Aiseee!!!! Dar kuna matapeli

Aiseee!!!! Dar kuna matapeli

Nimewahi mkuu ila kitambo kidocho🤣🤣🤣.
Nilitaja mpaka namba za siri za airtelmoney 🤣🤣.
😂😂😂Nimecheka Aisee, sasa unaona hapo uliyemwambia kaibiwa kiboya tulinganishe au tuishie hapo any way pole mkuu
 
Mkuu mimi siyo kinda. Na kwenye maisha na mishe nimeshakutana na matapeli wengi sana. Kuanzia wale walikuwa wanaitwa wafunga kanyaboya, wanywesha watu madawa ya kulala kwa kutumia chambo cha demu mzuri etc... Na wote hao wameshindwa. Only kwa sababu mimi sina tamaa na nikiona mtu anataka kunizoea bila mpango namkwepa. Trust me, tapeli bila wewe kuwa na tamaa ya kutaka shortcut hakutapeli. Na pia kuwa na imani za kishirikina nako kunasababisha utapeliwe. Mimi aliyeweza kuchukuwa kitu kwangu ni mdokozi (siyo tapeli) mmoja mwanamke. Alikuwa na ''mimba'' kubwa akaja sehemu jamaa aliniomba nimsaidie kuuza nguo za watoto, akawa ananiambia ''hebu lete ilee'', nikigeuka, anachukua vinguo vilivyokuwa mezani, anatumbukiza kwenye lile tumbo la ''mimba''. Kumbe hakuwa na mimba bali alikuwa ameweka uwazi kwa ndani wa kutumbukiza vitu na kwa juu kuna ki-mlango chenye zipu.
Na mimi niliibiwa kwa staili hiyo.
Kipindi natoka home natembea kwenda shule ya Yemeni kwenye mahafari nilikua natembea kwa miguu.
Alitokea jamaa akanisimamisha akaonesha ID feki ya polisi sikuzingatia nikawa namsikiliza kipindi namsikiliza kuna mwengine alitokea nyuma akachomoa simu na wallet.
Na akati naongea nae ili kumjibu tu haraka niondoke pasi na kujua kama nimefokolewa simu nikamtajia na neno siri akaondoka.
Nafika mbele nicheki saa ngapi simu sina na wallet sina.
Ila mimi haikuwa kama jamaa kuamini kurogwa.
Mie nilikutana na FAKE POLICE.
 
Hizi simulizi za kuibiwa,kutapeliwa kuna uzi wake humu utafuteni mvunjike mbavu.
 
Hapo nimemaliza fomu 4. Nimekuja Dar kusoma pre form 5 nakatamani nirudi na simu ya GPS kijijini. Yule muhuni ili kunivuruga akili akanionyesha picha za X akanambia mwanangu utaenjoy sana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Siku moja nipo kwenye mizunguko yangu ya hapa na pale maeneo ya Ubungo nikakutana na jamaa mmoja baada ya kuzungumza nae kwa muda akaniambia nimelogwa na kuanza kuniambia mambo ya nyumbani kwetu, akaniambia kama huamini tafuna hili karatasi nikatafuna nikatema nywele Daah si nikaanza kumuamini aisee

Akaniambia nimkabidhi pesa zangu nilikuwa na Sh elfu 30 na simu akaniambia chukua hii dawa nenda mpaka pale kituo cha mwendokasi usigeuke nyuma wala kuongea na MTU ukifika itupe pale.

Ile nafika kituo cha mwendokasi akili inarudi kwamba huyu jamaa nimemuamini VP kumuachia simu yangu na pesa, nikageuka nyuma kumcheki simuoni nikaamua kurudi pale kilichofuata ni majonzi na kilio nimetapeliwa

Sitaisahau simu yangu ya Tecno spark 4 asee, niliumia sana siku hiyo
Yaani mpaka kipindi hiki cha mwendokasi bado mnatapeliwa kwa style hii??😆😆,
 
Hizo nywele huwa zinatoka wapi? Kuna binti nae alishatapeliwa hivi alitafuna karatasi akatema nywele
Hivi na wwe kweli mtu anakusimamisha barabarani hamjuwani,eti anakwambia tafuna hii karatasi na wwe unatafuna, siku ingine mtatafuna sumu mfe huku mnajiona live!!
 
Pole sana, ndio kujifunza huko mkuu.

Na ukitapeliwa hamna ataesema umetapeliwa kijanja, sote tutakwambia umetapeliwa kijinga.

Mimi nilitapeliwa 25k ila sio kesi nilijifunza kutofatilia na kujisogeza kwenye mikusanyiko isiyo na maana.
 
Wengi wanao tapeliwa chanzo ni tamaa zao wameshindwa kuzii control!!
 
Siku moja nipo kwenye mizunguko yangu ya hapa na pale maeneo ya Ubungo nikakutana na jamaa mmoja baada ya kuzungumza nae kwa muda akaniambia nimelogwa na kuanza kuniambia mambo ya nyumbani kwetu, akaniambia kama huamini tafuna hili karatasi nikatafuna nikatema nywele Daah si nikaanza kumuamini aisee

Akaniambia nimkabidhi pesa zangu nilikuwa na Sh elfu 30 na simu akaniambia chukua hii dawa nenda mpaka pale kituo cha mwendokasi usigeuke nyuma wala kuongea na MTU ukifika itupe pale.

Ile nafika kituo cha mwendokasi akili inarudi kwamba huyu jamaa nimemuamini VP kumuachia simu yangu na pesa, nikageuka nyuma kumcheki simuoni nikaamua kurudi pale kilichofuata ni majonzi na kilio nimetapeliwa

Sitaisahau simu yangu ya Tecno spark 4 asee, niliumia sana siku hiyo
wee ni boya aisee sasa ujinga kama huu unaandika humu
 
Hili lilinitokea mbagala kule sijui kunaitwa majimatitu!
The same kwangu pia nilitafuna karatasi, kutema hivi natema nywele.
Aise jamaa kanipanga pale mambo kibao nikawa namsikiliza tu.
Mwishoni kasema nimpe kibegi changu (kibegi kilikuwa na hela maana wakati huo nilikuwa nafanya biashara) akasema nimpe na simu yangu halafu anasema eti niende nyumbani kuna kitu nitakikuta uvunguni mwa kitanda.
Sasa geto kwangu sikuwa na kitanda kulikuwa na godoro tu, nikapata mashaka kumhusu jamaa na nilikuwa nimeshaanza kutaka kumpa kibegi changu.
Ilikuwa mbele za watu nikaanza kuongea kwa sauti kubwa kwamba wewe ni tapeli unataka uniibie,
Cha ajabu watu waliokuwa pale wakaanza kucheka tu wanasema dogo kidogo uingizwe mjini, hiyo hela yako kunywa soda maana umeponea chupuchupu.

Nikawaona hawa jamaa nao ni wasenge, naibiwa hapa halafu wananiangalia tu.
 
Back
Top Bottom