Tetesi: Air Tanzania kukamatwa. Ndege ya Rais haikamatwi kwa sheria za IATA

Tetesi: Air Tanzania kukamatwa. Ndege ya Rais haikamatwi kwa sheria za IATA

Hela inayopotea ni yetu sote. Siyo hela ya Magufuli au CCM.

Rais Magufuli, arudi nyuma mpaka mambo yalipoharibikia. Aliunganishe Taifa. Katika umoja na maelewano ya kitaifa, hata mkulima anaweza kushaurika, anaweza kutupatia nafuu ya deni, na anaweza kukubali kulipwa kidogo kidogo. Na ndege zikaendelea kuruka bila wasiwasi wowote. Hiyo inaweza kufanyika pia kwa wadai wengine.

Bila hivyo, Rais Magufuli atapambana sana lakini hatafanikiwa hata kimoja. Kila siku atazidi kudidimia katika mipango yake. Kwa sasa kuna mambo kibao hayaendi (hata kabla ya Covid 19):
1) ukuuaji wa uralii umeshuka kutoka 15% mpaka 3.6%

2) Ukuaji wa uwekezaji umeahuka toka 28% mpaka 4%

3) Thamani ya mauzo ya nje ya mazao ya kilimo yameshuka kwa 50%

4) Makusanyo ya kodi hayaongezeki pamoja na kuchukua vyanzo vote vya mapato vya halmashauri, miji na majiji

5) Misaada kutoka taasisi mbalimbali za kimataifa imeshuka kwa zaidi ya 60%

Wakati huo huo kuna sauti nyingi toka jamii ya kimataifa dhidi ya Serikali.

1) Mahusiano ya kimataifa yamezorota kiasi cha kunyoshewa vidole na taasisi mbalimbali kutokana na kutozingatia haki za binadamu, uhuru wa maoni, uhuru wa vyombo vya habari, utawala wa sheria, chaguzi za kidemokrasia, misingi ya demokrasia ya vyama vingi, sheria mbovu zinazodidimiza misingi ya uwazi na utawala bora. Haya yote yameifanya Serikali ya sasa kuonekana ni ya ajabu kwa vile inalipeleka taifa gizani badala ya kulipeleka kwenye mwanga.

2) Mauaji, upotezaji na mashambulio ya watu wenye mawazo pinzani dhidi ya serikali au Rais. Vitendo hivi vya hovyo vimeifanya Serikali kuwa unpopular kwa kila genuine person, bila ya kujali mtu huyo ana mlengo gani wa kisiasa.

3) Uanzishaji wa kundi la kijambazi la 'watu wasiojulikana' kwa nia ya kudhibiti wasiokuwa tayari kuisifia serikali, n.k. Kundi hili limeharibu kabisa image ya serikali na Rais.

Nadhani Rais anajua wazi kuwa njia zilizofikiriwa kuwa zingeisaidia Serikali yake kupata mafanikio, hazifanyi kazi. Hivyo ni vema kurudi nyuma na kutafakari, na kisha kutafuta mbinu mpya kwa kutumia mawazo mapya kutoka kwa watu wapya. Bila hivyo, atakuja kutoka Ikulu akiwa ameinamisha kichwa kwa sababu ya kukosa cha kujivunia kama alama nzuri aliyoiacha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu uzi pasi comment ya huyu Bia yetu ni batili


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unayeanza na herufi ndogo baada ya kituo na kuanza na herufi kubwa sehemu isiyostahili sidhani kama hiyo akili utakuwa umenizidi.
Ujumbe hujapata? hicho ndicho kitu cha maana kuliko punctuation!!
 
Kama hukujua, mkulima wa South Afroika bado anadai bilioni 40 zake na riba kubwa tu, katika hali isiyo kawaida, ametoa waranty nchi nyingi isipokuwa India ndio walisema hawata kamata hizi ndege.
Lakini pia, Air Tanzania zimepakiwa tu viwanjani isipokuwa bomberdier tatu zinafanya safari za ndani kwa shida sana kwakuwa hakuna abiria, [matajiei waishi kama mashetani].

Jumatano iliyopita MAGUFULI alituma ndege yake[ya Rais] kwenda madagaska kuchukua mitishamba, haikuwa bahati mbaya na si kwamba hakuna Bomberdier zaidi ya 8 zilizopaki, hapana ila zitakamatwa ndio maana akatoa ndege ambayo ina IMMUNITY kutokamatwa .

Jana ndege ya RWANDA, RWANDAIR imetua mwanza na imesaini kandarasi na kiwanda cha mwanza kubeba minofu na kuacha mapanki yaliwe na wanyonge, jiulize kwanini JIWE hana guts za kusema lazma samaki wabebwe na AIR TANZANIA kwa jinsi mnavyomjua alivyo ? ni kwasababu huko nje Ndege ikienda hairudi, na hii korona nakwambia mkulima atafugia hata MABATA huko ndani.


RWANDAIR YABEBA SAMAKI MWANZA KWENDA UBELGIJI
WAZIRI WA MAGUFULI AKAPELEKA NGENGA ZAKE PALE KUZINDUA UBEBAJI, watanzania hakuna wa kuhoji maana hofu kuu imejaa, Shirika la Ndege la Rwanda RwandAir, limezindua safari zake za ndege ya mizigo kutoka jijini Mwanza nchini Tanzania kwenda Brussels Ubelgiji kwa lengo la kusafirisha samaki kwenda katika soko barani Ulaya.

Image may contain: one or more people

Kwa hiyo umefulahi sana?
Ila ni haki yako, pia tuanataka kujua hiyo minofu inaenda nchi gani? Je hiyo nchi tayari tuna mikataba ya kibiashara kupitia ATCL?
 
SGR mkandarasi hana hela, hata wazabuni toka january hawajalipwa, kila kitu hakiendi, KUONGOZA NCHI SI KUHESABU IDADI YA SAMAKI ZIWA VICTORIA
Pupa za huyu mzee kufanya mambo yote kwa pamoja atamaliza mda amekamilisha na Ubungo interchange na Daraja la Sarenda hata lile la Mwanza sidhani kama atamaliza
 
Kwahiyo unaona JIWE alikuwa na BILIONI 40 za kumlipa?
Hujui ndio mana kapeleka ndehge ya raisi kubeba miti shamba MADAGASKA?
Sasa kesi iliishaje boss...Na kwa nini itue India pekee kwan sisi tuna miadi na India? Tupe data yawezekana unazo nyingi.
 
Back
Top Bottom