Air Tanzania yapigwa Marufuku kufanya safari zake Katika nchi 28 za Umoja wa Ulaya kwasababu za Kiusalama

Air Tanzania yapigwa Marufuku kufanya safari zake Katika nchi 28 za Umoja wa Ulaya kwasababu za Kiusalama

Kwa sababu wanaubia na mashirika ya hao Mabeberu. ATCL haina ubia na shirika lolote la EU ndio maana wanaanza kuwekewa vikwazo. Wazungu ni mashetani yanayoishi hapa duniani.
Tusishutumu kwanza. Tuone je tunapewa standard tofauti na wenzetu. Kama kuna double standards au standards zimewekwa kihuni ili tushindwe ndipo tuseme kuna hujuma. Lakini kama ni hatujatimiza vigezo halali basi tukavifanyie kazi, tutakuwa bora zaidi. Maana hata hizo route zingine watu watasita kupanda wakiona hatujatimiza vigezo vya EU.
 
Hakuna viongozi wenye kukasirika; yaani wakikasirika wanaogopa kuchukiwa na watu kuwasema vibaya. Unawezaje kuwekwa kwenye orodha yenye makampuni sijui ya wapi na wapi huko... Ni kuendekeza ufisadi tu.
 
Ni kwasababu Air Tanzania ina taswira ya state owned corporation na ukitizama Tanzania inaonekana kama ina kiburi kwenye masuala ya haki za kidemokrasia, nadhani maamuzi kama haya tuyategemee.

Air Tanzania inapaswa kubinafsishwa kiasi fulani kama wanataka liwe shirika competitive, kama ilivyokuwa Kenya Airways, yaani liwe na sura ya private company na sio state owned corporation
 
Back
Top Bottom