Aisee kumiliki gari kumbe gharama hivi? Nimetumia 505,000/= kufanya service!!

Hydraulic mim nanunua 115-120k..ya nissan
Kwa Nissan ni sahihi kabisa
 
Juzi fundi aliniuliza mara ya mwisho kufanya service gari langu. Nikamwambia mie tangu niagize nikaanza kutembea nayo sijawahi kufanya intensive service mpaka ipate tatizo ndio naileta kwako...
Hiyo sio service , hiyo ni maintenance repair kaka.

Halafu usiwasikilize mafundi kila kitu , mafuta ya ATF ( mnayoita hydraulic ) ya gearbox haibadilishwi kila mara, ni mpaka ibadilishe rangi yake iwe nyeusi nyeusi hivi baada ya kutembea kilomita 50,000+ ndo inabadilishwa kama miaka mitatu hivi..
 
Kitendo cha kuamka tuu na kuweka maji ya kawaida kwenye gar kimenisikitisha sana....kuna coolant maalum sio unaweka tu mimaj yako..we utakua unapigwa sana maana hujui gar

Extrovert sorry. Naomba unisaidie kukata huu ubishi hapa, nakuamini. Wewe ukisema kitu nakuelewa.

1. Huwa unatumia coolant au maji kwenye gari yako? Be honest.

2. Percentage ngapi ya wabongo wanatumia special coolant daily? Kadiria tu labda 90%, 70%, 45%
 
Unataka kuwa "A jack of all trades.........."
 

Wengi wenye uwelewa na magari wanatumia coolant
 
Mi natumia maji coz hata gari za mshua home toka niko dogo nilikuwa natia maji na kucheki fluids zingine. Coolant ni mbadala wake tu na iko un-neccessarily expensive unless ununue feki ilichanganywa maji na rangi tu 😂😂😂

Maji yana disadvantages zake ikiwemo kuweka rust kwenye radiator na horse pipes ambazo ni 100% chuma na pia maji yana evaporating effect. Hivyo kila baada ya muda yatakulazimu kuongeza ingawa system yako ya cooling ikiwa freshi hayapungui haraka.

Coolant evaporating effect iko chini kwa sababu yenyewe haichemki kirahisi kama maji hivyo iko efficient na hudumu muda mrefu ukiitumia purely bila kumix na mimaji. Kubwa zaidi ni anti-rust na hio ndio faida yake ingine.

Kwahio kutumia maji sio dhambi wala kosa maana miaka yote ya 1980's-2006 watu gari walikuwa wanazitia maji tu. Wala sio kitu cha ajabu to date maybe 25% ya wamiliki gari TZ ndio wanatia coolant.
 

Asante bro.

Endapo nimekua nikitumia maji kwa muda mrefu kidogo. Then nikataka sasa niwe natumia coolant yenyewe, ni inawezekana. Ama ishakua too late. Itabidi nipeleke kwa fundi anisafishie radiator aondoe kutu na maji yote?

Sorry kama unafaham pia, average bei ya coolant inacheza kwenye ngapi (babywoka za Toyota).
 
Hata mimi nimeshangaa sana labda hana shuguli nyingine za kufanya au ametia chumvi masaa 3 ni mwendo wa Dar Moro
Yani uzunguke masaa matatu ili uokoe elfukumi au 20?

Unaokoa 50 masaa 3 kazini kwako unapigwa laki 2 au zaidi.

Kujua sanaaa kuna leta uboya pia
 
Coolant haina shida mkuu, unatumia hata leo ukitaka hela yako tu.

Kuna litre 1 ile substandard wanauza 10K ila ya kueleweka ni kuanzia 20K na kuendelea.
 
Sasahv unavyoliendesh after service unalionaje.?
 

Gawana ridhiki na wenzio jamani
 
Hahaha..kijana hiv unajua why unashauriwa kutumia coolant na sio mimaj yako hyo ya kawaida..kwanza tambua maj meng ya kawaida yana chumvi.hard water so ukiwa unatumia mara kwa mara.ukungu ule wa hard water siunaujua..

Pia nahis coolant haisupport kihivyo rusting.kutu.so ukiweka mimaj ya kawaida nahis unakaribisha mazingira hayo(sina uhakika hapa)

Mkuu kama ulizoea weka mimaj ya kawaida acha
 
Sasahv unavyoliendesh after service unalionaje.?

Liko vizuri. Jepesi, linachanganya haraka. Brake ziko very sensitive. Lina nguvu. Mlimani napanda kama nashuka.
 
Juzi fundi aliniuliza mara ya mwisho kufanya service gari langu. Nikamwambia mie tangu niagize nikaanza kutembea nayo sijawahi kufanya intensive service mpaka ipate tatizo ndio naileta kwako....
Kupigwa kuko pale pale na umepigwa tu, mafundi na wazuza spair ni kitu kimoja, hizo bei tayari kuna cha juu cha fundi hapo. Ndo maana unaona mara nyingi bei za ufundi zinakuwa chini ili kukuvuta siku nyingine uende, lakini kwenye spair ndo anapata faida.
 
Mi natumia maji coz hata gari za mshua home toka niko dogo nilikuwa natia maji na kucheki fluids zingine. Coolant ni mbadala wake tu na iko un-neccessarily expensive unless ununue feki ilichanganywa maji na rangi tu...
Faida za coolant vs maji ya kisima/bomba/mtoni/ziwani

1.coolant ina dawa zinazozuia radiator isipate kutu
2.Coolant ina dawa zinazosaidia coolant isigande na kuwa barafu hata kama ni kwenye zile nchi za bari kali....maji huganda..

3.Coolant inapoa haraka sana kuliko maji, hivyo coolant inakuhakikishia upoozaji mzuri wa engine yako.

4.Coolant hai'evaporate haraka kama maji ya kawaida.

5.Kwa wale wanaotumia magari ya CVT, coolant itapooza gearbox yako vizuri ukilinganisha na maji ya bomba.

6.coolant italinda mfuniko wako wa radiator, ila maji yatauharibu kwa kutu..

NB....magari mengi ya siku hizi. tumia maji kama dharura tu endapo huna hela ya coolant kwa wakati huo, ukipata hela weka coolant kwa maisha marefu ya Head yako, Radiator yako na CVT transmission.

Thanks guys.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…