Aishi Manula anapewa sifa asizostahili! Hawezi kuifikisha popote Simba na Taifa Stars

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Huu ni kweli mchungu, Manula amekuwa akisemwa ni 'Tanzania one' na maneno kibao, lakini ukweli ni kipa wa kawaida sana na kwa kuwa ni wa kawaida naomba niseme timu ya Taifa na Simba hazitafikia kilele cha mafanikio.

Ili timu ifikie kilele cha mafanikio inahitaji kuwa na kipa aliyekamilika wataalamu wanaita A GOOD STOPPER,

Kuna kipindi kipa anatakiwa aibebe timu, hasa kwenye mazingira magumu, hii ndio sifa ya STOPPER,

Kwa kipindi cha nyuma Smba waliwahi kufikia angalau mafanikio ya juu, kwa kuwa na STOPPER kama JUMA KASEJA

Naomba niseme sioni Smba ikitusua mbali zaidi kwa kuendelea kuwa na makipa wa kiwango cha Manula. Hata timu yetu ya Taifa haitafika popote kwa kuendelea kuwa na makipa wakiwango cha Manula

Hebu angalia mtu kama Kakolanya au Jma Kaseja wa enzi zake au yule Dida( Deo Munishi) wa Yanga, kuna kipindi waliziokoa timu zao, zilipokuwa kwenye mazingira magumu

Sikatai Manula ni golikipa mzuri ila sio Stopper wakuifikisha kwenye kilele cha mafanikio Smba na timu ya Taifa,
 
Manula simkubali. Naona Kakolanya anaweza kuwafaa ikiwa ubora wake ni endelevu
 
Yani umezunguka mbuyu weeeeee kumbe lengo lako ni kumtaja kakolanya.
.
Brother let me tell you manula ni habari nyingine usimlinganishe na mtoto mdogo kwa udakaji kama kakolanya, manula enzi yupo azam hakuna aliyekuwa akimsema sana ila kwa kuwa kahamia kwa simba SC basi miyanga nyote nyie mko tofauti nae.
.
Kakolanya kufanya vizuri kwenye mechi dhidi ya simba si sababu ya yeye kuwa bora.
.
Ni sawa na oblak wa atletico de madrid useme ni bora kumzidi de gea eti kwa sababu degea anafanya mistake ndogondogo NEVER degea is still the best.
 
Manul anafungwa magoli ya kindezi sana....
 
Manula ni kuagizia za mbali tu.
Lakini nashauri aendelee kuwa No. 1 pale Simba.
 
Ndani ya miezi minne kafungwa magoli manne kutoka nje ya 18...Alliance,Mwadui,African Lyon na Leo Nkana...ukiona kipa anafungwa mbali kuna walakini
 
Umesema kweli.Hata Mohammed Mwameja alimzungumzia Aishi Manula siku chac kabla ya game ya leo,ana tatizo la kufungwa magoli ya aina ile ile consecutively.

Na Mwameja alisema ushindi wa (kufungwa kwa) Simba dhidi ya Nkana ulikuwa juu ya mabega ya Manula.
 
Mkuu AROON

Uko sahihi kwa hoja yako hii...Manula uwezo wake kwa sasa umepungua mno....Taifa Stars inabidi atafutwe kipa mwingine...Simba waendelee naye au wamtumie Beno ambaye atakwenda huko baada ya Yanga kumshitukia
 
Mkana ni wazuri sana kushinda Simba.
Wanatuzidi fiziki tu basi
 
AROON,
Tukiwaambia ni pazia hawaamini ngoja aendelee kutunguliwa.....Timu iliyofail Azam kimataifa ipo Simba,wawa,boko,manula,kapombe na nyoni
 
Ndani ya miezi minne kafungwa magoli manne kutoka nje ya 18...Alliance,Mwadui,African Lyon na Leo Nkana...ukiona kipa anafungwa mbali kuna walakini
Mpelekeni hospital ya macho inawezekana haoni kama de gea alivyofika United
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…