Pre GE2025 Aisha Machano, Katibu mwenezi BAWACHA Taifa, alitekwa na kupigwa sana, ameokotwa porini akiwa na hali mbaya

Pre GE2025 Aisha Machano, Katibu mwenezi BAWACHA Taifa, alitekwa na kupigwa sana, ameokotwa porini akiwa na hali mbaya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
huenda wenye kuhitaji vile vitenge vilivyochomwa walipata hasira sana kwamba why this,

ingawa kuchoma vitenge sio jambo la kiungwana lakini pia kumpiga mtu kwa hasira sio jambo zuri pia 🐒
Kwendeni zenu, ingekuwa hasira si wangempiga hadharani? Kwanini atekwe kwa kuviziwa, apigwe na kuteswa bila kionekana then atupwe porini?! Haya mambo hayakubaliki kwa lugha yoyote ile
 
CCM wana mambo ya kitoto sana. Kwa nini sasa wanajikuta wamevurugwa wakisikia tu picha au vitenge vya mwenyekiti wao vimechomwa moto!!
Leo ukichoma moto kitenge, kwa nini tusidhani kesho utachoma kitanda na kumuua kabisa?

Kitenge kimekosea nini? Hivi mtu anasafishaje nyumba kwa kutumia uchafu?

Kama huoni kwamba hilo ni tatizo, basi kuna tatizo kubwa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Katibu Mwenezi Bawacha Taifa Mhe. Aisha Machano akiwa Kibiti kuendelea na majumu ya Chama ametekwa na kupigwa sana kisha kutupwa porini.

Vijana wa bodaboda wamemuokota akiwa katika Hali mbaya na maumivu makali. Waliomteka walitaka maelezo ni nani aliwaelekeza kuchoma vitenge vilivyogawiwa na Rais
SuluhuSamia katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2023 mkoani Kilimanjaro.

Kwa sasa amefikishwa hospitali kwa ajili ya matibabu na ameingizwa chumba maalum cha upasuaji (Theatre) kwa huduma zaidi.Taarifa za kina zitakuja hapo baadaye kadiri ya tutakavyozipokea.


Pia soma:
Kama ni kweli wavichome Nchi nzima ili waendelee kuwateka maana ndio sababu watekaji na wauaji hawakamatwi wanatumwa kuitishia watu wasiongelee ufisadi uliopo Nchini.
 
Sasa mtu amewaletea suluhu ya kisiasa na uhuru wa kujieleza mkamchomea vitenge vyake 😂😂😂

Si walimshangilia sana kwamba hatawatesab😂😂 anyway tuendelee kutazama huu mchuano
Huko Lumumba mtakuwa mnalishwa ujinga sana.
 
 
Hizi Taarifa za kupeana online ukiwa unazifata kichwa mchungaa unaweza kujikuta unaitendea makosa makubwa sana nafsi yako,Naomba iwekwe walau picha akiwa ameokotwa polini au ya hospitali ili wakati tunacomment na na kulaaani vikali vitendo hivi tuwe tunaitendea haki afya yetu ya akili.
 
KUTEKWA,KUTESWA NA KUTUPWA KWA BI AISHA MACHANO WA BAWACHA...!

Baada ya tukio la kutekwa,kuteswa na kuuawa na kisha Kutupwa kwa Ali Kibao mjumbe wa secretarieti ya CHADEMA Taifa

Bi Aisha Machano binti wa Kiislamu alitekwa Jana Wilayani Kibiti na Wanaume Saba,wakiwa na mwanamke mmoja.

Bi Aisha Machano akiwa stendi ya daladala Kibiti alifuatwa na watu waliojitambulisha kwake kuwa ni askari wa jeshi la Polisi,na alipo waomba waonyeshe Vitambulisho walimgomea na Kumkamata kwa nguvu.

wakiwa ni wanaume saba na mwanamke mmoja walimkamata na kumfunga pingu mikononi

Kisha wakamuingiza katika gari aina ya Landcruiser hard top nyeupe na kuelekea naye mapori ya Kisarawe. Kuanzia Jana Saa Saba mchana wakakaa nae hadi Saa Saba usiku walipo muacha akiwa hoi porini wakidhani wamesha muua.

Bi Aisha Machano ambaye ni Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) amepigwa na kuteswa sanaaa,muda wote wa mateso,watekaji walitaka amtaje kiongozi ambaye aliwatuma BAWACHA kuchoma Vitenge walivyopewa na Rais @SuluhuSamia ktk siku ya wanawake Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 March 2023.

Aisha Machano alimchaniwa nguo zake zote (HIJAB ) akabakia uchi wa mnyama,anapigwa marungu na waya mwilini akiwa na pingu mkononi ,Wakati wote anarekodiwa video na picha na mwanamke mmoja ambaye alikuwa anasimamia zoezi la uteswaji wake.

Wamempora simu yake ya mkononi na Kumtishia akienda Kuongea popote watasambaza picha zake za uchi.

Baada ya Kuachwa porini usiku ule wa Saa Saba ,watekaji wakifikiri wameshamuua tayari.

Bi Aisha Machano baada ya kuhisi pana utulivu na hali ya ukimya alifungua macho na kukuta tayari watekaji wameondoka,

kisha akajikongoja taratibu kutoka porini hadi barabara ya vumbi alipokutana na Vijana wa bodaboda huku akiwa na damu mwili mzima akiwa katika hali ya utupu kama alivyozaliwa.

Bodaboda walimsaidia kumsogeza barabarani na kujistiri na Kumsaidia mawasiliano na viongozi wenzie walio hakikisha anakimbizwa hospitali haraka sana.

Kwa sasa Aisha Machano yupo katika Chumba cha matibabu ya dharula (emergency) jina la hospitali tuna ficha kwa sasa,Madaktari wanajaribu kuokoa uhai wake.
 
Leo ukichoma moto kitenge, kwa nini tusidhani kesho utachoma kitanda na kumuua kabisa?

Kitenge kimekosea nini? Hivi mtu anasafishaje nyumba kwa kutumia uchafu?

Kama huoni kwamba hilo ni tatizo, basi kuna tatizo kubwa.

#MaendeleoHayanaChama
Kwa hiyo mtu akionesha hisia zake kwa kuchoma picha au hicho kitenge basi anatakiwa kutekwa, kujeruhiwa, kuteswa, au kuuwawa siyo!! Nyinyi CCM ni laana tu kwenye hii nchi.
 
Kwa mambo yanayotokea sasa inadhihirisha kabisa Uongozi wa Chadema ni dhaifu. Don’t moan, take actions
Uko wapi udhaifu kutoa taarifa nyie ndo mnasemaha chama cha matukio kwahiyo yakitukia wasitoe taarifa we vipi bans!
 
Chadema wanajiteka wenyewe kuipakazia serikali.

Hawana sera hao.
 
Back
Top Bottom