KUTEKWA,KUTESWA NA KUTUPWA KWA BI AISHA MACHANO WA BAWACHA...!
Baada ya tukio la kutekwa,kuteswa na kuuawa na kisha Kutupwa kwa Ali Kibao mjumbe wa secretarieti ya CHADEMA Taifa
Bi Aisha Machano binti wa Kiislamu alitekwa Jana Wilayani Kibiti na Wanaume Saba,wakiwa na mwanamke mmoja.
Bi Aisha Machano akiwa stendi ya daladala Kibiti alifuatwa na watu waliojitambulisha kwake kuwa ni askari wa jeshi la Polisi,na alipo waomba waonyeshe Vitambulisho walimgomea na Kumkamata kwa nguvu.
wakiwa ni wanaume saba na mwanamke mmoja walimkamata na kumfunga pingu mikononi
Kisha wakamuingiza katika gari aina ya Landcruiser hard top nyeupe na kuelekea naye mapori ya Kisarawe. Kuanzia Jana Saa Saba mchana wakakaa nae hadi Saa Saba usiku walipo muacha akiwa hoi porini wakidhani wamesha muua.
Bi Aisha Machano ambaye ni Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) amepigwa na kuteswa sanaaa,muda wote wa mateso,watekaji walitaka amtaje kiongozi ambaye aliwatuma BAWACHA kuchoma Vitenge walivyopewa na Rais @SuluhuSamia ktk siku ya wanawake Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 March 2023.
Aisha Machano alimchaniwa nguo zake zote (HIJAB ) akabakia uchi wa mnyama,anapigwa marungu na waya mwilini akiwa na pingu mkononi ,Wakati wote anarekodiwa video na picha na mwanamke mmoja ambaye alikuwa anasimamia zoezi la uteswaji wake.
Wamempora simu yake ya mkononi na Kumtishia akienda Kuongea popote watasambaza picha zake za uchi.
Baada ya Kuachwa porini usiku ule wa Saa Saba ,watekaji wakifikiri wameshamuua tayari.
Bi Aisha Machano baada ya kuhisi pana utulivu na hali ya ukimya alifungua macho na kukuta tayari watekaji wameondoka,
kisha akajikongoja taratibu kutoka porini hadi barabara ya vumbi alipokutana na Vijana wa bodaboda huku akiwa na damu mwili mzima akiwa katika hali ya utupu kama alivyozaliwa.
Bodaboda walimsaidia kumsogeza barabarani na kujistiri na Kumsaidia mawasiliano na viongozi wenzie walio hakikisha anakimbizwa hospitali haraka sana.
Kwa sasa Aisha Machano yupo katika Chumba cha matibabu ya dharula (emergency) jina la hospitali tuna ficha kwa sasa,Madaktari wanajaribu kuokoa uhai wake.