Ajali iliyohusisha Magari Nane, maelezo ya Polisi yanatia shaka

Ajali iliyohusisha Magari Nane, maelezo ya Polisi yanatia shaka

Hawa Polisi wenzako hata hawafai, Ila Howo mjanja sana, gari lake ziiima, Tela lake ni chuma cha pua, akitoka hapo tajiri anampa allowance yake pooowa kabisa.

gari iko powa??unaandika nini wewe umeona hiyo mipira??

sema dereva mzima,sio lori zima.
 
Nimeshapata misukosuko mingi Sana huko barabarani. Ila kitu niligundua ni kwamba kesi zinazohusu ajali barabarani huwa hazina ushahidi. Kile atakachoandika trafiki ndio ukweli, sana unaishia kuambiwa kama unakubali au unakataa kosa uliloandikiwa. Ili kuokoa muda pia kuondokana na usumbufu unaishia kukubali kosa na kulipa hiyo faini.
 
Ukute Howo alimaliza kuovateki na kurudi upande wake wa kushoto lakini kutokana na mwendo kasi wa Ashok ya nyuma akashindwa kufunga break akaamua kutanua kulia ili asimgonge Ashok mwenzake ndio akakutana na Howo. Just thinking [emoji848].
Aliekuwa anaovertake ni lori au gari ya polisi? Manake aliegongwa ni lori tena akiwa upande wake.
 

Kufa kufaana, waniuzie hiyo V8 aise
2796260_1622708172411.png
 
Angali lory lipo kwenye mstari wake, ila angali picha nyingine dereva wa Lory kakwepesha kichwa chake, dereva wa Gari ya Polisi kaingia hapo. Tusaidiane kuujua ukweli

View attachment 2013481

View attachment 2013482

Angali lory lipo kwenye mstari wake, ila angali picha nyingine dereva wa Lory kakwepesha kichwa chake, dereva wa Gari ya Polisi kaingia hapo. Tusaidiane kuujua ukweli

View attachment 2013481

View attachment 2013482

View attachment 2013483
Mkuu kwa maoni yangu na uzoefu wangu wa udereva, maelezo ya Polisi yako sahihi
Dereva wa Lori alijaribu kurudi kwenye njia yake baada ya kuona uso kwa uso lakini bahati mbaya horse tu ndio ilifanikiwa, tela ndio ikasababisha ajali
ukitizama kwa makini kwenye lami hiyo picha ya mwisho utaona jinsi tairi za kichwa zilivyoacha alama kwenye lami kutoka upande mmoja kwenda mwingine
Ifahamike pia picha huwa inajigeuza hapo ndio wengi mnajichanganya kupata uelekeo
 
Dereva wa Lori alijaribu kurudi kwenye njia yake baada ya kuona uso kwa uso lakini bahati mbaya horse tu ndio ilifanikiwa, tela ndio ikasababisha ajali
ukitizama kwa makini kwenye lami hiyo picha ya mwisho utaona jinsi tairi za kichwa zilivyoacha alama kwenye lami kutoka upande mmoja kwenda mwingine
Ifahamike pia picha huwa inajigeuza hapo ndio wengi mnajichanganya kupata uelekeo
Hebu angalia tena hizo picha taratibu kabisa

IMG-20211116-WA0119.jpg


IMG-20211116-WA0102.jpg


IMG-20211116-WA0091.jpg


IMG-20211116-WA0105.jpg


IMG-20211116-WA0087.jpg
 
Umenena vyema
Nimeshapata misukosuko mingi Sana huko barabarani. Ila kitu niligundua ni kwamba kesi zinazohusu ajali barabarani huwa hazina ushahidi. Kile atakachoandika trafiki ndio ukweli, sana unaishia kuambiwa kama unakubali au unakataa kosa uliloandikiwa. Ili kuokoa muda pia kuondokana na usumbufu unaishia kukubali kosa na kulipa hiyo faini.
 
1. Polisi walikua mwendo kasi kuanzia 80kph.
2. Dereva wa polisi aliovertake sehem isiyoruhusiwa akiwa kwenye mwendo mkali.
3. Baada ya overtake akakutana na lori uso kwa uso ila mwenye roli kajitahidi sana kumwepa.
4. Msafara wa polisi ulio nyuma yao sababu ulkua kwenye mwendo mkali wakajikuta kila mmja anagonga gari la mbele yake, pia hilo ni tatizo la kuendesha mwendo mkali bila kuchukua tahadhari yan walikalibiana sana nd maana wakagongana ovyo ovyo.
5. Polisi wamezembea barabarani, tatizo ajali wanapima wenyewe nd maana dereva wa Lori asie na makosa wamempa kesi ila mwenye makosa ni dereva wa bus la polisi alieovertake sehemu iliyokatazwa.
Polisi wawajibike kwa uzembe wanakataa makosa yao kwan wao ni malaika wamekosea wakubali tu mbn ni kitu kidogo tu.
Hapa natafakari hilo lorry lingekua ni mali ya jeshi sijui wangetunga uongo gani?
Maskini Kristo anabebeshwa msalaba na kwenda kusulubiwa kwa kosa asilolitenda.
 
Nimejaribu kusoma kwa utulivu kisha nikaangalia picha, naona kama yanapingana na uhalisia, anyway Wajuvi nisaidieni, lory HOwo ame-ovrtake kweli hapo??

AFANDE TAARIFA YA AJALI:
KAB/TR/AR/16/2021(×)AJALI YA MAGARI MANANE KUGONGANA NA KUSABABISHA MAJERUHI NA UHARIBIFU WA MAGARI (×) MNAMO TAR 14/11/2021 MAJIRA YA SAA 18:30 HUKO KATIKA KIJIJI CHA KWEDILOMBA KATA YA KWEDIBOMBA TARAFA YA MZUNDU WILAYA YA HANDENI MKOA WA TANGA BARABARA KUU YA SEGERA-CHALINZE GARI NO.T.131 DVU AINA YA HOW YENYE TELA NO.T.329 DMR IKIENDESHWA NA SAIMON S/O KRISTO @MWANYILA, 36YRS, MBENA, MKAZI WA KIBAHA PWANI AKITOKEA KABUKU KUELEKEA CHALINZE ALIPOKUWA AKIJALIBU KULIPITA GARI LA MBELE YAKE MAHALA PASIPO RUHUSIWA NDIPO GHAFLA MBELE YAKE KUKATOKEA GARI NYINGINE ILIYOKUWA IKITOKEA CHALINZE KUELEKEA KABUKU YENYE NO.PT.4036 ASHOK LEYLAND MALI YA JESHI LA POLISI TANZANIA LIKIENDESHWA NA H.3637 CPL JUMA WA CHUO CHA POLIS CCP KILIMANJALO NA NDIPO DEREVA WA GARI NO.PT.4036 ALISIMAMA GHAFLA ILI KUEPUKA AJALI ISITOKEE NA NDIPO BAADA YA GARI HIYO KUSIMAMA GHAFLA IKATOKEA GARI NYINGINE KWA NYUMA ILIYOKUWA IKITOKEA CHALINZE KUELEKEA KABUKU PT.4087 ASHOK LEYLAND IKIENDESHWA NA F.7658 CPL JOHN ROBERT WA MAKAO MAKUU MADOGO YA POLISI DSM NA KUGONGA KWA NYUMA GAFLA TENA IKAJA GARI NYINGINE KWA NYUMA NO.PT.4097 ASHOK LEYLAND IKIENDESHWA NA F.5889 CPL KIGIRI WA POLISI MAKAO MAKUU MADOGO YA POLISI DSM NA KUSIMAMA GHAFLA PT.4087 ASHOK LEYLAND NA KUSABABISHA GARI NO. PT.2370 ISUZU BUS IKIENDESHWA NA G.6123 CPL ABEL WA CHUO CHA POLISI KIDATU NA KUGONGA UBAVUNI GARI NO.PT.4087 ASHOK LEYLAND PIA IKATOKEA TENA GARI NO.T.573 AYR TOYOTA COROLLA IKIENDESHWA NA AMIN S/O UR RASUL@KHAN, 60YRS, MKAZI WA TANGA NA KUSIMAMA GHAFLA BAADA YA KUONA AJALI NA KUSABABISHA GARI NO.SU 44275 GX V8 MALI YA TANESCO DSM IKIENDESHWA NA JUMA S/O HASSAN Lean NA KUIGONGA KWA NYUMA GARI HIYO NO.T.573 AYR TOYOTA COROLLA PIA IKASABABISHA GARI NYINGINE YENYE NO T.773 CND TOYOTA HILUX KUIGONGA KWA NYUMA GARI HIYO NO.SU.44275 GXV8 TANESCO NA KUSABABISHA MAJERUHI KWA WATU 16 AMBAO NI 1.D.8420 S/SGT JOHN MWAKIPESILE 2.PF.18891 INSP SISTER 3.G.6123 CPL ABEL AMBAO WOTE WATATU WAMEPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA BOMBO KWA MATIBABU NA 4.PF.17534 INSP RASHIDA 5.PF.18326 INSP NYALUGEMBE 6.PF.17896 INSP GONGA 7.PF.18202 INSP SAID 8.PF.17166 INSP ALLY JUAKAL 9.PF.17899 INSP SANYA 10.PF.18445 INSP PANGANE 11.PF.17691 INSP PETER 12.PF.18719 INSP OHUSSO 13.PF.17321 INSP ILOMO 14.PF.18616 INSP ANTHONY 15.PF.17674 INSP ZONGHO 16.H.1659 PC GIFT (×) MAJERUHI WOTE WAMEUMIA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI NA KUTIBIWA KITUO CHA AFYA KABUKU NA KURUHUSIWA (×) CHANZO CHA AJALI NI UZEMBE WA DEREVA WA GARI NO.T.131 DVU HOW YENYE TELA NO.T.329 DMR KUJALIBU KULIPITA GARI ILIYOKUWA MBELE YAKE PASIPO KUCHUKUWA TAHADHALI (×) DEREVA AMEKAMATWA YUPO MAHABUSU KITUO CHA POLISI KABUKU KWA AJILI YA MAHOJIANO (×) ENEO LA TUKIO LIMEKAGULIWA NA ACP. SOFIA JONGO RPC TANGA AKISAIDIWA NA SSP LEOPORD .N. FUNGU RTO TANGA , SP. ELIAS RWAMBANO OCS KABUKU, A/INSP RAJABU KAIMU DTO HANDENI PAMOJA NA G.3191 CPL MUSSA AMBAYE NDIYE AMECHORA NA KUPIMA ENEO LA TUKIO (×)///////////
TAARIFA KWA MAANDISHI INAFUATA //////////

TOKA RTO TANGA ///////////

View attachment 2013471
Hawa madereva wa polisi walikuwa wanashindana barabarani na kusababisha ajali na majeruhi, sasa wanamuangushia zigo la kesi dereva raia. Ajabu hadi RPC anahusika kwenye kubambika kesi kwa raia, aibu kubwa, wanathibitisha mashaka ya raia juu ya uadilifu wa jeshi la polisi.

Vv
 
Back
Top Bottom