Ajali Morogoro: Gari liliwekewa Mashada ya Maua na abiria waliomboleza ili kukwepa Doria ya Polisi

Ajali Morogoro: Gari liliwekewa Mashada ya Maua na abiria waliomboleza ili kukwepa Doria ya Polisi

Ni sehemu moja ambayo kwa dereva anayechukua tahadhali hiyo sehemu ni kama ina mvutano hivi hauelezeki, lakini sio sehemu salama sana kwa nguvu tu za kibinaadam, hiyo sehemu nimekuwa nikipita mwili unasisimka kabisa, yaan unastukia tu ushalizua la kuzua. Kuna vipande huwa siviamini kabisa, mikese- moro, segera- tanga- na kipande cha dumila- gairo, huwa naongeza umakini sana njia hizo,
Pale hakupo sawa,gari inahama njia bila kutarajia, sijui kuna nini pale.pana rekodi ajali nyingi sana pale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina uhakika iyo coaster nizile tunazitumia wasafiri wa usiku kwenda mkoani kufata mazao,last week walisema SUMATRA wapo mikese gar ikipita na abiria faini nikuanzia 250,000 kuendelea.

Hii imesababisha madereva kufanya udanganyifu kua wanabeba maiti ili waweze kupita kwenye kizuizi cha sumatra...

Nchi yetu wote jamani,tuijenge pamoja

Hizi coaster zinatusave sana wale wa usiku
 
Hiyo sehem inavutia kukanyaga wese
Pako tofautia sana.

Embu fikiri umetoka huku kasanga umejiachia alafu pale kama pamejificha ivi na mitimiti
Sasa matokeo yake ndo hayo, maafa tyuuh. [emoji24][emoji24]
 
Ni sehemu moja ambayo kwa dereva anayechukua tahadhali hiyo sehemu ni kama ina mvutano hivi hauelezeki, lakini sio sehemu salama sana kwa nguvu tu za kibinaadam, hiyo sehemu nimekuwa nikipita mwili unasisimka kabisa, yaan unastukia tu ushalizua la kuzua. Kuna vipande huwa siviamini kabisa, mikese- moro, segera- tanga- na kipande cha dumila- gairo, huwa naongeza umakini sana njia hizo,
Yaan hapo sijui pana nini hata, duuuh Jah asaidie kwa kweli.
 
Pole kwa wafiwa! mwenyezi Mungu yupo pamoja nanyi
 
Mungu wakati wote hafanyiwi mizaha na dhihaka za kipumbavu, hawa walikaribisha wenyewe mauti na wakadhamiria kabisa abiria wengi wana upumbavu mwingi.

Mimi kuna siku nilimfokea dereva kwa kuendesha ovyo uwezi amini abiria wote walikaa kimya wakaniacha peke yangu na pambana na dereva hadi alipopunguza mwendo baadae wengine ndio wanasema oooh huyu anaendesha lafu.

Usiombe upande gari na abiria mizigo na wasio na uwezo wa kufikiri, utakoma
 
1624368257242.png

Kati ya Makamanda wa Traffic waliokuwa na mbwembwe na vituko katika utekelezaji kazi zao ni Kamanda Fortunatus Muslimu, amabye sasa ni RPC Morogoro.

Barabara karibu nyingi kwenda mikoani huptia mkoa huu, na hivyo huyu kamanda "Nyakua Nyakua" tulitegemea umakini mkubwa katika mkoa huu wa Morogoro.

Tunajua ajali ni ajali, lakini kuna zile za uzembe kama iliyotokea jana , kati ya dala dala na magarimengine hivyo kuchukua uhai sasa tunaamibwa watu saba.

Kamanda Musilimu, Nyakua Nyaua wapi tena?
 
View attachment 1826436

Basi linadaiwa kusababisha ajali jana mkoani Morogoro lilibeba mashada ya maua, dereva aliposimamishwa kwa mwendo kasi alidai Wanawahi Msibani

Taarifa za kuaminika kutoka kwa abiria ni kuwa gari hilo halikubeba maiti na abiria wote waligeuka waombolezaji kila gari liliposimamishwa.

Na taarifa za hivi punde kutoka kwa kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Fortunatus Musilim amesema idadi ya waliofariki dunia imeongezeka kutoka 7 mpaka kufikia 9.

My Take:
Gari ikisafirisha maiti huwa inapewa vibali na kuna nyaraka za kusafiri nazo,JE ZILIHAKIKIWA?, Lakini je Gari yenye maiti inaruhusiwa kukimbia zaidi ya mwendo halali?

Jeshi la polisi msikwepe hili lawama.

====

Watu Tisa wamefariki dunia huku wengine 23 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka katika eneo la Oil Com Manispaa ya Morogoro.
AJALI-MORO-1.jpeg

Ajali hiyo imehusisha magari matatu gari la Abiria Toyota Coster yenye namba za usajiri T686 DUK, iliyokuwa ikitokea Dar es salaam kuelekea Mbeya, Gari ndogo aina ya Crester yanye namba za usajili T563 ASA pamoja na Lori la Mizigo kampuni ya Dangote.

Wako busy kukagua ubovu wa magari. Magari mabovu yako garage.

Ajali ipi imesababishwa na ubovu wa gari?

Dar - Mbeya gari mbovu? Issue ni mwendo kasi kama wa yule OCD wa Kagera!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] majini na yenyewe yako free sahivi, yanatafuta chakula holela tyuuh, kazi iendelee.

Wawekezaji wamerud kwa kasi ya 6G, kule majambaz yametolewa jela, huku wachawi na wao wameruhusiwq kunywa Damu hadharan, ccm mbele kwa mbele
 
View attachment 1826436

Basi linadaiwa kusababisha ajali jana mkoani Morogoro lilibeba mashada ya maua, dereva aliposimamishwa kwa mwendo kasi alidai Wanawahi Msibani

Taarifa za kuaminika kutoka kwa abiria ni kuwa gari hilo halikubeba maiti na abiria wote waligeuka waombolezaji kila gari liliposimamishwa.

Na taarifa za hivi punde kutoka kwa kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Fortunatus Musilim amesema idadi ya waliofariki dunia imeongezeka kutoka 7 mpaka kufikia 9.

My Take:
Gari ikisafirisha maiti huwa inapewa vibali na kuna nyaraka za kusafiri nazo,JE ZILIHAKIKIWA?, Lakini je Gari yenye maiti inaruhusiwa kukimbia zaidi ya mwendo halali?

Jeshi la polisi msikwepe hili lawama.

====

Watu Tisa wamefariki dunia huku wengine 23 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka katika eneo la Oil Com Manispaa ya Morogoro.
AJALI-MORO-1.jpeg

Ajali hiyo imehusisha magari matatu gari la Abiria Toyota Coster yenye namba za usajiri T686 DUK, iliyokuwa ikitokea Dar es salaam kuelekea Mbeya, Gari ndogo aina ya Crester yanye namba za usajili T563 ASA pamoja na Lori la Mizigo kampuni ya Dangote.
Israel uwa habeepiwi...R.I.P ya ukweli waombelezaji
 
Back
Top Bottom