Ajali mbaya Ilula: Basi limegonga na kuua waendesha bodaboda wawili

Ahsante kwa taarifa na pole kwa wafiwa na wahanga wa ajali kwa ujumla.
 
Basi limefyeka waendesha bodaboda wawili Ilula mabandani asubuhi hii.

Wamekufa papo hapo.

Safari yangu na siku yangu imeharibika asubuhi hii kwa kuona maiti.
Pole sana Ndugu kwa Kuishuhudia hiyo Ajali mbaya ila kuna sehemu nyingine Gari ya Wagonjwa iliyokuwa imembeba Mgonjwa mahututi kumuwahisha Hospitali imepata Ajali ambapo Dereva na Muuguzi wamekufa papo hapo na cha Kushangaza Mgonjwa nae ghafla tu akapona na kutaka arejeshwe Kwake aendelee na Majukumu yake ya Kawaida ya Kujenga nchi.
 
Guys na mimi ni msafiri tu.

Huyo bodaboda mmoja alikuwa kampakia mama, bodaboda na huyo mama wote wamekufa.

Mbele tumeona basi mbili zimekamatwa mojawapo ni NEW FORCE, nahisi huyu New Force ndio kafanya mambo kwa fujo zake.

Sehemu inaitwa Ilula mabandani.

Basi lilikuwa linaenda Dar
 
Hivi hao New Force huwa wana nani nyuma yao,wameua sana watu kwa ajali lakini bado wanaendelea na biashara au ni ma agent wa shetani?
 
Waafirka tuna matatizo sana. Yaani inakuwaje unamwona binadamu mwenzio anakatisha halafu ndio kwanza unakanyaga mafuta wakati chombo kina pedal ya breki? Kuna ushetani fulani, eh?

isitosho barabara ya mwendo kasi ni clear unaona hata km 1 haina msongamano wala guta wala baiskeli huwa wanafanya kusudi kugonga mtu
 
Hii habari imeletwa hapa 3hrs ago.... New Force gani imefika Ilula saa 4 asubuhi? Kutoka wapi?
 
Reactions: y-n
Hii habari imeletwa hapa 3hrs ago.... New Force gani imefika Ilula saa 4 asubuhi? Kutoka wapi?
Inawezekana mtu akaleta thread ya ajali bila kushuhudia? Atakuwa anataka kuleta taharuki.
 
Nilijuta. Yaan yule kijana ameniumaa[emoji24][emoji24]
Na simu akaibiwaa. Bodaboda akakimbia. Ila hawa wanajeshi wanaoendesha mwendokasi wanakimbia sana. Yaan dah
Ni kweli wanajeshi ndio wanaendesha mwendokasi? Basi serikali itakuwa imefeli sana.
 
Hii habari imeletwa hapa 3hrs ago.... New Force gani imefika Ilula saa 4 asubuhi? Kutoka wapi?

Kwa sababu gari za Njombe kama Njombe Xpress, Luwinzo, Galaxy nk hufika Iringa Mjini saa 3 na Ilula saa4. Kampuni ya New Force haina route ya Njombe.
 
Reactions: y-n
Ni kweli wanajeshi ndio wanaendesha mwendokasi? Basi serikali itakuwa imefeli sana.
Eeh. Niliwaelewa kwa kiasi chake kwa sababu zilizopelekea kuendesha.

Aisee zinatembea mno. Ukute express tena yale yako joint utafurahi. Yaan huo mwendo dah. Abiria alianguka kwneye boda. Mwendokasi akawa anajitahidi kumkwepa lkn wapi. Ndo akaenda pasua mpk ubongo. Kijana wa just 25 mpk 27 yrs hv alikua anasafiri maskini[emoji24][emoji24]
Begi lake likabaki palepale. Boda akakimbia akaacha pikipiki palepale. Mwendokasi akanyoosha aakaenda telekeza basi sijui big brother pale. Acha kbs. Mpk sasa roho inaniuma. Na ni siku 3 zimepita hapohapo shekilango wamegongwa wawili tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…