Ajali iliyohusisha Magari Nane, maelezo ya Polisi yanatia shaka

chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari no.T.131 dvu how yenye tela no.T.329 dmr kujalibu kulipita gari iliyokuwa mbele yake pasipo kuchukuwa tahadhali (×) dereva amekamatwa yupo mahabusu kituo cha polisi Kabuku kwa ajili ya mahojiano
Polisi si wa kuwamini hata kidogo,
Ukiangalia kwa macho ya kawaida kabisa utaona kwamba Lorry T131 DVU lipo kwenye site yake isipokuwa Basi la Polisi Ashok Leyland ndilo linaonekana lilikuwa likitaka kulipita Basi lingine la Polisi lkn alishindwa kumaliza kwa sababu aidha alikosea timing au ni uzembe ambao polisi wanao kwa kutumia nguvu zaidi kuliko akili!!!

Wakati mwingine Polisi wasijitishe hiz aibu za waziwazi kwa kuihada Umma. naamini Polisi wachache ndio wanaoharibu taswira ya jeshi zima la polisi ni jukumu la viongozi wao kutokufumbia macho maswala kama haya yaliyo waziwazi!!!
 
Basi la Polisi Ashok Leyland ndilo linaonekana lilikuwa likitaka kulipita Basi lingine la Polisi lkn alishindwa kumaliza kwa sababu aidha alikosea timing au ni uzembe ambao polisi wanao kwa kutumia nguvu zaidi kuliko akili!!!
Walikuwa kwenye ligi, kwa mtazamo wangu, jamaa akakomaa ampite jamaa sehemu isiyoruhusiwa, ghafla likatokea lory, jamaa aakrudisha basi kushoto, jamaa yake badala ya kukwepa aingee mtaroni, akakomaa barabarani, matokeo yake huyo kaingi hapo na huyo kamla hapo kwenye shoo
 
Ashok kwa Ashok mweee polisi jamani kweli wanatakiwa walinde tu bank mengine wayaache!!!
 
ndio polisi wa Tanzania; nguzo yao kuu ni UONGO! Kama jambo la wazi hivi wanadanganya, yale ya sirini hali ikoje? Kinachoitwa taarifa za polisi nchi hii sio cha kuamini kabisa!


Sina mengi ya kusema ila polisi wa tz ni waongo sana
 
Kuna mkanganyo mkubwa:

1: Namba ya tela inayotajwa siyo inayoonekana kwenye picha, labda kuna gari jingine?

2: Mpaka upate namba za magari yote kwa uhakika ndo unaweza kujua ukweli.
Peleka upumbavu wako huko,kusoma hujui hata picha ?
 
Picha tu, zinaeleza kila kitu. Lorry liko upande wake, tena karibu linaacha njia, basi la polisi limechukua nafasi ya lori linalojaribu kulikwepa Hilo basi la kwanza. Kama kawaida yao, inaonesha polisi walikuwa mwendo Kasi, wakifuatana Kwa karibu, wakitanua pia ndio maana wameishia kugongana Kwa nyuma. Magari mengine yote ni wahanga wa ubabe wa hii laana inayoitwa polisi.
 
Kama ni kweli RTO, anaweza kutoa maelezo hayo, huku picha zinaonyesha basi mbili za PT zikiwa sambamba kama parallel lines za kwenye maumbo ya hesabu za darasa la 5, basi niungane na James Mbatia, kulia mama Tanzania.

Everyday is Saturday................................😎
 
Kuna mkanganyo mkubwa:

1: Namba ya tela inayotajwa siyo inayoonekana kwenye picha, labda kuna gari jingine?

2: Mpaka upate namba za magari yote kwa uhakika ndo unaweza kujua ukweli.
Na sio No tu na hata hicho kichwa cha lorry ni FAW na sio HOWO me naona watu wanatiririka tuu au kuna picha nyingine mimi sijaziona
 
Inawezekana wewe ni polisi au akili zako hazipo timamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…