Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
AINA 4 ZA WANAWAKE AMBAO HUTAKIWI KUANZISHA NAO FAMILIA HASA UKIWA NA UMRI CHINI YA MIAKA 45.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Umri wa 20-45 ni umri muhimu Sana kwako kama kijana wa kiume. Huo ndio umri ambao unanguvu ya kujenga empire yako. Kumbuka mwanaume hazaliwi akiwa na thamani. Kama ulikuwa unajiuliza kwenye hesabu Value of X ni ipi basi ndio hiyo ambayo mwanaume unaitafuta. Huzaliwi nayo.
Hii ni tofauti na Mwanamke ambaye value of X anayo. Mwanamke anazaliwa akiwa na thamani. Yeye hana haja ya kupambana kutafuta Value of X. Wakati Uzuri wake ndio X yenyewe. Anachotakiwa yeye ni kutunza na kulinda thamani yake. Basi! Elewa kila Mwanamke ni Mzuri, hata hivyo hiyo haitaondoa ukweli kuwa Sio kila Mwanamke anamvuto. Wapo wazuri wasio na mvuto wa wazi.
Anyway! Naona nachochora.
Umri chini ya miaka 45, unatakiwa upambane kufa na kupona. Ndio umri WA kujijenga.
Umri huu ni mfupi Sana. Kutoka miaka 20 mpaka 45 ni almost 25 years. Ni miaka michache Sana.
Wakati huu ndio wakati wa ku-focus na ndoto zako. Tafuta pesa kadiri uwezavyo.
Sio muda wa kukimbizana na wanawake.
Watakupotezea target. Utajikuta ukifeli kama hautakuwa makini.
Elewa, hata uwe handsome boy kama sisi Watibeli(ambao uhandsome boy kwetu ni Jambo la kawaida na sio lakujivunia). Thamani ya uhandsome boy wako huondoka utakapofikisha miaka 30. Chini ya miaka 30 unaweza kujivunia uhandsome boy wako na pengine kuutumia kwa wanawake hasa wenye umri mdogo.
Lakini baada ya miaka 30, mambo hubadilika. Kitachoangaliwa, unakazi gani, kipato chako, unanafasi gani. Thamani ya mwanaume IPO kwenye KAZI, kujishughulisha na kujipata. Ukifeli hapo ndugu yangu umekwisha.
Miaka ya 30+ ndio umri utaoanza kutaka kuanzisha Familia na unatafuta mwanamke wa kumuita Mke na mama wakukuzalia watoto. Msaidizi wako. Ubavu wako.
Basi hawa ndio aina ya wanawake ambao unatakiwa uwaepuke kuanzisha nao familia;
1. Single Mother
Hili lishaongelewa Sana. Madhara ya know single mother yapo ya Muda mfupi na yapo ya Muda Mrefu.
Hata hivyo jitahidi kuanzisha familia na mwanamke wako akiwa Fresh. Sio uanzishe familia na mwanamke aliyekuwa na familia, au anayefanya muendelezo.
Asije kukudanganya mtu yeyote, hata nafsi yako. Kwa umri huo usioe Single Mother. Usijesema anamtoto mmoja, au sio wote wanatabia hizo. Noo!
2. Mwanamke anayekuzidi Kipato na mwenye hadhi kijamii kukushinda.
Mwanamke yeyote anayekuzidi kipato zaidi ya busy ya kipato chako huyo achana naye.
Mfano. Kipato chako ni 500k alafu mwanamke ni 750k. Huyo achana naye.
Asije akakudanganya mtu au ukajidanganya. Ooh! Mbona tunapendana! Acha ujinga. Upendo wa mwanamke niwa msimu tuu.
3. Aliyekuzidi Umri kuanzia miaka Mitano kuendelea.
Huyo ni Mzee kwako. Watu wazima wenyewe wenye akili timamu huoa vibinti vidogo vibichi. Unafikiri wao wajinga?
4. Aliyekuzidi Nguvu za Mwili;
Kuna wanawake ni vijeba haswa. Mwili mkubwa, wengine vikomazi, wengine wakakamavu kwelikweli. Wewe unataka kuanzisha familia na mwanamke wa aina hiyo mbaya zaidi kakuzidi. Hivi unajitakia Mema kweli? Hivi kichwani zimo?
Ukishakuwa Baba na Mume unatoka kwenye kuwa Mpenzi(Lover) unaingia kwenye Uongozi/ Kiongozi( Leadership/Leader). Sasa unaoa mwanamke mwili nyumba, kila themanini wewe kila sitini, anamiguvu wewe maskini huna lolote. Hivi utaweza kumuongoza kweli? Hivi hujui uongozi kuna wakati itakupasa utumie Mabavu huku hekma na busara ukiziweka pembeni.
Utaweza ku- enforce sheria za hapo nyumbani ikiwa mkeo kakuzidi nguvu ya mwili, au kakuzidi uchumi. Embu tuambie.
Tafuta mwanamke ambaye utammudu maeneo nyeti ya uongozi ndani ya familia.
Haya! Endeleza ukaidi!
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam