
Chadema hawajasema lolote kuhusu huyu dada na madiwani zaidi ya kusema wasiende kuapishwa. Kama watapuuza na wakaenda kuapishwa, Chadema wawaache waendelee na ubunge na udiwani wao bila kutoa tamko lolote. Wanachoweza kufanya ni kutowapa msaada wa chama katika utendaji wao na kuweka wazi kuwa hawawatambui kama wawikilishi wa chama.

Hata hivyo ukweli wa msimamo wao kama wapinzani utaonekana mapema tu. Na haitawachukua muda kujitoa kwenye chama na kwenda kwenye chama tawala. Na kama wataonyesha kuwa ni wapambanaji hasa hata wakiwa peke yao, Chadema haitapata hasara. Changamoto ya Chadema ni kwenye viti maalum.

Amandla...
 
Huyu mbunge ninashaka sana huenda ni mpango wa CCM kutaka kukigawa chama. Sababu anazotoa hazina mashiko kabisa Mfuteni uanachama kabla hajaapishwa.

Eti yupo mafichoni kwa kuogopa kuuawa. Afukuzwe mapema hii akawatumikie vizuri Wananchi
 
Ni kweli kabisa, yupo sahihi, ila kama chama hakitaki aende Bungeni, ni kumchomolea kadi badala ya kusema tu asiende wakati akiwa mwanachama. Ingawaje sababu za kuchomoa kadi ziwe halali na za msingi!!
Wewe unafikiri Mbowe angeshinda ubunge asingeenda bungeni ?Thubuuutu.
 
Chama kiliniamini kikarudisha mamlaka kwa wananchi na wananchi wamenipa mamlaka. Kama niliapa Chadema siwezi isaliti hali kadhalika siwezi wasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini...
Sasaivi anawaza hela tu na maisha yake ao wananchi wa Nkasi ni kimbilio tu na mahali pa kujifichia, kama kweli ni mwanademokrasia angeangalia namna chama chake kilivyoumizwa kwenye uchaguzi feki na angesimama na maamuzi ya chama chake kwa manufaa ya Watanzania walionyimwa kwa makusudi haki zao na sio Nkasi tu.

Kwa nini amehudhuria kuapishwa kwa JPM ni wazi anabariki kile kilichofanywa na kutokujali haki za wengine badala yake anaangalia nafasi yake tu aliyonayo. Nadhani Chadema wasiende mbali na huyu mama nina wasiwasi ata huo uteuzi wake kuwa mbunge huenda alipandikizwa tu na wala sio kuchaguliwa kwa kura, tunafahamu maneno ya Ally Kessi pale bungeni mara ya mwisho kutaka mkuu anendelee kuwa rais wa maisha huenda yalimkera sana mkuu na haya kuwa ndio malipo yake. Tusifichane uchaguzi huu hakuna kura ata moja iliyohesabiwa kutoka kituoni everything was on pepars already.
 
Cha kushekesha uchaguzi huu ni kwamba ukiwa jeuri pia unafyekelewa mbali - Sijajua kosa la Kessy na Ghasia.... yawezekana ni u team Membe umewaponza.

Overall hatukuwa na uchaguzi anyway so nothing to be worried ndani ya roho zetu.
 
Chama kiliniamini kikarudisha mamlaka kwa wananchi na wananchi wamenipa mamlaka. Kama niliapa Chadema siwezi isaliti hali kadhalika siwezi wasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini...
ACT ilikuwa inawakilishwa na Zitto tu mbona hakususwa tatizo ni umimi kwani yeye akiwa mbunge pekee wa CHADEMA hatoweza kuongea na kupewa hoja na chama chake kupeleka bungeni.
 
Anawajibika kuwawakilisha wananchi waliomchagua na kwenda kwake bungeni hakumzuii kuwatetea wenzake ktk upinzani waliodhulumiwa ktk uchaguzi mkuu.
Na huu ndio msimamo wake kama umemsikia vizuri.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Tanzania ina vituko kila kona. Ukifa kwa stress ni umejitakia tu.
Leo hii I'd imechangia kwenye uzi.

Kweli Tanzania inavituko kila kona. Ukifa kwa stress ni umejitakia tu.
 
Huyu afukuzwe Mara moja maana wameshaanza kumtumia maccm , halafu anajidai kuja na hoja za ajabuajabu eti wapiga kura wake wanataka aende bungeni , hivi hao wapiga kura wake Nkasi unafikiri wajinga hawajui kilichofanywa na maccm nchi nzima , kwahiyo we Aidsh Kenan ukienda bungeni peke yako ndio utafanya mageuzi gani?

Au hoja zako ndio zitadikilizwa ?, Tumia akili Kama njaa inakusumbua nenda sisi wanamageuzi wote hstuafiki wewe kwenda maana hauna utakachoenda kukifanya wewe peke huko bungeni au una miujiza?

Nenda ukawe sehemu ya laana ya yaliyopangwa kufanyika .Si unayajua lakini? Wewe si ulikuwa bungeni viti maalumu so unajua yaliyopangwa na maccm na uchaguzi huu Ni uthibitisho tosha kuwa wamedhamiria .
 
Huyu afukuzwe Mara moja maana wameshaanza kumtumia maccm , halafu anajidai kuja na hoja za ajabuajabu eti wapiga kura wake wanataka aende bungeni , hivi hao wapiga kura wake Nkasi unafikiri wajinga hawajui kilichofanywa na maccm nchi nzima , kwahiyo we Aidsh Kenan ukienda bungeni peke yako ndio utafanya mageuzi gani? Au hoja zako ndio zitadikilizwa...

Ni kujivika upofu tu kwani kwa sheria zetu hakuna Mbunge anaye ning'inia bila chama cha siasa! Chama chake kikiamua kususa kushiriki HARAMU na yeye akadhani atabebwa na wapiga kura wake ajue akifutwa uanachama na ubunge wake unakoma. Hivyo Tume kulazimika kutangaza kuwa Jimbo liko wazi na utatangazwa uchaguzi mpya. Swali ni je, akiamua kuunga juhudi mkono, ccm watakubali kumbeba na kumpiga chini Kessy?
 
Ushindi usiothibitika hatuwezi kuungelea. Wewe unaona kumshinikiza Aidah ajiuzulu ni haki?
👇
Sasa hivivi anawaza hela tu na maisha yake ao wananchi wa Nkasi ni kimbilio tu na mahali pa kujifichia, kama kweli ni mwanademokrasia angeangalia namna chama chake kilivyoumizwa kwenye uchaguzi feki na angesimama na maamuzi ya chama chake kwa manufaa ya Watanzania walionyimwa kwa makusudi haki zao na sio Nkasi tu.

Kwa nini amehudhuria kuapishwa kwa JPM ni wazi anabariki kile kilichofanywa na kutokujali haki za wengine badala yake anaangalia nafasi yake tu aliyonayo. Nadhani Chadema wasiende mbali na huyu mama nina wasiwasi ata huo uteuzi wake kuwa mbunge huenda alipandikizwa tu na wala sio kuchaguliwa kwa kura, tunafahamu maneno ya Ally Kessi pale bungeni mara ya mwisho kutaka mkuu anendelee kuwa rais wa maisha huenda yalimkera sana mkuu na haya kuwa ndio malipo yake. Tusifichane uchaguzi huu hakuna kura ata moja iliyohesabiwa kutoka kituoni everything was on pepars already.
 
Huyu binti aende akawatetee wananchi wake. Mbona wakati ule palikuwa Dr Slaa, Zitto Kabwe na wengine hawakufika 5, Bunge lilikua moto tuu.

Huyu mmoja na wa CUF watapiga kelele tuu na kuitoa usingizini CCM.
Riziki yake huyu Mbuge muachieni. Ni maisha yake na ajira yake. Asipoenda munaongeza wasiokua na ajira.

Muacheni akapambane na asionewe jamani, muacheni mwana mama aendelee.

Misimamo ya kupambana na CCM iendelee nje ya Bunge. Hujuma imetendeka kama kuna ushahidi pelekeni mahakamani. Na tupambane kudai Katiba mpya kwa marithiano. Wakati mwingine, tutumie akili na sio nguvu kudai haki.

CCM niwaoga sana, na wanapenda sana kutumia Polisi na vitisho, CHADEMA na upinzani mzima, tumieni akili kupambana na adui mwenye dola.
 
Tulia Viongozi Wakae Waamue
Mwenyekiti Wetu Aliposema Usinichanganyie Battery Na Gunzi Hiyo Torch Sitaiwasha. Alikuwa Na Maana Nzito
Ili Aweze Kuwawajibisha Mbunge, Diwani Wanaotokana Na Chama Dola!!😶🤨😑😏😐😐
 
Back
Top Bottom