TANZIA Ajali Mbeya: Watu wanne akiwemo Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wamefariki dunia

TANZIA Ajali Mbeya: Watu wanne akiwemo Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wamefariki dunia

1 na 2 ni kwa kiasi kidogo sanaaa, 3 ndo baba lao
Mkuu huwezi kuamini namba moja ndio kubwa kuliko. Magari yanatembea bila kufanyiwa service. Hata ukaguzi mdogo mdogo tu kama pre start watu hawafanyi (hii ni kutokana na kuwa hawana sifa za udereva).

Magari ambayo yapo mengi hapa Tanzania ni magari ambayo yalishaonekana hayafai tena kwa matumizi ya binadamu huko nchi za mwenzetu so huku ni kama dampo tu. Amini kwamba.
 
Watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia huku wengine wakijeruhiwa baada ya Lori kufeli breki na kugonga Magari madogo mawili, katika mteremko wa Inyala mkoani Mbeya.


Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi.

ITV

==============================

Watu wanne akiwemo Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, wadaiwa kufariki dunia hii leo huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya Lori kufeli breki na kugonga magari madogo mawili, katika mteremko wa Inyala Mkoani Mbeya.


Wapumzike kwa amani.

Bahati mbaya ni kuwa tunaongozwa na watu wajinga. Wao hawana kujifunza kokote na kwa lolote.

Ajali Barabarani: Tuzijue sababu, kuepuka upotoshwaji
 
WATU WANNE AKIWEMO MKURUGENZI WA IGUNGA WAFARIKI KATIKA AJALI

Watu wanne wanahofiwa kupoteza maisha hii leo Septemba 14, 2022, akiwemo Mkurugenzi wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora Fatuma Omary Latu na dereva wake huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya Lori kufeli breki na kugonga magari madogo mawili, katika eneo la Shamwengo, Inyala mkoani Mbeya.

Mkurugenzi huyo alikuwa anatoka kwenye mkutano wa ALAT.
#CgOnlineUpdates

Ukiwa hai ishi...

Chanzo CG FM
View attachment 2356845View attachment 2356844View attachment 2356846
 
Ndani ya wiki 3-4 hapo inyala

Lori/ Super rojas ikachomoa watu 20+

Lori / gari ndogo ikiwemo ya jeshi watu 5+

Leo tena Lori na gari ndogo watu 5+

Waliweka utaratibu wa kushuka kwa foleni, yani malori yanakaa kwa muda then yanashuka pamoja lakini naona haijasaidia..
πŸ˜ͺ
 
Huo mteremko Ni balaaaa Sana,Kuna mda Nikifika huko Inyala karibia na Sunrise schools
 
Daaah gari imeisha kabisa sijui ni speeding
IMG-20220914-WA0017.jpg
 
1.Kuwepo kwa vyombo vya usafiri visivyo kidhi vigezo vya kuwepo barabarani (yani havifai kwa matumizi lakini vipo)

2. Kuwepo kwa madereva wasiokidhi vigezo vya kuwa madereva. Hupelekea kuvunja sheria hovyo.

3. Unywaji wa pombe na matumizi ya dawa za kulevya kisha kuendesha vyombo ya moto.

Hizo nadhani ni sababu kuu.
Hizi ni hisia zako. Huna tofauti na waganga wa kienyeji
 
Back
Top Bottom