Ajali iliyoua watu 17 Tanga imeondoka na Mume, Watoto 2 na Mjukuu

Ajali iliyoua watu 17 Tanga imeondoka na Mume, Watoto 2 na Mjukuu

Wachaga na makabila mengine wenye huu mtindo wa kwenda kuzika mikoani waache nao umepitwa na wakati lasivyo matukio kama haya yataendelea
 
Mioyo yao imepooza kwa kutanguliza kitu sio utu, dah hiyo kauli ingesemwa na watu wa nje sio mwanafamilia labda kidogo wangesubiri wazike,, aisee balaa hili
Ni kawaida kwa binadamu hata ungekuwa wewe ungesema maneno hayo hayo maana yapo ktk mtiririko wa sentence moja ya kuonyesha jinsi gani tukio fulani limekuumiza na pia hatujui kiini cha jibu hilo labda mwandishi aliuliza swali lenye maudhui hayo.
 
Mh hata mwandishi kuuliza haikutakiwa kulijibu kiivyo na mwandishi nae kuuliza swali la mlengo huo sio utu
 
Wachaga na makabila mengine wenye huu mtindo wa kwenda kuzika mikoani waache nao umepitwa na wakati lasivyo matukio kama haya yataendelea
Mzee!!!

Kifo kikipangwa ufe/mfe utakufa au mtakufa tu,haijalishi unaenda Msanga au makaburi ya Kisutu.kuacha kusafiri hakujawahi kufanya ajali zizisitokee unless umeamua kujitoa ufahamu tu.
 
Acha tu 😢 😭 hili ni pigo kubwa sana. Mbali na kuwapoteza wanafamilia kwenye msiba huu. Nimepata taarifa mbaya jirji yangu wa kike mtani wangu kakutwa kafariki ufukweni kigamboni. Mkononi alikuw na barca kuwa kajiua, Marehemu yuko muhimbili mochwary. kesho nadhani taarifa zitakuja kamili kuhusu kifo chake. Asha maini tutakukumbuka daima. .
Pole saana mzee
 
Tatizo wachaga wana mila nyingi bado. Wachek kwenye makabrasha yao huenda wazee wao hawajapata mbege bado
Kwakweli wajichunguze vizuri, tatizo la koo kubwa hamnaga maelewano tena viongozi wawe ni kizazi chetu hiki aaah hawachelewi kukwambia tupo digital, mi kwenye familia nilijaribu kidogo kuweka ishu sawa kusuluhisha migogoro ila vikwazo nilivyopata hamu sina, na vile ni ke basi tunadharaulika, nikaachana navyo kwetu ni kule nilikoolewa fullstop
 
🤣🤣🤣

Sasa wakibosho hadi leo wanatafuna mkungu mzima wa ndizi mbichi na kutema kwenye kaburi la mzazi...eti km ni wewe umeua unakufa🤣🤣🤣🤣🤣

Mtoto wa nje ya ndoa ambaye mama alimsingizia baba hazikwi kwenye mji ule kwakuwa ikifanyika hivyo msururu utaambatana nae

Yani mila lukukii
 
🤣🤣🤣

Sasa wakibosho hadi leo wanatafuna mkungu mzima wa ndizi na kutema kwenye kaburi la mzazi...eti km ni wewe umeua unakufa🤣🤣🤣🤣🤣

Mtoto wa nje ya ndoa ambaye mama alimsingizia baba hazikwi kwenye mji ule kwakuwa ikifanyika hivyo msururu utaambatana nae

Yani mila lukukii
Mila ndo asili yetu wazungu wanatamani wangekuwq nazo ila ndo hivyo, kinachofata ni kutupumbaza ili tudharau mila zetu
 
Mzee!!!

Kifo kikipangwa ufe/mfe utakufa au mtakufa tu,haijalishi unaenda Msanga au makaburi ya Kisutu.kuacha kusafiri hakujawahi kufanya ajali zizisitokee unless umeamua kujitoa ufahamu tu.
Nisawa ila isingetokea kama hivyo ukoo mzima au familia nzima bila survivor katika famillia
 
Ni vilio na simanzi vimetawala nyumbani kwa familia iliyopoteza ndugu 14 wa familia moja kati ya 18 waliofariki kwa ajali ya gari mkoani Tanga jana Ijumaa usiku wa Februari 3, 2023.

Katika ajali hiyo wamo mume na mke waliopeza maisha, mama na mwanaye na nyumba moja ambayo imepoteza watu wanne wakiwemo baba na watoto wake wawili pamoja na mjukuu huku wengine wakiwa ni ndugu wa familia hiyo ya Mrema.

Ajali hiyo ilitokea eneo la Magira Gereza, Kata ya Magira Gereza, wilayani Korogwe, barabara ya Segera - Buiko na kusababisha vifo hivyo pamoja na majeruhi 12 wakati wakisindikiza mwili wa ndugu yao, Athanas Mrema (59) aliyefariki dunia Februari Mosi, kutokea jijini Dar es salaam kuja mkoani Kilimanjaro ndipo walipokutana na ajali hiyo.

Hata hivyo, miili hiyo ya watu 14 inatarajiwa kupokewa kesho Jumapili wilayani Rombo na itahifadhiwa katika Hospitali ya Huruma na Kituo cha afya Karume kwa ajili ya taratibu za mazishi ambayo yatafanyika Jumatatu katika Kitongoji cha Kirungu Mokala, Kata ya Kelamfua Mokala, wilayani humo.

Mmoja wa ndugu wa familia hiyo, Colman Mrema amesema tukio hilo la vifo vya watu 13 ni pengo kubwa kwa familia na halitazibika na kwamba limewaachia majeraha makubwa kwani siyo tukio la kwanza kutokea.

Wakati akizungumza na Mwananchi Digital, idadi ya vifo ilikuwa 13 lakini baadaye jioni ya leo, majeruhi ambaye ni mtoto aliyekuwa amelazwa chumba cha ungalizi maalum (ICU) naye alifariki dunia.

Amesema miaka 10 iliyopita familia hiyo hiyo ya Mrema ilipoteza watu wengine wanne katika ajali eneo la Makanya wilayani Same.

Amesema tukio hilo limeleta sehemu kubwa ya umaskini katika ukoo wao kwani wengi wao waliofariki katika ajali hiyo ni wafanyabiashara na wasomi ambao walikuwa wakitegemewa katika ukoo huo wa Mrema.

"Hili tukio haliwezi kuelezeka ni la kutisha na limeleta sehemu kubwa sana ya umaskini katika familia na ukoo wetu, hili ni pengo ambalo kamwe haliwezi kuzibika kwani ndani yake kuna wasomi, wafanyabaishara, ni tukio lisilo la kawaida," amesema.

Selina Silayo, mmoja wa majirani na familia hiyo amesema tukio hilo ni la kihstoria na kwamba katika mazingira ya kawaida ya kibinadamu ni ngumu kuipokea hali hiyo.

"Hili tukio limetuumiza sana kwa kweli maana leo tumekuja hapa kuzika lakini tumekutana na taarifa nyingine, Mungu aitie familia hii nguvu kuupokea huu msiba maana siyo mwepesi," amesema.

MWANANCHI
So sad
 
Nisawa ila isingetokea kama hivyo ukoo mzima au familia nzima bila survivor katika famillia
Mkuu nielewe!!!

Siyo mimi wala wewe anayeijua dakika moja ijayo tutakuwaje kwani unadhani hao marehemu ni mara yao ya kwanza kusafirisha misiba kama hivi?imepangwa iwe hivyo na imekuwa hakuna cha wangebaki mjini wala wangefanyaje hao ilishaandikwa wataondoka saa fulani mwaka fulani na kwa pamoja wakati umefika wametembea.
 
This is so sad! Mungu azilaze roho za marehemu mahali salama. 🙏🏽
 
Miaka 10 iliyopita familia hiyo ya mrema ilitokea ajali wakafariki watu wengine 4 Makanya same,huenda walikua na mitambiko na sasa wameacha
Lakini bado hawakujifunza familia nzima kukaa kwenye gari pamoja , wakati mwingine ni vizuri kugawana usafiri wengine huku wengine kule..

Wapumzike kwa amani.
 
Lakini bado hawakujifunza familia nzima kukaa kwenye gari pamoja , wakati mwingine ni vizuri kugawana usafiri wengine huku wengine kule..

Wapumzike kwa amani.
Yes,watu wasilundikane kwenye bus moja,alisisitiza marehemu babu yangu
 
Back
Top Bottom