TANZIA Ajali Mbeya: Watu wanne akiwemo Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wamefariki dunia

TANZIA Ajali Mbeya: Watu wanne akiwemo Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wamefariki dunia

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia huku wengine wakijeruhiwa baada ya Lori kufeli breki na kugonga Magari madogo mawili, katika mteremko wa Inyala mkoani Mbeya.

ca9fc0f3-d636-4806-951f-70e494cd1d32.jpg

Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi.

ITV

==============================

Watu wanne akiwemo Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, wadaiwa kufariki dunia hii leo huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya Lori kufeli breki na kugonga magari madogo mawili, katika mteremko wa Inyala Mkoani Mbeya.

2f85db3c-f11e-45df-9f50-542218b59432.jpg


DED.jpg

PICHA: Fatuma Latu enzi za uhai wake​
 
Pepo la ajali na nchi yetu, kuna nini?
1.Kuwepo kwa vyombo vya usafiri visivyo kidhi vigezo vya kuwepo barabarani (yani havifai kwa matumizi lakini vipo)

2. Kuwepo kwa madereva wasiokidhi vigezo vya kuwa madereva. Hupelekea kuvunja sheria hovyo.

3. Unywaji wa pombe na matumizi ya dawa za kulevya kisha kuendesha vyombo ya moto.

Hizo nadhani ni sababu kuu.
 



Kuna tatizo hapo
 
Si ni juzi tu Ndg raisi wa Tanganyika alikuwa hapo akitoa maagizo kufuatia ajali iliyotokea?
 
DED wa Igunga Fatuma Latu amefariki dunia muda huu ktk ajali akitokea kwenye kikao cha ALAT Mbeya.

--
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Fatuma Omary Latu na dereva wake wanahofiwa kufariki dunia leo katika ajali iliyotokea katika eneo la Shamwengo, Inyala mkoani Mbeya. Mkurugenzi huyo alikuwa anatoka kwenye mkutano wa ALAT

DED.jpg

PICHA: Muonekano wa gari iliyombeba DED baada ya kupata ajali

DED.jpg

PICHA: Fatuma Omary Latu enzi za uhai wake
 
Kwanini serikali ya CCM haitaki kutanua barabara maeneo hatarishi mkoani Mbeya?

Ajali isipotokea Inyala, inatokea Mlima Nyoka, isipotokea hapo inatokea mteremko wa Mbalizi, lakini serikali inachukulia poa tu miaka nenda rudi.
Ndiyo maana mimi huwa nasema tatizo kuu ni institutional failure..
Imagine kuna TANROAD, TARURA, halmashauri ya wilaya husika, and many more others
 
Kwanini serikali ya CCM haitaki kutanua barabara maeneo hatarishi mkoani Mbeya?

Ajali isipotokea Inyala, inatokea Mlima Nyoka, isipotokea hapo inatokea mteremko wa Mbalizi, lakini serikali inachukulia poa tu miaka nenda rudi.
Juzi Makamu wa Rais alikuwa Mbeya na alitoa agizo kwa TANROADS kurekebisha na kutanua barabara kwenye maeneo korofi sasa sijui hawajaanza kujenga au vp

Sent from my CLT-L29 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom