Air Tanzania yapigwa Marufuku kufanya safari zake Katika nchi 28 za Umoja wa Ulaya kwasababu za Kiusalama

Mbona tumewekwa category ya Madikiteta jamani au ni mimi natafsiri vibaya?
 
Wahuni hawa,wanaogopa kisiwatokee kilichofanywa na Emirates,Qatar air na Ethiopian airlines kumiliki soko na ndege zao kuonekana hazina mpango au kudoda kwenye biashara....
 
Umoja wa Ulaya EU umezuia Shirika la Air Tanzania Kuruka Kwenye Anga lake Kwa kile ilichodia ni kutokidhi viwango vya usalama.

Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza kuzuia ndege za shirika la ndege la Air Tanzania kuingia katika anga la nchi wanachama wa umoja huo, ambazo ni jumla ya nchi 27, kwa kile ambacho jumuiya hiyo imeeleza kuwa shirika hilo halijakidhi vigezo vya usalama wa anga vya kimataifa.

“Umoja wa Ulaya leo umerekebisha orodha yake ya mashirika ya ndege yanayozuiwa kuingia, au kuwekewa vikwazo vya kiutendaji katika kuingia Umoja wa Ulaya,” taarifa hiyo ambayo The Chanzo imeiona inaeleza. “Kutokana na taarifa hii, Air Tanzania imeongezwa kwenye orodha hiyo.”

Taarifa hiyo inaeleza zaidi kuwa sababu kubwa ya kuiongeza Air Tanzania kwenye mashirika yaliyozuiwa ni zile za kiusalama wa anga ambazo zimeainishwa na Wakala wa Usalama wa Anga wa Umoja wa Ulaya (EASA).

Kutokana na taarifa hiyo, Air Tanzania inakuwa sehemu ya mashirika 129 yaliyozuiwa kuingia Umoja wa Ulaya. Air Tanzania imejumuishwa pamoja na mashirika saba mengine ambayo taarifa hiyo imetaja kuwa yana changamoto kubwa, ikiwemo Air Zimbabwe la Zimbabwe, Avior Airlines la Venezuela, Blue Wing Airlines la Suriname, Iran Aseman Airlines la Iran, Fly Baghdad la Iraq and Iraqi Airways la Iraq.


Akizungumzia orodha hiyo, Kamishna wa Usafiri Endelevu na Utalii Umoja wa Ulaya, Apostolos Tzitzikostas, amenukuliwa akisema kuwa yuko tayari kushirikiana na Air Tanzania kuiwezesha kukidhi vigezo husika.

“Uamuzi wa kuijumuisha Air Tanzania katika Orodha ya Usalama wa Anga ya EU ni kwa sababu ya dhamira yetu thabiti ya kuhakikisha kuwa kuna viwango vya juu zaidi vya usalama kwa abiria barani Ulaya na duniani kote,” amesema Tzitzikostas.

Toka mwaka 2016, Tanzania imekuwa ikiboresha shirika lake la Air Tanzania, hasa kwa kununua ndege mpya. Shirika hilo kwa sasa lina ndege kadhaa, ikiwemo ndege mbili za Boeing

================================

The European Commission has updated the list of air carriers banned from flying in EU airspace due to non-compliance with international safety standards. Following the latest update, Air Tanzania was added to the list.

Reasons for the ban


The decision to include Air Tanzania on the list is based on safety concerns identified by the European Union Aviation Safety Agency (EASA). The airline also failed to obtain a third country operator (TCO) permit.

Apostolos Tsitsikostas, Commissioner for Sustainable Transport and Tourism, said

Today, the total number of airlines banned from flying in EU airspace is 129.

  • 100 airlines from 15 countries were included in the list due to inadequate safety oversight by their respective aviation authorities.
  • The 22 Russian airlines were added after the complete closure of EU airspace to Russian aircraft on 27 February 2022 due to the invasion of Ukraine.
  • Seven airlines are included in the list due to specific safety concerns: Air Tanzania (Tanzania), Air Zimbabwe (Zimbabwe), Avior Airlines (Venezuela), Blue Wing Airlines (Suriname), Iran Aseman Airlines (Iran), Fly Baghdad (Iraq) and Iraqi Airways (Iraq).

My Take
Naishauri Serikali na ATCL wawekezd zaidi Nguvu zao za kibiashara Bara la Asia, South America , Africa na usafiri wa Ndani badala ya kujikomba huko ambako hakuna chochote Cha maana tunapata.
 
NANUKUU.


Akizungumzia orodha hiyo, Kamishna wa Usafiri Endelevu na Utalii Umoja wa Ulaya, Apostolos Tzitzikostas, amenukuliwa akisema kuwa yuko tayari kushirikiana na Air Tanzania kuiwezesha kukidhi vigezo husika.
Hapo wanataka ubia kwa nguvu. Hawapendi kuliona shirika letu likijiendesha lenyewe.
 
“Tunawahimiza Air Tanzania kuchukua hatua za haraka na thabiti kushughulikia masuala haya ya usalama wa anga. Kamisheni yetu itakuwa tayari kutoa msaada kwa mamlaka za Tanzania katika kuboresha usalama wa ndege za Air Tanzania na kuwezesha kuweza kufikia vigezo vyote vya usalama wa ndege kimataifa,” Tzitzikostas anaeleza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…