Aiseee!!!! Dar kuna matapeli

Mi washawahi kunifata wa hivi hivi eti una matatizo umerogwa leo sikj isingeisha ungekufa akanipa karatasi nitafune ile kutema ikatoka nywele ila mi hapo nikashtuka kwa kuwa wiki moja nyuma rafiki angu aliibiwa kwa staili hiyo hiyo so sababu alinihadithia nikajua ni wale wale nikamkataa
 
Utapewaje kitu na mtu usiyemjua akuambie tafuna na wewe utafune?
 
Pole usijilaumu sana

Baki na funzo wafundishe na wengine

Ilikuwa ni siku yako ya kuibiwa tu
 
Siku nyingine watakubamiza vikubwa zaidi ulivyonavyo hapo ndio utakua umejipata
 
Karibu Daslamu Mkuu.
 
Tecno Spark4, ok
 
Mimi Kwa maneno kutapeliwa hapana labda niangushe uokote au uniibie Kwa kunikaba tena waje kuanzia 4+
 
Mkuu hayajakukuta we aya tu.
Mkuu mimi siyo kinda. Na kwenye maisha na mishe nimeshakutana na matapeli wengi sana. Kuanzia wale walikuwa wanaitwa wafunga kanyaboya, wanywesha watu madawa ya kulala kwa kutumia chambo cha demu mzuri etc... Na wote hao wameshindwa. Only kwa sababu mimi sina tamaa na nikiona mtu anataka kunizoea bila mpango namkwepa. Trust me, tapeli bila wewe kuwa na tamaa ya kutaka shortcut hakutapeli. Na pia kuwa na imani za kishirikina nako kunasababisha utapeliwe. Mimi aliyeweza kuchukuwa kitu kwangu ni mdokozi (siyo tapeli) mmoja mwanamke. Alikuwa na ''mimba'' kubwa akaja sehemu jamaa aliniomba nimsaidie kuuza nguo za watoto, akawa ananiambia ''hebu lete ilee'', nikigeuka, anachukua vinguo vilivyokuwa mezani, anatumbukiza kwenye lile tumbo la ''mimba''. Kumbe hakuwa na mimba bali alikuwa ameweka uwazi kwa ndani wa kutumbukiza vitu na kwa juu kuna ki-mlango chenye zipu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…