TANZIA Ajali Mbeya: Watu wanne akiwemo Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wamefariki dunia

TANZIA Ajali Mbeya: Watu wanne akiwemo Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wamefariki dunia

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia huku wengine wakijeruhiwa baada ya Lori kufeli breki na kugonga Magari madogo mawili, katika mteremko wa Inyala mkoani Mbeya.


Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi.

ITV

==============================

Watu wanne akiwemo Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, wadaiwa kufariki dunia hii leo huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya Lori kufeli breki na kugonga magari madogo mawili, katika mteremko wa Inyala Mkoani Mbeya.

pole kwa ndg jamaa na marafiki.
 
Na kale kamteremko ka Inyala kamenyooka kweli kweli kutoka pale kwenye Rail.
 
Kwanini serikali ya CCM haitaki kutanua barabara maeneo hatarishi mkoani Mbeya?

Ajali isipotokea Inyala, inatokea Mlima Nyoka, isipotokea hapo inatokea mteremko wa Mbalizi, lakini serikali inachukulia poa tu miaka nenda rudi.
Mkuu nilikuwa najiuliza kwanii serikali iko kimya juu ya maeneo hatarishi!

Kila siku ajali zinatokea maeneo yale yale, Je kamatai ya Taifa ya usalama barabarani hawaoni hili.

Kitu kingine ambacho ni mzizi hasa kwa Dar es Salaam, Je wameshindwa kubuni njia ya kupunguza ajali hasa maeneo ya mataa yanapokuwa yamezima mfano.
Barabara ya morogoro road maeneo ya taa za Bucha, Baruti Suka ni maeneo ambayo hazipitu siku mbili bila mtu kugongwa au magari kugongana!

Tunahitaji kuja na suluhisho la kudumu kwa maeneo haya, watu tunateketea kila uchwao.

Vyuo kama DIT, St joseph, CoET, MUST, Arusha Tech, VETA mko wapi kuja na suluhisho la taa zinazo dumu!
 
1.Kuwepo kwa vyombo vya usafiri visivyo kidhi vigezo vya kuwepo barabarani (yani havifai kwa matumizi lakini vipo)

2. Kuwepo kwa madereva wasiokidhi vigezo vya kuwa madereva. Hupelekea kuvunja sheria hovyo.

3. Unywaji wa pombe na matumizi ya dawa za kulevya kisha kuendesha vyombo ya moto.

Hizo nadhani ni sababu kuu.
1 na 2 ni kwa kiasi kidogo sanaaa, 3 ndo baba lao
 
Back
Top Bottom