View attachment 3170731
Haya mambo ya kununua vifurushi vya buku buku unaweza kujikuta unaunga mara 3 na zaidi kwa siku, haba na haba hujaza kibaba mwisho wamwezi umechoma 80k hadi kilo kwenye bando
Suluhisho ni huduma ya unlimited internet na hadi sasa Airtel ndie mwenye nafuu, Gharama za matumizi binafsi ya data zimepunguzwa sana Na nyumbani/ofisini hakuna tena ule usumbufu wa kuombwa hela za bando
Vodacom na tigo wana huduma za unlimited lakini ni ghali, Kujisali inabidi ununue router ya bei ya chini 250,000, vifurushi vyao vya chini kabisa ni 120,000
Airtel wana gharama nafuu, kwa 110,000 utapewa router iliyoungwa bando la mwezi mzima na miezi ijayo unaweza kuchagua kifurushi cha elf 70, 110k, 150k, n.k. kulingana na speed (hulipii tena gb unalipia speed)
Vodacom na Tigo wakiendelea kukomaa na bei zao za 120k watakuja kustuka soko lishamezwa
Halotel wapo kimya, itapendeza waje na bei za kizalendo kama ilivyo kawaida yao.