Tetesi: Air Tanzania kukamatwa. Ndege ya Rais haikamatwi kwa sheria za IATA

Tetesi: Air Tanzania kukamatwa. Ndege ya Rais haikamatwi kwa sheria za IATA

Na sasa Magufuli anasimamia show tangu 2015 hadi sasa 2020 kaboresha sana Vituo vya afya 370 nchi mzima,Hospitali za Wilaya 60+,Umeme Vijijini 85% ,Maji mini na Vijijini 80+%,Ujambazi umepungua ndani ya Utawala wake ,uwajibikaji mzuri katika taasisi za serikali ,Uhuru wa kuishi na mengineyo😁😁😁👍
Hayo unayosema ni majuku ya kawaida sana ya serikali...
Kama ndo yanayokufanya umsifie basi hujui kuwa hujui...
 
Acha kupotosha uma bas. Sio kwamba air Tanzania haiwez kwenda ulaya kwa ajiri ya mkulima. Sio kumiliki ndege ndo kuwa na uwezo wa kutua popote utakapo, kila kitu kina taratibu zake.

Leseni ya Rwandair sio sawa naya air Tanzania, Rwanda leseni yao inawaruhusu kutua viwanja vya ulaya sisi hiyo bado hatuna, na usizanie kupata leseni ya kutua ama kupita kwenye anga la ulaya ni kitu rahisi, inachukua mda.

Ata bus uwezi ipeleka tu unapo taka kwakuwa umepata abiria wa huko pasipo kuwa nakibari cha hiyo route
Usingewajibu. Hawa waache wajipe nafuu. Maana wiki hii wamekula vichapo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wajinga wenu huko juu hawakujua hilo wakanunua madege na kupark sasa zaidi ya miaka mitatu? Wanaweza nini kama mambo ya kawaida kama hayo yanawashinda? ATCL ilikuwepo na EAA kabla take kwa nini hawakuweza kujifunza kutokana na mafanikio au failures za mashirika hayo mawili? Musukuma ana kampuni yake ya Mabasi yakifanya safari kati ya Geita na Chato na Mwanza si angefaa zaidi kuendesha ATCL kuliko hayo yaliyokabithiwa Shirika kwa Usukuma tu? ATCL ina ndege nyingi zaidi kuliko RwandAir lakini wanachukua biashara ya samaki tukiangalia. What good are we?
Kupata leseni ya kimataifa hasa kwenye mataifa makubwa sio kitu rahisi kama unavyofikiria. Na huyo king msukuma unaemsea wenda ujui magari yake yalivyo, atawezaje kuendesha shirika kama Air Tanzania ikiwa mabas yake tu yamemshinda magari mabovu ana bus ata moja ya luxury, kashindwa kuchukua route ata moja ya mwanza-dar au mwanza- arusha ndio ataweza kuendesha ATCL?
 
Hawa jamaa ndio maana Mkapa aliwaita malofa na wapumbavu.
Hivi kuna mpumbavu kama anaye weza kununua ndege kwa kulipa cash ili atambe kumbe baada ya hapo hana hata hela za kununulia PPE kuponya maisha ya watumishi wa Afya hadi apitishe bakuli?
Lofa huyo kisha ndege hizo anazipaki tuu airport hazina la kufanya huku akilipa wafanyakazi na marubani bure?
Hamjitambui jamaa yangu, kila kitu mnakwama na majirani wamegundua kushirikiana nanyi ni gundu tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ikikamatwa Mnamuumiza rais au ninyi wenye! Watanzania punguzeni upumbavu wa akili! Too much nonsense! Hamuwezi kutwa kuitakia nchi Mabaya, ifikie hatua kila mtu awe responsible na Nchi yake.
Responsible wa kitu gani? Serikali isiyotaka ushauri na kila jambo inajifanya wababe sio ya kuonea huruma kwa ujinga huo.
Unadhani nani anaitakia mabaya kama sio wenyewe ndio wanajitakia mabaya? Nchi imekuwa ya kishamba mno awamu hii na nyie mavuvuzela ndio mnachagia upumbavu kutamalaki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kuna mpumbavu kama anaye weza kununua ndege kwa kulipa cash ili atambe kumbe baada ya hapo hana hata hela za kununulia PPE kuponya maisha ya watumishi wa Afya hadi apitishe bakuli?
Lofa huyo kisha ndege hizo anazipaki tuu airport hazina la kufanya huku akilipa wafanyakazi na marubani bure?
Hamjitambui jamaa yangu, kila kitu mnakwama na majirani wamegundua kushirikiana nanyi ni gundu tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani kwa akili zako za kilofa lofa unafikiri unarusha tu ndege nchi yeyote ile bila vibali sio? Mdude Nyagali keshakamatwa na kete za unga huko Mbeya, mateja wakubwa nyie.
 
Hili swala la mapanki nakumbuka liliwahi kuleta mtafaruku huko nyuma baada ya mzungu mmoja kutoa filamu namna wakazi wa kanda yetu pendwa kubaki wanaambulia mifupa ya samaki baada ya minofu kunyofolewa kupelekwa ulaya, naomba serikali wasimamishe haraka utaratibu huu ili tuokoe minofu ya samaki kwa ajili ya lishe ya watoto na akina mama wajawazito, kwa Tanzania udumavu kwa watoto upo zaidi ya asilimia 35, kwa hiyo tulichukulie hili swala seriously...
 
Na sasa Magufuli anasimamia show tangu 2015 hadi sasa 2020 kaboresha sana Vituo vya afya 370 nchi mzima,Hospitali za Wilaya 60+,Umeme Vijijini 85% ,Maji mini na Vijijini 80+%,Ujambazi umepungua ndani ya Utawala wake ,uwajibikaji mzuri katika taasisi za serikali ,Uhuru wa kuishi na mengineyo😁😁😁👍

Sasa mbona tuna mashine mbili tu za kupimia korona nchi nzima, haya ni mafanikion gani kwenye tasnia ya agya?
 
Acha kupotosha uma bas. Sio kwamba air Tanzania haiwez kwenda ulaya kwa ajiri ya mkulima. Sio kumiliki ndege ndo kuwa na uwezo wa kutua popote utakapo, kila kitu kina taratibu zake.

Leseni ya Rwandair sio sawa naya air Tanzania, Rwanda leseni yao inawaruhusu kutua viwanja vya ulaya sisi hiyo bado hatuna, na usizanie kupata leseni ya kutua ama kupita kwenye anga la ulaya ni kitu rahisi, inachukua mda.

Ata bus uwezi ipeleka tu unapo taka kwakuwa umepata abiria wa huko pasipo kuwa nakibari cha hiyo route
Leseni ya kupita kwenye anga inalipiwa mkuu sio swala la muda ni swala la kua na hela za kulipia ambazi hazipo hujiulizi kwanini ndege nyingi hua zinapitia sana baharini?
 
Ndege - Kimeo

Stieglers - bwawa limeshaingia luba

Bado SGR
SGR nayo ikibuma basi mzee wa chato atapiga marktime time bila kuacha legacy yoyote ya maana
Pengine ndo mana kajichimbia Chato. Pengine akiibuka huko atakuja na kioja kingine. Tuvute subra.
 
Na sasa Magufuli anasimamia show tangu 2015 hadi sasa 2020 kaboresha sana Vituo vya afya 370 nchi mzima,Hospitali za Wilaya 60+,Umeme Vijijini 85% ,Maji mini na Vijijini 80+%,Ujambazi umepungua ndani ya Utawala wake ,uwajibikaji mzuri katika taasisi za serikali ,Uhuru wa kuishi na mengineyo😁😁😁👍
Uhuru wa kuishi? Na ugumu wote huu? Hii habari ya huduma za afya, dawa bei juu au hakuna. Kuna makundi ya watu walikuwa wanapata huduma bure enzi hizo. Siku hizi hakuna cha wazee wala watoto.

Bila kuinua kilimo, hakuna maendeleo ya kweli vijijini. Hata uweke umeme kwenye nyumba zs tope!
 
Acha kupotosha uma bas. Sio kwamba air Tanzania haiwez kwenda ulaya kwa ajiri ya mkulima. Sio kumiliki ndege ndo kuwa na uwezo wa kutua popote utakapo, kila kitu kina taratibu zake.

Leseni ya Rwandair sio sawa naya air Tanzania, Rwanda leseni yao inawaruhusu kutua viwanja vya ulaya sisi hiyo bado hatuna, na usizanie kupata leseni ya kutua ama kupita kwenye anga la ulaya ni kitu rahisi, inachukua mda.

Ata bus uwezi ipeleka tu unapo taka kwakuwa umepata abiria wa huko pasipo kuwa nakibari cha hiyo route
Kwaiyo kibali tunapata lini? Kumbuka kuyapaki madege hayo ni gharama ya kufa mtu.
 
Kama hukujua, mkulima wa South Afroika bado anadai bilioni 40 zake na riba kubwa tu, katika hali isiyo kawaida, ametoa waranty nchi nyingi isipokuwa India ndio walisema hawata kamata hizi ndege.

Lakini pia, Air Tanzania zimepakiwa tu viwanjani isipokuwa bomberdier tatu zinafanya safari za ndani kwa shida sana kwakuwa hakuna abiria, [matajiei waishi kama mashetani].

Jumatano iliyopita MAGUFULI alituma ndege yake[ya Rais] kwenda madagaska kuchukua mitishamba, haikuwa bahati mbaya na si kwamba hakuna Bomberdier zaidi ya 8 zilizopaki, hapana ila zitakamatwa ndio maana akatoa ndege ambayo ina IMMUNITY kutokamatwa.

Jana ndege ya RWANDA, RWANDAIR imetua mwanza na imesaini kandarasi na kiwanda cha mwanza kubeba minofu na kuacha mapanki yaliwe na wanyonge, jiulize kwanini JIWE hana guts za kusema lazma samaki wabebwe na AIR TANZANIA kwa jinsi mnavyomjua alivyo ? ni kwasababu huko nje Ndege ikienda hairudi, na hii korona nakwambia mkulima atafugia hata MABATA huko ndani.

RWANDAIR YABEBA SAMAKI MWANZA KWENDA UBELGIJI

WAZIRI WA MAGUFULI AKAPELEKA NGENGA ZAKE PALE KUZINDUA UBEBAJI, watanzania hakuna wa kuhoji maana hofu kuu imejaa, Shirika la Ndege la Rwanda RwandAir, limezindua safari zake za ndege ya mizigo kutoka jijini Mwanza nchini Tanzania kwenda Brussels Ubelgiji kwa lengo la kusafirisha samaki kwenda katika soko barani Ulaya.

Image may contain: one or more peopleView attachment 1449006ya
AIR TANZANIA/Ndege ya Urais inatumika kubebea miti shamba, dawa ya kienyeji huku wenzetu wakibeba samaki kuuza ulaya​
Kweli tunakazi awamu hii. Nchi haiendeshwi kwa amri tu bali hekima, busara na maarifa. Tutapata hasara sana kuhusu ndege. Kwasasa mambo mengi bado hayajulikani na yanafichwa kama corona. Itakapokuja kujulikana checks and balance za ATCL ni wakati mkuu alishang'atuka na kila mtu atahuzunika.
 
Umemaliza kabisa ambae hata elewa hapa basi tena
Hela inayopotea ni yetu sote. Siyo hela ya Magufuli au CCM.

Rais Magufuli, arudi nyuma mpaka mambo yalipoharibikia. Aliunganishe Taifa. Katika umoja na maelewano ya kitaifa, hata mkulima anaweza kushaurika, anaweza kutupatia nafuu ya deni, na anaweza kukubali kulipwa kidogo kidogo. Na ndege zikaendelea kuruka bila wasiwasi wowote. Hiyo inaweza kufanyika pia kwa wadai wengine.

Bila hivyo, Rais Magufuli atapambana sana lakini hatafanikiwa hata kimoja. Kila siku atazidi kudidimia katika mipango yake. Kwa sasa kuna mambo kibao hayaendi (hata kabla ya Covid 19):
1) ukuuaji wa uralii umeshuka kutoka 15% mpaka 3.6%

2) Ukuaji wa uwekezaji umeahuka toka 28% mpaka 4%

3) Thamani ya mauzo ya nje ya mazao ya kilimo yameshuka kwa 50%

4) Makusanyo ya kodi hayaongezeki pamoja na kuchukua vyanzo vote vya mapato vya halmashauri, miji na majiji

5) Misaada kutoka taasisi mbalimbali za kimataifa imeshuka kwa zaidi ya 60%

Wakati huo huo kuna sauti nyingi toka jamii ya kimataifa dhidi ya Serikali.

1) Mahusiano ya kimataifa yamezorota kiasi cha kunyoshewa vidole na taasisi mbalimbali kutokana na kutozingatia haki za binadamu, uhuru wa maoni, uhuru wa vyombo vya habari, utawala wa sheria, chaguzi za kidemokrasia, misingi ya demokrasia ya vyama vingi, sheria mbovu zinazodidimiza misingi ya uwazi na utawala bora. Haya yote yameifanya Serikali ya sasa kuonekana ni ya ajabu kwa vile inalipeleka taifa gizani badala ya kulipeleka kwenye mwanga.

2) Mauaji, upotezaji na mashambulio ya watu wenye mawazo pinzani dhidi ya serikali au Rais. Vitendo hivi vya hovyo vimeifanya Serikali kuwa unpopular kwa kila genuine person, bila ya kujali mtu huyo ana mlengo gani wa kisiasa.

3) Uanzishaji wa kundi la kijambazi la 'watu wasiojulikana' kwa nia ya kudhibiti wasiokuwa tayari kuisifia serikali, n.k. Kundi hili limeharibu kabisa image ya serikali na Rais.

Nadhani Rais anajua wazi kuwa njia zilizofikiriwa kuwa zingeisaidia Serikali yake kupata mafanikio, hazifanyi kazi. Hivyo ni vema kurudi nyuma na kutafakari, na kisha kutafuta mbinu mpya kwa kutumia mawazo mapya kutoka kwa watu wapya. Bila hivyo, atakuja kutoka Ikulu akiwa ameinamisha kichwa kwa sababu ya kukosa cha kujivunia kama alama nzuri aliyoiacha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom