Ajali mbaya, madereva muwe makini

Pole yao
Wenye magari wawe wanaangalia matairi kabla ya safari na kuhakikisha imefanyiwa service kwa ujumla

Usidharau kitu chochote na kusema ntaifanya tukifika mahali bora kulala kuliko kuendesha ikiwa na faulty

Ajali zinazotokea kila kukicha ni uzembe wa kutokufanya ukaguzi wa mara kwa mara
Hakuna mchawi hapo
 
Uko sahihi sana. Mara nyingi watu wanatumia usemi "Aa, mungu yupo tutafika salama!" Mungu Mwenyewe anasema:"Hapendi kujaribiwa!" Siku zote Huwa hamsaidii mtu mzembe.
 
Sasa mzee umetoka kwny Intercooler umehamia kwny Evo vs Subaru.

Dunia Ina Mengi aisee.
 
Uko sahihi juzi naelekea sehemu gari imezingua wakajifanya mafundi wakafunga kamba sijui nini...kila tukisogea gari inasumbua mbona hatukufika....yaani madereva wanachukuliaga poa sana but mwisho wa siku mambo yanaharibika!
 
Yaani hizo Mitsubishi Pajero 2800 Intercooler Turbo zenye Hp 124 tu ndio unasema Zina performance Kali?Kwa kunesanesa tu hilo Gari nalikubali.
Mwenyewe nimeshangaa sababu hata kale kaji Opa kangu on full speed kanakamua horses zaidi ya hizo! Pajero toka lini ikawa performance car?

Hio ni gari ya Towing zaidi sababu torque yake ni kali ila sio speed!
 
Mkuu ongelea Lancer ila sio hilo dubwana aisee!

Tunaweza kubeti kwenda jino kwa jino Nikaweka kamkweche kangu vs hilo jigari na ntalichapa fasta na kula hela yako na hutaamini kuwa natumia engine yenye 1000cc less than hilo 2.8L
 
Yaani hizo Mitsubishi Pajero 2800 Intercooler Turbo zenye Hp 124 tu ndio unasema Zina performance Kali?Kwa kunesanesa tu hilo Gari nalikubali.
Dah.... Labda aliposema performance Kali ndiyo kajichanganya...hakuelezea...lakini M/Pajero naikubali sana....na... imekuwa na best performance kwa kundi lake mara nyingi zaidi kuliko gari lolote. 🤣🤣🤣🤣🤭
 
Mwenyewe nimeshangaa sababu hata kale kaji Opa kangu on full speed kanakamua horses zaidi ya hizo! Pajero toka lini ikawa performance car?

Hio ni gari ya Towing zaidi sababu torque yake ni kali ila sio speed!
Dah...mkuu Kila gari lina kundi lake...Kama ilivyo michezo....soka...kikapu...netball....Sasa sijui unalinganishaje Opa na Pajero? 🤣🤣🤣🤣🤭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…