Aisee! Mkeo anatosha. Anaweza kukupa kila kitu kuliko mchepuko yeyote

Aisee! Mkeo anatosha. Anaweza kukupa kila kitu kuliko mchepuko yeyote

Upo sawa kabisa, kuna mbaba kuchepuka mpaka kazalisha huko nakumtambulisha kwa mkewe kama mke mwenza sasa dada kalipokea kwa machozi kweli aliponyamaza jamani naye uwii kapata mchepuko halafu wamaana kumzidi mmewe daa naye kamwaga mboga na ugali Mme anakenua tu kumbe naye analiwa, visasi huwa vikali usiombe
Duh...!
 
Yani nimekuelewa kwa mbaliii yani naona inakuja, inakataa
Nilichogundua wanaume wengi tunadanganyika saana kuliko uhalisia. Kuna watu hatuthamini wake zetu,tunathamini michepuko zaidi.

Kuna watu tunawatendea Kwa ukatili wake zetu saana na kuwalea michepuko kama mayai!

Kuna watu tunawafanya wake zetu kuona maisha hayana maana kiasi cha kuona ndoa ni janga kuubwa hivi lisilo na matumaini wala mwisho wake haujulikani itakuaje!

Lakini unajua mkeo huyo uliye naye na unayemchukulia poa, kama utamthamini,utamheshimu,utamtunza na kumpa hadhi anayoistajili na akawa na Amani ya kutosha na wewe,atakufanya upate Raha ya maisha kuliko unavyodhani ama ulivyowahi kujua!

Unajua anaweza kukuridhisha kuliko mchepuko Yeyote unayemthamini leo kuliko mkeo!

Mchepuko yupo kwa ajili yake (anakutumia wewe kwa maslahi yake),mkeo ypo Kwa ajili yako na yeye! (Na wengine wanakuthamini kuliko wao wenyewe...)

Lakini zingatia unatakiwa kumthamini,kumheshimu,kumtunza na kumpa hadhi anayoistajili ndipo atakuwa na Amani ya kutosha na wewe kisha utafaidi mema ya nchi![emoji3][emoji3]

Angalizo: Nimezungumzia mke mwenye nia njema nawe, anakupenda na aliyeridhika nawewe ila wewe unamkomoa! Kwa mwanamke aliyekuja Kwa lengo la kuchuma kwako hahusiki hapa!
 
Back
Top Bottom