Kwanza kabisa nianze kwa kutoa pole kwa Familia zote zilizokumbwa na huu Msiba mzito na mkubwa kabisa, pili nitoe pole zangu za dhati kabisa kwa Wana Arusha wote bila kumsahau Mkuu wao wa Mkoa Comrade Mrisho Gambo na mwisho kwa Watanzania wote kwa janga hilo lililotokea hapa nchini Kwetu Tanzania na tumuombe Mwenyezi Mungu azipokee roho na Watoto wetu wote, Walimu na Dereva wa gari lile la Shule ya Lucky Vicent aziweke mahala pema peponi Amin / Inshaallah.
Kwa mtazamo wangu binafsi naweza nikapingana na Mtoa mada juu ya baadhi ya lawama zake alizoziweka hapo juu japo nikiri wazi pia kuwa kuna mahala pengine amesema mambo ya wazi na ya kweli kabisa ambayo Mamlaka husika zinapaswa kuyachukua na kuyafanyia Kazi.
Najua kuwa wengi wetu tunaweza kumtupia lawama yule Dereva wa lile Basi ila niseme tu wazi kuwa ile ajali ya jana imetokea kwa BAHATI MBAYA sana na haina cha kumlaumu. Ukiona ajali yoyote ile inayohusisha Mabasi ya Abiria halafu hadi Dereva na zingine Dereva na Utingo / Kondakta wake nao ' wamekufa ' basi jua ya kwamba hiyo Gari hata Yeye ( Dereva ) ilimshinda na siyo ya kawaida.
Inasemekana kwamba sababu kubwa hadi iliyopelekea hiyo ajali ni kwamba Basi lilikuwa katika Spidi kiasi na siyo kubwa kama ambavyo tunaanza kupeana ' Sumu ' mitandaoni na kwamba Gari lilipofika katika huo Mlima kulitokea ' Ukungu ' mkubwa mno wa ghafla hali ambayo ulimchanganya Dereva kiasi cha kutaka kupunguza kidogo Spidi ili aende kwa ' tahadhari ' ndipo Gari lile ( Basi ) likaanza ' kuyumba ' huku likisaidiwa na ' utelezi ' uliokuwepo pale na ambao ulitokana na hali ya ' unyevu unyevu ' hali ambayo ilifanya Gari lile likose mwelekeo na kuanza kuyumba yumba hadi likaingia ' Korongoni ' pale na kusababisha yale ' mauti ' ya kutukuka ya Watoto wetu wapendwa, Walimu wao na Dereva.
Nadhani kwa maoni yangu kama tukisema tutupe lawama mahala fulani basi itapendeza sana kama tukizipeleka hizi lawama zetu kubwa kwa Mamlaka husika hasa Tanroads ya Mkoa wa Arusha na hata Serikali vile vile kwa kuweza ' kuzembea ' kuweka angalau ' Vizuizi ' vya pembeni ( Kingo ) ili kuweza kuepusha ' Ajali ' kama hii kwani hata ukiangalia tu ile sehemu ilipotokea ajali utaona ni barabara nzuri tu ila hapo katika bonde hakuna ' Kingo ' zozote hivyo ni rahisi mno kwa Gari lolote kutumbukia humo pindi pakitokea ' hitilafu ' yoyote.
Mwisho kabisa nimalizie tu kwa kusema kuwa kuanza kuwalaumu Walimu wa Shule au Mmiliki wa Shule au sijui Madereva wa wale Wanafunzi hakutosaidia kitu kwani wao kama wao walitimiza wajibu wao na bahati nzuri ni kwamba kumbe hii siyo mara ya Kwanza hao Watoto wanaenda kufanya hiyo mitihani ya ujirani mwema na kwamba ni mara ya tatu isipokuwa tu sisi kama Wanadamu tutambue kuwa kuna bahati mbaya maishani na siamini kabisa kama Walimu au Mmiliki wa Shule hiyo ya Lucky Vicent alipanga hili kutokea au hata amelifurahia.
Ni ajali tu ya bahati mbaya hivyo kikubwa tu kama Wanadamu kuanzia sasa tunatakiwa tuchukue tahadhari siyo tu hapo Karatu bali hata maeneo mengine ambapo tunajua kuna miundo mbinu mibovu au hali ya barabara siyo nzuri pindi pakiwa na mvua na hata Wahusika hasa TANROADS nao wanapashwa kuhakikisha kuwa sehemu zote hatarishi za barabara Kuu za Mabasi usalama wake hasa wa Kingo za bondeni umezingatiwa ili basi Tanzania isije ikapata tena ' Mkasa ' mkubwa kama huu.
Poleni sana Watanzania wote na GENTAMYCINE nipo nanyi katika ' majonzi ' katika kipindi hiki kigumu kabisa cha huu Msiba kikubwa tuwape ushirikiano mkubwa na wa hali na mali ' Wafiwa ' wote, tuwafariji na tuwaombee Mwenyezi Mungu awape moyo wa ' subira / uvumilivu ' mpaka pale tutakapowapumzisha ' Wapendwa ' wetu katika Nyumba zao za Milele na wala hakuna haja ya kuanza kuichukia Shule ya Lucky Vicent au kumchukia sijui Mwalimu Mkuu au Mmiliki wake kwani hili jambo lingeweza kutokea mahala popote pale na hata kumtokea Mtu yoyote yule.
Muinto Obrigado nyote na tupo pamoja.