TAKUKURU isiishie kukamata viongozi wa vyama vya michezo na vilabu kwa ubadhirifu , sasa naomba waingie kuchunguza hizi tuhuma nzito zinazo tolewa dhidi ya chama changu pendwa cha ccm, haiwezekani tuka pakwa matope kiasi hiki kwamba chama kimeshiriki katika tendo hili ovu na chafu la kuwahonga ( kutoa rushwa ) kwa madiwani wa chadema ili wahamie ccm. Haiwezekani tukavumilia dhidi ya kashfa nzito kama hii na ikibainika kuwa kuna ukweli juu ya hili wahusika wachukuliwe hatua kali sana za kisheria ikiwa ni pamoja chama chetu kuwafukuza uanachama mara moja.