Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 8,252
- 18,335
Mkuu kuna watu wameniuliza hapo juu nimewaelekeza but incase hujaona iko hivi:zielezee kdgo mkuu zinapatikan vip?
kwahyo mkuu hoja yako hapo ni ipi watu wasinunue hzo route kisasa watanzania wengi hawana uwezo au wafanya biashara wasiziuze kwasababu umaskin mkubwa? Maana kama bando za buku zipo hakuna aliekatazwa kununua, na ambao wana uwezo wananunua hzo route kwasababu uwezo unawaruhusu we malalamiko yako upande upi ? Maan toka mwanzo wa uzi nakuona umeng'ng'ania 99% wananunua bando za bukuZinanunuliwa na wachache sana. Na hao wanaonunua zinawashinda wanarudi tena kwenye mabando ya siku na wiki.
Tatizo mnafikiri Tanzania ni hapo M/City na maduka makubwa zinazouzwa hizo router
Watanzania wengi kwanza hawajui hata router ni nini.
Hili taifa bado lina umasikini mkubwa sana wa kipato cha mtu mmoja mmoja
Kweli Mtanzania wa kawaida atoe 250k au 110k kwa ajili ya intaneti? Tembeeni vijana mjionee uhalisi wa maisha ya Mtanzania
Lakini mkuu hii siyo UNLIMITED...Mkuu kuna watu wameniuliza hapo juu nimewaelekeza but incase hujaona iko hivi:
Hizi ni laini special kwa ajili ya internet pekee, hazipigi wala kupokea simu, text wala pesa. Unazipata kwenye maduka ya halotel na unaweza ukanunua pamoja na device (router) yake ambazo zipo kuanzia elfu hamsini na kwenda juu. Lakini kama unaona hauwezi kununua hizo device unaweza kuchukua laini pekee ukawa unaitumia kupitia simu.
Vifurushi vyake
Wiki
5000 = 4 GB
Mwezi
15,000 = 18 GB
30,000 = 38 GB
50,000 = 68 GB
75,000 = 110 GB
100,000 = 210 GB
Hapa bado umeniacha kidogo, wanakuuzia GB ama wanakuuzia SPEED?Device unanunua, wana MiFi za 50k na 150k. But wakati mimi naenda kununua nilienda na 50k kwa ajili ya device ila nikakuta device za 50k zimeisha so nikaacha kununua device, nikachukua tu laini now nimeweka hiyo laini kwenye simu.
Kuhusu kupunguza speed kwa uzoefu wangu sijakutana na hiyo hali. Na nafikiri kwa kuwa wanakuuzia data ambayo ni limited mfano 210GB, sidhani kama watakuwa wanahitaji kulimit speed. Tangu nimeenza kutumia naona iko sawa tu. Kwa mfano wa sasa nimetest speed ni 16mbps. Siyo kubwa ila kwa matumizi ya kawaida kustreem iko poa tu.
Unalipa laki nzima kwa gb 200!mkuu unapigwa hapoKifurushi cha chini ni cha wiki ambacho kwa elfu 5 unapata GB 4.
Ila vifurushi vizuri ni vile vya mwezi ambavyo bei yake ni kama ifuatavyo:
15K = 18 GB
30K = 38 GB
50K = 68 GB
75K = 110 GB
100K = 210 GB
Mi nilichukua cha laki moja na mambo yako poa tu maana sina matumizi makubwa na device ninazotumia ni PC na simu tu...
Siyo unlimited...Lakini mkuu hii siyo UNLIMITED...
Hii ni limited so wanakuuzia data...Hapa bado umeniacha kidogo, wanakuuzia GB ama wanakuuzia SPEED?
Itakuwa strong sana hioMie natumia 95k, 40MBS.
Yeah, pengine... Lakini nimeshatumia huduma za internet za makampuni mengine ambazo zilikuwa ni unlimited hali ilikuwa ni mbaya sana. Hao voda na 5G yao hata sitaki kuwasikia, huduma ya hovyo, walituuzia kifurushi cha speed 100mbps lakini speed tuliyokuwa tunapata ni chini ya 5mbps. So ukizingatia matumizi yangu kwa siku yapo chini ya GB 7 saba so GB 200 kwa mwezi zinanitosha. Kulipa laki kupata GB 200 na kulipa laki kupata unlimited kwangu haina tofauti. Labda siku matumizi yakiongezeka au nikiongeza device nyingi nitaweza kutafuta option ya unlimited...Unalipa laki nzima kwa gb 200!mkuu unapigwa hapo
Iko njema, shida tu haiendi umbali mrefu, haswa kama inazuiliwa na maukuta ukuta.Itakuwa strong sana hio
Kwa hoja hizi inaonekana utoto unakusumbua. Netlix ni nini?Yaani we unataka kusemaje, watu wasiuze routers kwa kuwa kuna kundi la watu masikini..!?
Halafu ambacho hukijui (au unakijua ila unajipa uchizi usiokuwa nao) pamoja na uwepo wa routers hizo bando za buku buku zenu bado zipo... router sio ya kila mtu, sasa wewe mtu huna kazi ya kukuhitajia mtandao, huna hata account ya netlix ili tuseme japo unahitaji router kwa ajili ya movies...router ya kazi gani.
Huu ndio ukweli haya ndiyo maisha ya watanzania wengi. Wengi wanaipambania leo, ndio umwambie aweke bando la 30kUnapata buku unaunga Sasa hivi. Baada ya muda labda jioni unapata buku unaunga Tena. Aliyeshiba haezi elewa....
Ndio maana mtu anamwambia mwezie nunua Michele uweke ndani, kwa mama ntilie unapoteza hela....Sasa ukiangalia huwezi pata cash ya kununua kilo 10 kwa mara Moja ila kila siku unaeza pata buku ya kula wali maharage kwa mama ntilie....... So........
Fuatilia mjadala ulipoanziakwahyo mkuu hoja yako hapo ni ipi watu wasinunue hzo route kisasa watanzania wengi hawana uwezo au wafanya biashara wasiziuze kwasababu umaskin mkubwa? Maana kama bando za buku zipo hakuna aliekatazwa kununua, na ambao wana uwezo wananunua hzo route kwasababu uwezo unawaruhusu we malalamiko yako upande upi ? Maan toka mwanzo wa uzi nakuona umeng'ng'ania 99% wananunua bando za buku
Hao Airtel hata wajitanue hadi wapasuke, katu siyo wa kuwaamini huduma zaoView attachment 3170731
N:B: Ni muhimu kupima Network kwenye eneo lako kabla ya maamuzi
Haya mambo ya kununua vifurushi vya buku buku unaweza kujikuta unaunga mara 3 na zaidi kwa siku, haba na haba hujaza kibaba mwisho wa mwezi umechoma 80k hadi laki kwenye bando
Suluhisho ni huduma ya unlimited internet, Hulipii Gb unalipia speed, Kuna huduma za waya kama Zuku fibre na Ttcl fibre unavutiwa waya nyumbani lakini tatizo lake huwezi kutembea nayo, ipo maeneo machache ya mjini na umeme ukikatika kifaa kinazima.
Makampuni ya Simu wakaleta unlimited internet unayoweza kuhama nayo lakini changamoto ilikuwa gharama , Mfano Vodacom na Tigo kifaa (router) cha bei ya chini ni 250,000, Kifurushi cha chini kabisa ni 120,000 kila mwezi, ni wachache sana wanaweza kumudu.
Airtel wameona fursa ya kulikamata soko kwa kudeal na gharama, kwa shilingi 110,000 unapewa router iliyoungwa bando la mwezi mzima na miezi ijayo unaweza kuunga kifurushi cha elf 70, hapa at least pana unafuu.
mitandano mingine wapunguze bei za vifurushi vya unlimited lasivyo watakuja kustuka Airtel kajitanua kawa Monopoly kameza soko
Ninawatumia toka mwaka jana October, na sijawahi kujutia huduma zao. Cha msingi tu eneo ulilopo liwe na mtandao mzuri wa Airtel.Hao Airtel hata wajitanue hadi wapasuke, katu siyo wa kuwaamini huduma zao
Nilishawahi kutumia Airtel na nikawahi kujuta. Ingawa Voda nao ni walewaleNinawatumia toka mwaka jana October, na sijawahi kujutia huduma zao. Cha msingi tu eneo ulilopo liwe na mtandao mzuri wa Airtel.
Stori za mitandaoni achana nazo, wewe nunua kifaa upate experience personally.
View attachment 3171456
View attachment 3171457
Imekaa njema sana kwa 110k unapata Router +70k bando.Airtel wameona fursa ya kulikamata soko kwa kudeal na gharama, kwa shilingi 110,000 unapewa router iliyoungwa bando la mwezi mzima na miezi ijayo unaweza kuunga kifurushi cha elf 70, hapa at least pana unafuu.