Air Tanzania yapigwa Marufuku kufanya safari zake Katika nchi 28 za Umoja wa Ulaya kwasababu za Kiusalama

Air Tanzania yapigwa Marufuku kufanya safari zake Katika nchi 28 za Umoja wa Ulaya kwasababu za Kiusalama

Habari kwa kina ...

EU yaiongeza Air Tanzania kwenye orodha ya marufuku
snymok-%D1%8Dkrana-2024-12-13-v-17.24.22.png

Kampuni ya ndege ya Air Tanzania. Picha: Picha za Getty

Tume ya Ulaya imesahisisha (update) orodha ya ndege zilizopigwa marufuku kuruka katika anga ya Umoja wa Ulaya kwa sababu ya kutofuata viwango vya usalama vya kimataifa. Kufuatia sahihisho la hivi punde, Air Tanzania iliongezwa kwenye orodha ya kupigwa marufuku.


Sababu za kupiga marufuku

Uamuzi wa kuingiza Air Tanzania kwenye buku jeusi la orodha hiyo inatokana na masuala ya usalama yaliyoainishwa na Wakala wa Usalama wa Anga wa Umoja wa Ulaya (EASA ).

Shirika la ndege pia lilishindwa kupata kibali cha waendeshaji wa nchi ya tatu (TCO) kwa kimombo - third country operator TCO. Bw. Apostolos Tsitsikostas, Kamishna wa Usafiri Endelevu na Utalii, alisema:
“Uamuzi wa kuingiza Air Tanzania kwenye buku lenye orodha ya marufuku , inaonyesha dhamira yetu ya endelevu ya kuweka viwango vya juu vya usalama kwa abiria barani Ulaya na duniani kote. Tunatoa wito kwa shirika la ndege la Air Tanzania kuchukua hatua za haraka kushughulikia maswala haya."

Hali ya ujumla ilivyo sasa
Leo, jumla ya mashirika ya ndege yaliyopigwa marufuku kuruka katika anga ya Umoja wa Ulaya ni 129.
  • Mashirika 100 ya ndege kutoka nchi 15 yalijumuishwa katika orodha hiyo kutokana na uangalizi duni wa usalama wa mamlaka zao za usafiri wa anga.
  • Mashirika 22 ya ndege ya Urusi yaliongezwa baada ya kufungwa kabisa kwa anga ya Umoja wa Ulaya kwa ndege za Urusi tarehe 27 Februari 2022 kutokana na uvamizi wa Ukraine.
  • Mashirika saba ya ndege yamejumuishwa kwenye orodha hiyo kutokana na masuala mahususi ya kiusalama: Air Tanzania (Tanzania), Air Zimbabwe (Zimbabwe), Avior Airlines (Venezuela), Blue Wing Airlines (Suriname), Iran Aseman Airlines (Iran), Fly Baghdad (Iraq) na Shirika la Ndege la Iraqi (Iraq) .

Vikwazo vya uendeshaji
Mashirika mawili ya ndege, Iran Air (Iran) na Air Koryo (Korea Kaskazini) , yanaweza kuendesha safari za ndege hadi EU, lakini kwa kutumia aina fulani za ndege pekee.

Hatua hizi zinasisitiza umuhimu wa kudumisha viwango vya juu vya usalama kwa wachukuzi wote wa anga wanaofanya kazi katika anga ya Ulaya
 
Tusishutumu kwanza. Tuone je tunapewa standard tofauti na wenzetu. Kama kuna double standards au standards zimewekwa kihuni ili tushindwe ndipo tuseme kuna hujuma. Lakini kama ni hatujatimiza vigezo halali basi tukavifanyie kazi, tutakuwa bora zaidi. Maana hata hizo route zingine watu watasita kupanda wakiona hatujatimiza vigezo vya EU.
Wewe hujiuzi tu kwanini iwe sasa!!? Wakati ATCL haina route yoyote ya kwenda kwenye nchi za EU.
 
Usalama kwenye mabasi tu hatuna tukahamia na ndege
Sasa mnapigwa marufuku hata hamjatua Ulaya
Acha Kagame atambe kwa kweli
Rwandair inatua Heathrow
Ulaya hawana rushwa unapata leseni kihalali hata iwe ya pikipiki
 
Wazungu bhana ATCL hana safari yeyote huko Ulaya ila wanasema ATCL haina vigezo na pia kwa kauli hiyo hata usafiri wa ndani sio salama kwa hizo ndege wanachotakiwa ni kukaa nao chini ili wafikie viwango vyao maana hii biashara ina ushindani sana bila kukaza watatolewa nje.
 
Engineer Ladislaus Matindi mbobezi wa sekta ya Anga Afrika aliyetolewa Dakar Senegal kuja Tanzania kuliendesha shirika la Air Tanzania amemwachia zigo zito mkurugenzi mkuu mpya

1734112802538.jpeg

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) Eng. Peter Ulanga, leo Novemba 26, 2024 (kushoto) akikabidhiwa mikoba na Engineer Ladislaus Matindi aliyestaafu baada ya kutumikia shirika la Air Tanzania lilipopata ujio wa pili kufuatia serikali kuwekeza kulifufua shirika la Air Tanzania lililokuwa limekosa mtaji wa kuliendesha kama ndege n.k .


Eng. Ladislaus Evarist Matindi,
1734113724742.jpeg

is a master’s degree holder in Telecommunication Engineering and MBA degree in International Business. The outgoing managing director, worked with Air Tanzania Company Limited (ATCL) doubling as Managing Director and CEO of Air Tanzania Company Limited (ATCL). Prior to joining the ATCL, he was the CEO of the EGNOS Africa Joint Programme Office (JPO), a regional structure created to coordinate the deployment of the European Union GNSS/EGNOS services in Africa with its headquarters in Dakar, Senegal. He also served various aviation industry related to Management and Functional positions at the East African Community (EAC) Secretariat and in Tanzania Civil Aviation Authority. He is a well-known in aviation professional through his participation in EAC, SADC, COMESA, AFCAC, AU, USA, EU, and ICAO aviation related programmes.

Ladislaus Matindi is an aviation professional with 30+ years of experience covering various disciplines of the aviation sector.
 
Usalama kwenye mabasi tu hatuna tukahamia na ndege
Sasa mnapigwa marufuku hata hamjatua Ulaya
Acha Kagame atambe kwa kweli
Rwandair inatua Heathrow
Ulaya hawana rushwa unapata leseni kihalali hata iwe ya pikipiki
Kagame hana ndege yule shirika ni la hao mabeberu hata uwanja wa ndege unaendeshwa na mabeberu. Uwanja wake unatumika kusafirisha madini yanayoibiwa huko DRC na Kongo. Siku DRC ikithibiti madini yake ndio kifo cha Rwanda mkuu.
 
Unaweza ukawa hauna route lakini una kibali cha kutua EU. Usikimbilie kusema hujuma, tuangalie kama tumetimiza vigezo halali.
Huyo ni kati ya wazee wa kutafuta mchawi. Sasa EU ituhujumu kwa lipi wakati tuna ndege chache ambazo hata sio tishio kwa biashara yao waache kuhujumu emirates ambao wanaweka oda hata ya ndege 200 kwa wakati mmoja.
 
Hapo wamelinda interests zao. Hata huku ukijichanga ununue vi bus vyako viwili vitatu lazima ukae vizuri kwanza na ulio wakuta barabarani la sivyo utasababishiwa ajali na kutoka barabarani
 
Hawa EU ni waseng tu mandege yao ndio yanaongoza kwa kuanguka duniani. ATCL waendelee kwenda nchi za Brics na Brics ipambane ukue zaidi na zaidi ili tuachane na hawa mabeberu majinga.
Majitu mapumbavu kama wewe ndiyo yanasimamia uchaguzi wa serikali za mitaa, hivyo inataka hata Ulaya wachakachue. Ndege zingekuwa zinarushwa hovyo hovyo kama unavyotaka unadhani kungekuwa na usalama?
 
Back
Top Bottom