Airtel inazidi kutanua soko la Unlimited internet, Vodacom na Tigo wakiendelea kushupaza shingo watastuka soko lishamezwa

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760


N:B: Ni muhimu kupima Network kwenye eneo lako kabla ya kununua kuzuia hasara.

Haya mambo ya kununua vifurushi vya buku buku unaweza kujikuta unaunga mara 3 na zaidi kwa siku, haba na haba hujaza kibaba mwisho wa mwezi umechoma 80k hadi laki kwenye bando

Suluhisho ni huduma ya unlimited internet, Hulipii Gb unalipia speed,

Kuna unlimited ya waya inaitwa fibre, kuna kampuni kama Zuku fibre, Halotel fibre, Ttcl fibre, Tigo / Yas fibre, n.k. unavutiwa waya mpaka nyumbani lakini changamoto yake huwezi kutembea nayo, ipo maeneo machache ya mjini na umeme ukikatika kifaa kinazima.

Makampuni ya simu wakaleta unlimited internet unayoweza kuhama nayo lakini changamoto ilikuwa gharama , Mfano Vodacom na Tigo kifaa (router) cha bei ya chini ni 250,000, Kifurushi cha chini kabisa ni 120,000 kila mwezi, ni wachache sana wanaweza kumudu.

Airtel wameona fursa ya kulikamata soko kwa kudeal na gharama, kwa shilingi 110,000 unapewa router bure iliyoungwa bando la 110k kwa mwezi mzima na miezi ijayo unaweza kuunga kifurushi cha elf 70, 110k, 150k, n.k. Bando la elf 70 limekuwa kinara kwa gharama rafiki.

mitandao mingine wapunguze bei za vifurushi vya unlimited lasivyo watakuja kustuka Airtel kajitanua kawa Monopoly kameza soko
 
Pia vifaa vyao bei sana.
 
fiber ya tigo tamu sana 55000, mbs 20 unlimited
 
Subiri Starlink anakuja, wataita maji mma wawaulize safaricom Kenya yanayowakuta!!
 
Unajua maana ya neno ''unlimited''? Kama ni unlimited mambo ya vifurishi yanatoka wapi tena?
 
KUna viti muwe mnashirikisha akili.

Hivi ni Watanzania wangapi wanaweza kuafford hizo huduma?

Buku buku ndio uwezo wa Watanzania 99.9%
Mabando ya buku buku yana gharama zaidi, unaweza kujikuta umeunga mara 3 kwa siku, kwa mwezi umefyeka elf 90.

Halafu uzuri wa router huombwi hela ya vocha 😀
 

( Hulipii tena gb unalipia speed)

Wizi umejificha hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…