Watu kadhaa wanahofiwa wamefariki dunia baada ya kutokea ajali iliyohusisha basi lijulikanalo kwa Jina la Geita Express kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T 134 DXR katika eneo la Chinangali II Mkoani Dodoma.
Habari zaidi zinafuata.
Your browser is not able to display this video.
AJALI YA BASI LA GEITA EXPRESS YAUA WATU WANNE
Watu wa nne wamefariki dunia na wengine 19 kujeruhiwa katika ajali ya basi la GEITA EXPRESS namba T 640 DLE linalofanya safari zake kutokea Dar es Salaam kwenda Geita baada ya kukongana na gari namba T 134 DXR Fuso katika kijiji cha Manchali wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Onesmo Lyanga akiwa eneo la tukio amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 10:30 Jioni na ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa gari aina ya fuso kujaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari nakusababisha ajali hiyo.
Majeruhi katika ajali hiyo wamefikishwa katika hospitali ya Uhuru wilaya ya Chamwino na wanaendelea kupatiwa matibabu, huku mmoja wa mashuhuda akitoa ushuhuda juu ya ajali hiyo.
Hapo lazima chanzo kilikuwa kwenye ku overtake
Nlisema hizi ajali watu watakufa kama sisimiz mamlaka husika, abiria nyie endeleeni kuwachekea hao madereva
Na mwendo waoo
Watu kadhaa wanahofiwa wamefariki dunia baada ya kutokea ajali iliyohusisha basi lijulikanalo kwa Jina la Geita Express kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T 134 DXR katika eneo la Chinangali II Mkoani Dodoma.
Awamu ya hofu hatukuona ajali kama hizi. Trafiki na polisi walisimamia sheria za barabarani ipasavyo ila Sasa awamu hii isiyo ya hofu tunapoteza watu kila siku.
Hapo lazima chanzo kilikuwa kwenye ku overtake
Nlisema hizi ajali watu watakufa kama sisimiz mamlaka husika, abiria nyie endeleeni kuwachekea hao madereva
Na mwendo waoo