Ajali iliyohusisha Magari Nane, maelezo ya Polisi yanatia shaka

Ajali iliyohusisha Magari Nane, maelezo ya Polisi yanatia shaka

Nimejaribu kusoma kwa utulivu kisha nikaangalia picha, naona kama yanapingana na uhalisia, anyway Wajuvi nisaidieni, lory HOwo ame-ovrtake kweli hapo??

Afande taarifa ya ajali:

KAB/TR/ar/16/2021(×)ajali ya magari manane kugongana na kusababisha majeruhi na uharibifu wa magari (×) mnamo tar 14/11/2021 majira ya saa 18:30 huko katika kijiji cha Kwedilomba kata ya Kwedibomba tarafa ya mzundu wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga barabara kuu ya Segera-Chalinze gari No.T.131 DVU aina ya HOW yenye tela No.T.329 DMR ikiendeshwa na Saimon S/O kristo @Mwanyila, 36yrs, Mbena, mkazi wa Kibaha Pwani akitokea kabuku kuelekea Chalinze alipokuwa akijalibu kulipita gari la mbele yake mahala pasipo ruhusiwa ndipo ghafla mbele yake kukatokea gari nyingine iliyokuwa ikitokea Chalinze kuelekea kabuku yenye No.Pt.4036 ashok leyland mali ya jeshi la polisi Tanzania likiendeshwa na H.3637 CPL Juma wa chuo cha Polis CCP Kilimanjalo na ndipo dereva wa gari No.Pt.4036 alisimama ghafla ili kuepuka ajali isitokee na ndipo baada ya gari hiyo kusimama ghafla ikatokea gari nyingine kwa nyuma iliyokuwa ikitokea Chalinze kuelekea Kabuku PT.4087 ashok leyland ikiendeshwa na F.7658 CPL John Robert wa makao makuu madogo ya polisi DSM na kugonga kwa nyuma.

Ghafla tena ikaja gari nyingine kwa nyuma No.Pt.4097 ashok leyland ikiendeshwa na F.5889 CPL Kigiri wa Polisi makao makuu madogo ya Polisi DSM na kusimama ghafla PT.4087 ashok leyland na kusababisha gari No. PT.2370 Isuzu bus ikiendeshwa na g.6123 CPL abel wa chuo cha polisi Kidatu na kugonga ubavuni gari no.Pt.4087 ashok leyland pia ikatokea tena gari No.T.573 AYR toyota corolla ikiendeshwa na Amin S/O UR Rasul@Khan, 60yrs, mkazi wa Tanga na kusimama ghafla baada ya kuona ajali na kusababisha gari no.SU 44275 gx v8 mali ya TANESCO DSM ikiendeshwa na Tuma S/O Hassan lean na kuigonga kwa nyuma gari hiyo no.T.573 AYR Toyota corolla pia ikasababisha gari nyingine yenye no T.773 CND Toyota hilux kuigonga kwa nyuma gari hiyo no.Su.44275 GXV8 TANESCO na kusababisha majeruhi kwa watu 16 ambao ni 1.D.8420 s/SGT John Mwakipesile 2.Pf.18891 insp sister 3.G.6123 CPL Abel ambao wote watatu wamepelekwa hospitali ya rufaa Bombo kwa matibabu

Na 4.Pf.17534 insp Rashida 5.Pf.18326 insp Nyalugembe 6.Pf.17896 insp Gonga 7.Pf.18202 insp Said 8.Pf.17166 insp Ally juakal 9.Pf.17899 insp Sanya 10.Pf.18445 insp pangane 11.Pf.17691 insp Peter 12.Pf.18719 insp Ohusso 13.Pf.17321 insp Ilomo 14.Pf.18616 insp Anthony 15.Pf.17674 insp Zongho 16.H.1659 pc gift (×) majeruhi wote wameumia sehemu mbalimbali za mwili na kutibiwa kituo cha afya Kabuku na kuruhusiwa (×) chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari no.T.131 dvu how yenye tela no.T.329 dmr kujalibu kulipita gari iliyokuwa mbele yake pasipo kuchukuwa tahadhali (×) dereva amekamatwa yupo mahabusu kituo cha polisi Kabuku kwa ajili ya mahojiano (×) eneo la tukio limekaguliwa na acp. Sofia jongo rpc Tanga akisaidiwa na ssp leopord .N. Fungu rto tanga , sp. Elias Rwambano ocs Kabuku, a/insp Rajabu kaimu DTO Handeni pamoja na g.3191 cpl Mussa ambaye ndiye amechora na kupima eneo la tukio (×)///////////

Taarifa kwa maandishi inafuata //////////


Toka rto tanga ///////////

Polisi kiutani utani mnaliingiza Taifa kwenye aibu ya mwaka kwa kuunga unga facts ambazo mwenye akili timamu anajua ni uongo mtupu.
 
Mbona huyo Mwenye Lorry yuko sahihi upande wake wa kushoto? Na inaonekana hilo basi jeusi la polisi ndio limemfuata upande wake?! Huu ujinga gani huu wanaleta?
Mkuu kwa kuangalia hiyo tu picha huwezi tambua mpaka uwe unalielewa eneo ikiwemo hiyo picha imepigwa toka upande gani.
 
Mkuu kwa kuangalia hiyo tu picha huwezi tambua mpaka uwe unalielewa eneo ikiwemo hiyo picha imepigwa toka upande gani.
Wewe ni mpumbavu sana, wewe ni hooligan , uiwe unapinga ujinga, ukute hata Suzuki Swift huna
 
Mimi nina V8 na nina ishi kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi Mbezi. Unafikiri mimi ni utopolo kama wewe!
Ewaaaaa, ndio maana akili zako ziko hivi zilivyo! Mnalinda matumbo yenu mnanyonya maskini, mjinga mkubwa wewe, you will soon pay....subiri.
 
chanzo cha ajali ni polisi hiyo iko obvious kabisa. ukiangalia gari ya kwanza ya polisi iko wrong site. alikuwa anatafuta nn huko? kama kuovertake je alijiridhisha kuko salama?
hilo halitoshi bado gari ya pili ikagonga hapo hapo ina maana alikuwa spidi sana.
 
Hii report ina walakin,,, maana hata plate number ya tela iliyoandikwa kwenye report ni tofauti na plate number inayoonekana kwenye picha,
Inawezekanaje hii???[emoji848]
Nasikitika watu wanalidiscuss lori wanaloliona pichani wakati lori lililotajwa kwenye maelezo siyo linaloonekana kwenye picha...

Watu wanashindwa kuuliza vitu vya msingi kama hivyo...

Usishangae hilo lori lililotajwa kwenye maelezo hata halikuwepo eneo la ajali ila polisi wameliweka ili kufunika makosa ya hilo basi la PT lililokuwa linaovertake.
 
Unajifanya MJUAJI utadhani ulikuwepo wakati ajali inatokea!!
Mimi nimesoma Crash investigation unaweza ukapewa tu picha ya ajali na mchoro ukatakiwa kurecreate video ajali ilitokeaje?

Usione kama ni vitu vya ajabu hiyo ajali iko simple inajieleza.
 
Nasikitika watu wanalidiscuss lori wanaloliona pichani wakati lori lililotajwa kwenye maelezo siyo linaloonekana kwenye picha...

Watu wanashindwa kuuliza vitu vya msingi kama hivyo...

Usishangae hilo lori lililotajwa kwenye maelezo hata halikuwepo eneo la ajali ila polisi wameliweka ili kufunika makosa ya hilo basi la PT lililokuwa linaovertake.
Mkuu Shalom,
Kwa hiyo unasuspect lori lililosababisha ajali limekimbia?
 
Na sio No tu na hata hicho kichwa cha lorry ni FAW na sio HOWO me naona watu wanatiririka tuu au kuna picha nyingine mimi sijaziona
We ni mtu wa tatu unayefikiria sawasawa hunu JF?

Kiukweli nimesikitika sana vitu watu wanachangia...

Maelezo ya Polisi ni ya uongo sababu hayaendani na picha zinazooneshwa.
 
kwa maelezo tajwa, dereva na lori lilihusishwa kuovertake halipo hapo..ukisoma tela no according to hiyo report na ukiangalia trailer iliyopo pichani haziwiani usajili.. huyo aliyehama na kwenda kubusanisha vyuma alitanua kulia badala ya kushoto baada ya gari ya mbele yake kusimama ghafla.. ishu kubwa hapo ni mwendo waliokuwa nao walinda usalama wa raia na mali zao, walikuwa mwendo wa msafara bila kisafisha njia wala strobes ..yaani mtaani tunasema walikuwa wanamwaga moto bila king'ora wala vimulimuli. hivyo basi, huyo deree aliyeacha zahma huko nyuma (inasemekana aliosha yaani chap kwa haraka )asibebeshwe zigo lote ..makosa ya kibinadamu yalitokea pande zote ..situation awareness and defensive driving haikukamilika kotekote.
Upo sawa
 
Hiyo HOWO ikowapi kwani naona kila mtu dereva wa HOWO mara hivi mara vile kwenye hizo picha mi nimeona kichwa cha lorry ni FAW
Suala la Howo wewe ndio umenifumbua macho ila toka mwanzo nilidoubt suala la plate number....

Kwamba plate za Lori linalotajwa kwenye report halipo pichani.,
 
Back
Top Bottom