Aisee! Mkeo anatosha. Anaweza kukupa kila kitu kuliko mchepuko yeyote

Aisee! Mkeo anatosha. Anaweza kukupa kila kitu kuliko mchepuko yeyote

Able man

Senior Member
Joined
Nov 22, 2020
Posts
132
Reaction score
174
Nilichogundua wanaume wengi tunadanganyika saana kuliko uhalisia. Kuna watu hatuthamini wake zetu,tunathamini michepuko zaidi.

Kuna watu tunawatendea Kwa ukatili wake zetu saana na kuwalea michepuko kama mayai!

Kuna watu tunawafanya wake zetu kuona maisha hayana maana kiasi cha kuona ndoa ni janga kuubwa hivi lisilo na matumaini wala mwisho wake haujulikani itakuaje!

Lakini unajua mkeo huyo uliye naye na unayemchukulia poa, kama utamthamini,utamheshimu,utamtunza na kumpa hadhi anayoistajili na akawa na Amani ya kutosha na wewe,atakufanya upate Raha ya maisha kuliko unavyodhani ama ulivyowahi kujua!

Unajua anaweza kukuridhisha kuliko mchepuko Yeyote unayemthamini leo kuliko mkeo!

Mchepuko yupo kwa ajili yake (anakutumia wewe kwa maslahi yake),mkeo ypo Kwa ajili yako na yeye! (Na wengine wanakuthamini kuliko wao wenyewe...)

Lakini zingatia unatakiwa kumthamini,kumheshimu,kumtunza na kumpa hadhi anayoistajili ndipo atakuwa na Amani ya kutosha na wewe kisha utafaidi mema ya nchi!😀😀

Angalizo: Nimezungumzia mke mwenye nia njema nawe, anakupenda na aliyeridhika nawewe ila wewe unamkomoa! Kwa mwanamke aliyekuja Kwa lengo la kuchuma kwako hahusiki hapa!
 
Amen mkuu kama ukisemacho ndicho Mungu azidi kukuongezea na uipate furaha itokananyo na kumjalii na kutumza mkeo,hakuna kitu kizuri kama familia nzuri hapa duniani

The feeling of being wanted,desired loved and cared for,nothing can beat that

Tuzithamini familia zetu wapendwa,tuwathamini wake zetu
 
Umenena mkuu!
 
umeweza kuacha dhambi
Hakuna mwandamu ambaye hatendi dhambi Kwa nguvu zake! Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Kwa nia ya dhati,Kwa mazoezi ya kila siku ya kuhitaji nguvu ya Mungu mtu anakuwa mshindi. Na hayo ndio nimeita mazoezi...!
 
Hata mimi ninashangaa kwa nini mtu anamwacha mkewe harafu anakuchukuliwa na mianamike mingine wakati wote wana nyuchi zile zile! Jamani nyama ni ile ile ila bucha ndizo tofauti.
Na usikute nyama unayokula ni tamu kuliko unayokwenda kusakanya huko uchochoroni...🤔🤔
 
Dah....Dalili ya kwanza kabisa ya mwanaume anayeanza kuzeeka siyo kutumia vidonge ya kisukari na BP...bali ni kuanza kumpenda sana mke wake 🤣 🤣🤭
 
Hao mchepuko nao ni watu wa watu maisha ni kusaidiana
 
Dah....Dalili ya kwanza kabisa ya mwanaume anayeanza kuzeeka siyo kutumia vidonge ya kisukari na BP...bali ni kuanza kumpenda sana mke wake 🤣 🤣🤭
Duh...! Umekariri vibaya...
 
Back
Top Bottom