Aisee, kumiliki gari raha sana. Leo nimewapa lift watu 6 kwenye babywoka yangu!

Recently nimenunua gari ndogo (babywoka).
Sisemi gari gani lakin ni mojawapo kati ya haya matano (IST, VITZ, Passo, Honda Fit, Suzuki Swift)

Leo asubuhi sana kuna issue nilikua nawahi pale UDSM. Nilikua natokea Ubungo mataa, wakati nakunja pale kona ya njia panda ya Chuo (kuna kituo cha daladala na babaji nyingi wanapaki pale). Nikaona watu wengi wanapiga mkono kuomba msaada wa lift. Wengi wao walikua kinamama wanaofanya usafi na upishi katika cafeteria mbalimbali za UDSM.

Kutokana na kuwa wanafunzi wameanza likizo ndefu, daladala zinapita kwa kuotea sana pale. Kuna ile tunasema "I wish" kila mtu anakua nazo.
Mimi siku zote nimekua najisemea, "siku nikimiliki gari, nitakua nawapa lift kina mama, watoto wanafunzi wadogo wa primary na wazee hasa during rush hours au pakiwa na tabu ya usafiri". Basi mtu mzima nikaachia mafuta, nikawasha indicator ya kushoto, nikabonyeza breki pssssssssss... Nikasimama. Nikawaambia "pandeni niwasogeze".

Aiseee huwezi amini, kwenye kibebi woka changu waliingia wamama watano na askari wa usalama barabarani mmoja. Wamama wanne na yule askari walikaa nyuma. Halafu mama mmoja bonge kuliko wote alikaa mbele. Jumla watu sita, na mimi dereva tukawa saba. Aisee nilitamani nigeuke nyuma nione wale wamama wanne na yule askari walivokaa mpaka wakaenea kule nyuma [emoji23] [emoji23] [emoji23] .

Nikawasha indicator ya kulia (kuingia barabarani tena), nikakanyaga mafuta. Hapo nikawa nafikiria maneno ya Extrovert, joshua_ok na mng'ato wanasemaga eti "hizi babywoka hazina nguvu mlimani, tena ukiwa umepakiza watu wazima zikifika mlimani zinazima, au kutetemeka sijui nini bla bla". Nikasema leo ngoja nipime ukweli wa argument hiyo.

Kutoka pale njia panda kwenda utawala kuna kamlima kamechangamka halafu kana kona kona. Naonaga bajaji zikianza kupanda ule mlima zinaenda kama zinasindikiza bibi harusi. Lakin mie nikapanda huku nakanyaga kidogo kidogo gari inaenda vizuri tu. Hakuna cha gari kutetemeka, kuzimika wala kuishiwa nguvu. Nikafika pale Utawala yule askari akashuka akasema "asante kamanda". Wale wamama watano nikawaacha pale CONAS walivoshuka wakasema "asante sana baba, uwe unapita kila siku" wenzake wakacheka "heheheeee".

Nimejisikia faraja sana kuwapa watu msaada wa lift, hasa mida ile ya asubuhi "rush hours". Hatimae ndoto yangu imetimia kwa 50%. Magari mengi yalikua yanapita pale (tena ni wafanyakazi wa UDSM), kina mama wanapunga mkono kuomba lift hakuna anayesimama. Nasubiri shule zifunguliwe siku moja nipite kituoni niwabebe wanafunzi wa primary hata wawili tu niwasogeze hapo nitakua nimekamilisha "I wish" yangu kwa 100%.

Halafu kitu kingine nimegundua ukiwa unaendesha gari unapata heshima fulani hivi kutoka kwa watu barabarani. Bila kujali gari ni lako ama umeazima, bila kujali unaishi wapi au mfukoni una shingapi.

View attachment 1566413
You are gentleman.
 
Tahadhari:sio kila unaempa lifti ni mtu mzuri,na usifikiri kuwa wengine hawatoi lifti kwakuwa tu wana roho mbaya,ni kwa sababu za kiusalama.Umeshawahi kutafakari kuwa umemuona ni mwanafunzi au ni binti mzuri una mpa lift halafu ghafla akiwa ndani anageuka kuwa jini?huo ni mfano tu iko mingi wengine wanaweza kuongezea...
Samahani mkuu, jini akikutaka hana njia nyingine ya kukupata isipokua njia ya lifti?

Basi ndugu wanaJF, tusitoe lifti ili tuepuke majini!
 
Sipiti tena, nilikuja mara moja tu. Halafu kayimukaa amenitisha hapo juu aliposema alifungwa jela kisa kutoa lift.
Sitoi tena lift hadi kufa kwangu
Amna toa ila kiuangalifu Sana na wanaposhuka unawakagua kwa macho hawajabeba kitu, wengine kwenye gari wanaanza Kula karanga au bigjii Kisha wanabandika kwenye kiti Cha gari, wengine kuchana sitina mengineyo mengi
 
Daaah... Kumbe mtata stephot amesema kweli, ngoja niwe makini.
Sitoi tena lift kuanzia leo
Hivi nimekusifu kumbe unajaribika kirahisi hivi?..tahadhari ni jambo la kawaida kwenye kila jambo..sio lift tuu...hatari zipo popote uwe na gari au huna...na unaweza kupatwa na janga lolote..popote...wakati wowote uwe na gari au huna..kila mazingira yana tahadhari zake...usiache kutenda wema kwa kuhofia eti nisijepatwa na hili au lile..unaweza ukakwepa kutoa lift ukapata ajali mbaya iliyosababishwa na dereva au mtumiaji mwingine wa barabara..kila jambo lina faida na lisk zake..suala muhimu ni kiasi na tahadhari tuu.
 
Tahadhari:sio kila unaempa lifti ni mtu mzuri,na usifikiri kuwa wengine hawatoi lifti kwakuwa tu wana roho mbaya,ni kwa sababu za kiusalama.Umeshawahi kutafakari kuwa umemuona ni mwanafunzi au ni binti mzuri una mpa lift halafu ghafla akiwa ndani anageuka kuwa jini?huo ni mfano tu iko mingi wengine wanaweza kuongezea...
Mmh huo mfano wa jini ni hekaya tu
 
Recently nimenunua gari ndogo (babywoka).
Sisemi gari gani lakin ni mojawapo kati ya haya matano (IST, VITZ, Passo, Honda Fit, Suzuki Swift)

Leo asubuhi sana kuna issue nilikua nawahi pale UDSM. Nilikua natokea Ubungo mataa, wakati nakunja pale kona ya njia panda ya Chuo (kuna kituo cha daladala na babaji nyingi wanapaki pale). Nikaona watu wengi wanapiga mkono kuomba msaada wa lift. Wengi wao walikua kinamama wanaofanya usafi na upishi katika cafeteria mbalimbali za UDSM.

Kutokana na kuwa wanafunzi wameanza likizo ndefu, daladala zinapita kwa kuotea sana pale. Kuna ile tunasema "I wish" kila mtu anakua nazo.
Mimi siku zote nimekua najisemea, "siku nikimiliki gari, nitakua nawapa lift kina mama, watoto wanafunzi wadogo wa primary na wazee hasa during rush hours au pakiwa na tabu ya usafiri". Basi mtu mzima nikaachia mafuta, nikawasha indicator ya kushoto, nikabonyeza breki pssssssssss... Nikasimama. Nikawaambia "pandeni niwasogeze".

Aiseee huwezi amini, kwenye kibebi woka changu waliingia wamama watano na askari wa usalama barabarani mmoja. Wamama wanne na yule askari walikaa nyuma. Halafu mama mmoja bonge kuliko wote alikaa mbele. Jumla watu sita, na mimi dereva tukawa saba. Aisee nilitamani nigeuke nyuma nione wale wamama wanne na yule askari walivokaa mpaka wakaenea kule nyuma [emoji23] [emoji23] [emoji23] .

Nikawasha indicator ya kulia (kuingia barabarani tena), nikakanyaga mafuta. Hapo nikawa nafikiria maneno ya Extrovert, joshua_ok na mng'ato wanasemaga eti "hizi babywoka hazina nguvu mlimani, tena ukiwa umepakiza watu wazima zikifika mlimani zinazima, au kutetemeka sijui nini bla bla". Nikasema leo ngoja nipime ukweli wa argument hiyo.

Kutoka pale njia panda kwenda utawala kuna kamlima kamechangamka halafu kana kona kona. Naonaga bajaji zikianza kupanda ule mlima zinaenda kama zinasindikiza bibi harusi. Lakin mie nikapanda huku nakanyaga kidogo kidogo gari inaenda vizuri tu. Hakuna cha gari kutetemeka, kuzimika wala kuishiwa nguvu. Nikafika pale Utawala yule askari akashuka akasema "asante kamanda". Wale wamama watano nikawaacha pale CONAS walivoshuka wakasema "asante sana baba, uwe unapita kila siku" wenzake wakacheka "heheheeee".

Nimejisikia faraja sana kuwapa watu msaada wa lift, hasa mida ile ya asubuhi "rush hours". Hatimae ndoto yangu imetimia kwa 50%. Magari mengi yalikua yanapita pale (tena ni wafanyakazi wa UDSM), kina mama wanapunga mkono kuomba lift hakuna anayesimama. Nasubiri shule zifunguliwe siku moja nipite kituoni niwabebe wanafunzi wa primary hata wawili tu niwasogeze hapo nitakua nimekamilisha "I wish" yangu kwa 100%.

Halafu kitu kingine nimegundua ukiwa unaendesha gari unapata heshima fulani hivi kutoka kwa watu barabarani. Bila kujali gari ni lako ama umeazima, bila kujali unaishi wapi au mfukoni una shingapi.

View attachment 1566413
Ila kutoka pale njia panda mpaka CONAS au Utawala ni karibu mbona?

Dk 10 kutembea.

Wangejiongeza.
 
Niliwai kupakiza watu wanne kwenye gari, baadae nafika home naona siti imechorwa chorwa na wamechukua triangle na matunda niliyoyanunua. Siku nyingine nimepakiza wanafunzi njian mmoja kapandisha shetani Kisha kafungua mlango na kujitupa nnje na kuumia mikono na miguu, niliwekwa ndani siku 2 maana wananchi walijua niliwateka na wazazi hawakuelewa kabisa mwisho baada ya kutoka ugomvi ukahamia kwa mke maana alijua yule dentist wa fom four Ni mchepuko. Tangu siku hiyo kupakia mtu Kwa gari labda niwe namjua au mtu mzima/mzee na matrafiki, wengine wanisamehe bure
Msaada unambatana na magumu yake.

Kuna siku niwainea watu huruma muda wa saa4 usiku wamesimama kituoni bila usafiri na hawana uhakika wa kupata usafiri.

Niliamua kuwachukua hadi town japo mimi tayari nilikuwa nimefika maeneo yangu.
Bahati mbaya gari lilikuwa halina maji kwani dereva aliyekuwa anaendesha mchana alikuwa mdogo wangu na hakukagua gari asubuhi.

Nilipoanza kupandisha mlima gari ikazima ghafla, kumbe nimekaanga injini.
Abiria wote 8 walishuka na kuniacha kimya kimya isipokuwa jamaa mmoja alisalia kunisaidia kusukuma niliweke pembeni.

Hii ilinivunja moyo sana kwani niliwabeba bure
 
Ila kutoka pale njia panda mpaka CONAS au Utawala ni karibu mbona?

Dk 10 kutembea.

Wangejiongeza.

Ni kweli bro. Sema nini... Mie naona watu wengi tumelemazwa na nature ya maisha ya mjini sijui.
Yaani mfano kutoka mlimani city mpaka mpakani kabla hujafika mwenge mataa mtu anapanda daladala.
 
Hao wanadeka wameshindwa kutembea ubungo maji mpka chuo, mbona shortcut ya coet ni karibu sana??

Mi nawapaga lift wanafunzi wanaokaa msewe tu, mwisho unajikuta unakula kimasihara [emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom